Mmoja Afariki, Wanne Walazwa Wakishindana Kunywa Pombe Moshi

Mmoja Afariki, Wanne Walazwa Wakishindana Kunywa Pombe Moshi

Mtu mmoja amefariki dunia, huku wengine wanne wakinusurika kifo wakati wakishindana kunywa pombe kali aina ya 'Smart Gin', baada ya kuahidiwa kupewa mkate, sukari na Sh50,000 kwa atakayeshinda.

Tukio hilo limetokea Juni 8, 2023 katika kata ya Sanya Juu, wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya watu hao kuahidiwa na mtu anayedaiwa kuwa mfanyabiashara wilayani humo, ambaye sasa ametoroka.

Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwaahidi kuwapa zawadi hizo na mpaka mmoja anafariki walikuwa wameshakunywa chupa tano kati ya tisa zilizokuwa zikishindaniwa.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kunywa chupa tano hali zao zilianza kuwa mbaya na wengine kupoteza fahamu ambapo baadaye waliokolewa kwa kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kupata msaada wa dharura.

Mkuu wa wilaya ya Siha, Christopher Timbuka alimtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Benson Mshiri, mkazi wa Kijiji cha Merad na kwamba waliolazwa hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na muda wowote wataruhusiwa kwenda majumbani.

Mwananchi
Huo mkoa ndo mana viribatumbo haviwaishi kheee.
 
Umasikin ni mbaya sana mungu atusaidie, unadhalilika na kukumbwa na magonjwa nyemelezi Kwa kukosa lishe bora mwisho unakuwa mwehu kama walimu
Mods mpigeni ban ya maisha huyu mtu analidhalilisha Sana kundi la walimu. Au twende mahakamani mkathibitishe wehu wa walimu wa nchi hii? Na kwani mnaruhusu haya kuruka?
 
Mtu mmoja amefariki dunia, huku wengine wanne wakinusurika kifo wakati wakishindana kunywa pombe kali aina ya 'Smart Gin', baada ya kuahidiwa kupewa mkate, sukari na Sh50,000 kwa atakayeshinda.

Tukio hilo limetokea Juni 8, 2023 katika kata ya Sanya Juu, wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya watu hao kuahidiwa na mtu anayedaiwa kuwa mfanyabiashara wilayani humo, ambaye sasa ametoroka.

Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwaahidi kuwapa zawadi hizo na mpaka mmoja anafariki walikuwa wameshakunywa chupa tano kati ya tisa zilizokuwa zikishindaniwa.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kunywa chupa tano hali zao zilianza kuwa mbaya na wengine kupoteza fahamu ambapo baadaye waliokolewa kwa kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kupata msaada wa dharura.

Mkuu wa wilaya ya Siha, Christopher Timbuka alimtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Benson Mshiri, mkazi wa Kijiji cha Merad na kwamba waliolazwa hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na muda wowote wataruhusiwa kwenda majumbani.

Mwananchi
Hao ndio wachaga huwezi kuwakuta wako kwenye mashindano ya riadha au mpira

Wao nashindano yao.makubwa kunywa pombe hasa wanaume

Wanawake wa kivhaga wako poa sana wengi sio chapombe kama wanaume

Mbowe shahidi ninaloongea abishe kama na yeye sio chapombe
 
Mashindano ya kijinga na kipuuzi sana. Classmate wangu moja pia majuzi mwezi April kijijini ametoka shamba kapitia kilabuni kakuta mabishano juu ya nani anaweza kumaliza k-Vant kubwa anunuliwe? Akajitokeza, na njaa yake na ulafi wake akaifakamia within 2minutes kaimaliza na aft10minutes akatapika damu mambonge mabonge ( kwa observation yangu isiyo ya kidaktari ni Maini yamekatikakatika) na akawa no more in20 minutes. Na hadidhi yake ikaishia apo.
So, Friends, ladies and gentlemen pombe si chai, na haina mashindano. Hebu kunywa kiasi kistaarabu utainjoy sana. Haiuzwi kwa aliye chini ya Miaka18. Pole kwa wafiwa, pole sana kwa ambao pia wamepata madhara baada ya kufakamia Gin.
Idd Amin dada" if you overdrank u feel bored , but if u take little alcohol u feel happy & proud !!
 
Back
Top Bottom