Mmoja kati ya Watanzania waliokuwa hawajulikani walipo Nchini Israel, yabainika amefariki Dunia

Sio kweli...

PA inadhibiti sehemu ya west bank (yapo baadhi ya maeneo yanakaliwa na Israel).

Hamas inadhibiti Gaza.

Hotuba hii hapa ya waziri mkuu yenye pointi za kina kuhusu Palestine Authority kutumika kama vikaragasi vya Palestine Authority, Iran n.k huku Mahmood Abbas akiwaza kuwa mfalme mwingine kwa kuidanganya HAMAS kufanya ugaidi

22 September 2023
UN HQ, New York

Hotuba mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA : Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu 2023.

View: https://m.youtube.com/watch?v=kNH85jgzJ0Y

Asante Mheshimiwa Rais!(Wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa)

Mabibi na mabwana, zaidi ya milenia tatu zilizopita, kiongozi wetu mkuu Musa, alihutubia watu wa Israeli walipokuwa karibu kuingia katika nchi ya ahadi. Alisema wangekuta milima yao miwili ikitazamana. Mlima Gerizimu, mahali ambapo baraka kubwa ingetangazwa, na Mlima Ebali, mahali pa laana kuu.

Musa alisema kwamba hatima ya watu ingeamuliwa na uchaguzi waliofanya kati ya baraka na laana. Chaguo lile la enzi ya Musa, limekuwa likijirudia enzi na enzi, si kwa watu wa Israeli pekee. Lakini kwa wanadamu wote. Tunakabiliwa na chaguo kama hilo leo. Chaguo letu litaamua ikiwa tunafurahia baraka za amani ya kihistoria, ya mafanikio na matumaini yasiyo na mipaka, au tutapata laana ya vita vya kutisha vya ugaidi na kukata tamaa.

Nilipozungumza mara ya mwisho kwenye jukwaa hili hili la UNGA miaka mitano iliyopita, nilionya kuhusu madhalimu wa Tehran. Wamekuwa ni laana, laana kwa watu wao wenyewe, kwa eneo letu, kwa ulimwengu mzima. Lakini wakati huo, nilizungumza pia kuhusu baraka kubwa ambayo ningeweza kuona kwenye upeo wa macho.

Hivi ndivyo nilivyosema. Nanukuu: "Tishio la kawaida la Iran limeifanya Israeli na nchi nyingi za Kiarabu kuwa karibu zaidi kuliko hapo awali katika urafiki ambao sijawahi kuuona maishani mwangu."

Nilisema: “Siku ingefika hivi karibuni ambapo Israeli ingeweza kupanua amani nje ya Misri na Jordan hadi kwa majirani wengine Waarabu.” Mwisho wa kunukuu.

Sasa, katika mikutano isiyohesabika na viongozi wa dunia, nilitoa hoja kwamba Israeli na mataifa ya Kiarabu yalishiriki maslahi mengi ya pamoja, na kwamba niliamini kwamba maslahi haya mengi ya pamoja yangeweza kuwezesha mafanikio ya amani pana katika eneo letu la Mashariki ya Kati

Makofi

Asante (kwa makofi) . Naam, mnanipongeza sasa kwa makofi . Lakini wakati ule, wengi walipuuzia matumaini yangu kudhani kuwa ni ndoto za kufikirika. Kukata tamaa kwenu kulitokana na robo karne ya nia ya kuwepo kupatika amani , na lakini ikashindikana. Na kwanini amani ilifeli? Kwani kulikuwepo nia njema? Kwanini siku zote walikutana na kushindwa? Kwa sababu yaliegemezwa kwenye wazo moja la kwamba tusipohitimisha kwanza makubaliano ya amani na Wapalestina, hakuna nchi nyingine ya Kiarabu ambayo ingerekebisha uhusiano wake na Israeli.

Kwa muda mrefu nimetafuta kufanya amani na Wapalestina. Lakini pia ninaamini kwamba hatupaswi kuwapa Wapalestina kura ya turufu ya veto juu ya mikataba mipya ya amani na mataifa ya Kiarabu. Wapalestina wanaweza kufaidika sana na amani pana zaidi. Wanapaswa kuwa sehemu ya mchakato huo, lakini hawapaswi kuwa na kura ya turufu ya veto juu ya mchakato huo.

Na pia ninaamini kwamba kufanya amani na mataifa mengi ya Kiarabu kungeongeza matarajio ya kufanya amani kati ya Israeli na Wapalestina. Tazama, Wapalestina ni 2% tu ya ulimwengu wa Kiarabu. Maadamu wanaamini kwamba 90% nyingine itabaki katika hali ya vita na Israeli, umati huo mkubwa, ulimwengu huo mkubwa wa Kiarabu unaweza hatimaye kutumika kuharibu taifa la Wayahudi.

Kwa hiyo Wapalestina watakapoona kwamba sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiarabu imejipatanisha na dola ya Kiyahudi, wao pia, watakuwa na uwezekano mkubwa wa kuachana na dhana ya kuiangamiza Israel, na hatimaye kuikumbatia njia ya amani ya kweli.

Sasa, kwa miaka mingi, mtazamo wangu wa amani ulikataliwa na wale walioitwa wataalamu wabobezi. Naam, walikuwa na makosa. Chini ya mtazamo wao, hatukuunda mkataba mmoja wa amani kwa robo karne. Walakini, mnamo 2020, chini ya njia ambayo nilitetea, tulijaribu kitu tofauti. Na kwa muda mfupi, tulipata mafanikio ya kushangaza. Tuliafiki mikataba minne ya amani - tukifanya kazi na Marekani, Israel ilitengeneza mikataba minne ya amani, katika muda wa miezi minne, na nchi nne za Kiarabu - Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco.

Makubaliano ya Abraham Accord yalikuwa msingi wa historia. Na leo, sote tunaona baraka za mapatano hayo. Biashara na uwekezaji na washirika wetu wapya wa amani inashamiri. Mataifa yetu yanashirikiana katika nyanja za biashara, nishati, maji, kilimo, madawa, mabadiliko ya hali hewa, na nyanja zingine nyingi. Takriban Waisraeli milioni moja wametembelea Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kila siku, Waisraeli wanaokoa muda na pesa kwa kufanya jambo ambalo hawakuweza kufanya kwa miaka 70 - wanaruka juu ya Rasi ya Arabia bila vikwazo hadi maeneo ya Ghuba, India, Mashariki ya Mbali na Australia.

Mikataba ya Abraham Accord ilileta badiliko jingine kubwa. Iliwaleta Waarabu na Wayahudi karibu zaidi. Tunaiona katika harusi za mara kwa mara za Kiyahudi huko Dubai, katika kuwekwa wakfu kwa shule ya Torati katika sinagogi huko Bahran. Katika wageni wakimiminika kwenye Jumba la Makumbusho la Uyahudi wa Morocco na Casablanca. Tunaiona katika masomo ambayo yanatolewa kwa wanafunzi wa Kiarabu kuhusu historia ya Maangamizi makubwa ya holocaust yaliyofanywa wakati wa Ujerumani ya Hitler katika mitaala ya shule za UAE.

Hakuna shaka. Makubaliano ya Abraham Accord yalitangaza mapambazuko ya enzi mpya ya amani.

Lakini ninaamini kwamba tuko kwenye kilele cha mafanikio makubwa zaidi - amani ya kihistoria kati ya Israel na Saudi Arabia. Amani kama hiyo itasaidia sana kumaliza mzozo wa Waarabu wa Israeli. Itahimiza mataifa mengine ya Kiarabu kurekebisha uhusiano wao na Israeli. Itaongeza matarajio ya amani na Wapalestina. Itahimiza mapatano mapana kati ya Uyahudi na Uislamu, kati ya Jerusalemu na Makka, kati ya uzao wa Isaka na uzao wa Ishmaeli. Hizi zote ni baraka kubwa sana.

Wiki mbili zilizopita, tuliona baraka nyingine zikiibuka. Katika mkutano wa G20, Rais Biden Waziri Mkuu Modi na viongozi wa Ulaya na Waarabu walitangaza mipango ya ukanda maalum wa ushoroba ambao utaunganisha rasi (Peninsula) ya Arabia na Israeli. Itaunganisha India na Ulaya na njia za meli baharini, mitandao ya reli, mabomba ya nishati, nyaya za mawasiliano fiber optic.

Ushoroba maalum (corridor) katika ukanda huu utawezesha kuondoa vituo vya ukaguzi vya baharini, barabarani, ktk reli na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya bidhaa, mawasiliano na nishati kwa zaidi ya watu bilioni 2.

Ni mabadiliko gani ya kihistoria zaidi ya haya kwa nchi yangu. Unaona, ardhi ya Israeli iko katika njia panda kati ya Afrika, Asia na Ulaya. Na kwa karne nyingi, nchi yangu ilivamiwa mara kwa mara na falme geni za mbali katika kampeni zao za uporaji na kutawala nchi za mbali. Lakini leo, tunapobomoa kuta za uadui, Israeli inaweza kuwa daraja la amani na ustawi wa kiuchumi na biashara kati ya mabara haya.

Amani kati ya Israel na Saudi Arabia itaunda Mashariki ya Kati mpya.

Ili kuelewa ukubwa wa mageuzi ambayo tunatafuta kuendeleza, ngoja nikuonyeshe ramani ya Mashariki ya Kati mnamo 1948, mwaka ambao Israeli ilianzishwa. Hapa kuna Israeli mnamo 1948. Ni kanchi kadogo, kilichotengwa, iliyozungukwa na ulimwengu wa Kiarabu wenye uadui.

Katika miaka yetu saba ya kwanza, tulifanya amani na Misri na Jordan. Na kisha mnamo 2020, tulifanya mapatano ya Abraham Accord - amani na nchi zingine nne za Kiarabu. Sasa angalia nini kinatokea tunapofanya amani kati ya Saudi Arabia na Israel. Mashariki ya Kati nzima inabadilika. Tunabomoa kuta za uadui. Tunaleta uwezekano wa ustawi na amani katika eneo hili lote. Lakini pia tunafanya jambo lingine.

Unajua, miaka michache iliyopita, nilisimama hapa na kalamu kuweka alama nyekundu katika ukanda wa Mashariki ya Kati kuonyesha laana, laana kuu, laana ya Iran ya nyuklia. Lakini leo, sasa, ninaleta alama hii kuonyesha baraka kuu, baraka ya Mashariki ya Kati mpya, kati ya Israeli, Saudi Arabia na majirani zetu wengine.

Hatutaondoa tu vikwazo kati ya Israel na majirani zetu, tutajenga ukanda mpya wa amani na ustawi unaounganisha Asia, kupitia UAE, Saudi Arabia, Jordan, Israel, hadi Ulaya. Haya ni mabadiliko ya chanya, mabadiliko makubwa. Alama nyingine ya historia.

Sasa, wakati ukanda wa amani Mashariki ya Kati upanuka, ninaamini kwamba njia ya kweli kuelekea amani ya kweli na majirani zetu wa Palestina inaweza hatimaye kupatikana. Lakini kuna tahadhari izingatiwe. Inapaswa kusemwa hapa, kwa uwazi na nguvu. Amani inaweza kupatikana tu ikiwa umebebwa na ukweli. Haiwezi kutegemea propaganda za uwongo. Haiwezi kuegemezwa kwenye chuki za kusambaza kashfa zisizo na mwisho kwa watu wa Kiyahudi.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas lazima akome kueneza propaganda na njama za kutisha dhidi ya Wayahudi katika Taifa la Kiyahudi. Narudia, nasisitiza , hivi karibuni Mahmoud Abbas alisema kwamba mtawala imla Hitler wa Ujerumani hakuwa anachuki za kuwasakama wayahudi (antisemite) - huwezi kufanya kampeni hizi . Lakini alifanya hivyo. Alisema hivyo.

Na Utawala wa Palestina lazima uache kuwatukuza magaidi, waache sera yake ya kihuni ya kuwafadhili kwa kulipa pesa kwa magaidi wa Kipalestina, kwa ajili ya mauaji ya Wayahudi. Haya yote ni ya kuchukiza, lazima njama hizi zikome ili amani itawale

Na chuki na propaganda hasi dhidi ya Wayahudi lazima zikataliwe popote zinapoonekana, iwe upande wa kushoto au wa kulia, iwe katika kumbi za vyuo vikuu au katika kumbi za Umoja wa Mataifa. Ili Amani idumu, Wapalestina lazima waache kutema chuki kwa Wayahudi, hatimaye wajipatanishe na taifa la Kiyahudi. Kwa hilo simaanishi tu kuwepo kwa taifa la Kiyahudi, bali kwa haki ya watu wa Kiyahudi kuwa na haki ya kiasili kuwepo katika nchi yao ya kihistoria - ardhi ya Israeli.

Na niwaambie, watu wa Israeli wanatamani amani kama hii. Natamani amani kama hii. Wakati nikiwa mwanajeshi kijana, zaidi ya nusu karne iliyopita, askari wenzangu na mimi katika vikosi maalum vya Israeli tulikabili hatari za kufa katika nyakati nyingi kwenye medani nyingi za vita, kutoka kwenye maji ya uvuguvugu ya Mfereji wa Suez, hadi miteremko iliyoganda theluji ya Mlima Hermoni, kutoka nyuma ya Mlima Hermoni. Mto Jordan hadi lami za njia za kuruka ndege uwanja wa ndege wa Beirut Lebanon.

Uzoefu niliopata nikiwa askari mstari wa mbele vitani na mambo mengine njliyoyaona kwa macho yalinifundisha gharama ya vita. Askari mwenzangu aliuawa mita chache karibu yangu na mwingine alikufa mikononi mwangu. Nilimzika kaka yangu mkubwa. Wale wenzangu ambao binafsi wamewahi teseka katika laana ya vita wanaweza kuthamini vyema baraka za amani.

Sasa, kuna vikwazo vingi kwenye njia ya amani. Kuna vikwazo vingi, kwa njia ya makubaliano ya Abraham Accord ya amani ambayo nimeeleza hivi punde. Lakini nimejitolea kufanya kila niwezalo ili kushinda vikwazo hivi, kutengeneza mustakabali bora wa Israeli, na watu wetu wote, watu wote katika eneo letu.

Siku mbili zilizopita, nilijadili maono haya ya amani na Rais Joe Biden. Tunashiriki matumaini sawa kwa kile kinachoweza kupatikana. Na ninathamini sana kujitolea kwake kuchangamkia fursa hii ya kihistoria. Marekani ni mdau muhimu sana katika juhudi hizi. Na kama vile tulivyofanikisha Makubaliano ya Abraham, na uongozi wa Rais Trump, naamini tunaweza kupata amani na Saudi Arabia, na uongozi wa Rais Biden.

Kwa kufanya kazi pamoja na uongozi wa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa ufalme wa Saudia , tunaweza kuunda mustakabali wa baraka kubwa kwa watu wetu wote.

Sasa, mwajua, mabibi na mabwana, mwajua, kuna nzi katika mafuta haya safi. Kwa sababu uwe na uhakika, mahafidhina wakereketwa wanaotawala Iran watafanya kila wawezalo kuzuia amani hii ya kihistoria. Iran inaendelea kutumia mabilioni ya fedha kuwapa washirika wake wa ugaidi. Inaendelea kupanua hema zake za ugaidi katika Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia, Amerika Kusini, hata Amerika Kaskazini.

Walijaribu hata kumuua waziri wa mambo ya nje wa Amerika. Walijaribu hata kumuua mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani. Hii inakuambia yote unayohitaji kujua kuhusu nia ya mauaji ya Iran, na asili ya mauaji ya Iran.

Iran inaendelea kutishia njia za meli za kimataifa baharini , kuwashikilia raia wa kigeni kwa ajili ya kuwakomboa kwa dau la fedha na kujihusisha na kuficha mipango ya kuwa na silaha za nyuklia. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, mgambo wake wauaji wameua mamia na kuwatia mbaroni maelfu ya raia jasiri wa Iran.

Ndege zisizo na rubani na programu za makombora za Iran zinatishia Israel na majirani zetu wa Kiarabu na ndege zisizo na rubani za Iran zimeleta na kuleta kifo na uharibifu kwa watu wasio na hatia nchini Ukraine.

Hata hivyo uchokozi wa utawala huo wa Iran kwa kiasi kikubwa unakabiliwa na hali ya kutojali katika jumuiya ya kimataifa. Miaka minane iliyopita, madola ya Magharibi yaliahidi kwamba iwapo Iran itakiuka makubaliano ya nyuklia, vikwazo hivyo virejeshwa. Kweli, Iran inakiuka makubaliano. Lakini vikwazo havijarejeshwa.

Kuzuia mipango kificho ya hatari ya nyuklia ya Iran. Sera hii ya kujifanya hamnazo ya mataifa na umoja wa mataifa lazima ibadilike . Vikwazo lazima virudishwe. Na zaidi ya yote, Iran lazima ikabiliane na tishio la kushughulikiwa .* Maadamu mimi ni Waziri Mkuu wa Israeli, nitafanya kila niwezalo kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia.

Vile vile, tunapaswa kuunga mkono wanawake na wanaume jasiri wa Iran wanajitokeza kupinga utawala Tehran, ambao wanatamani uhuru. Ambao wameamka kwa ujasiri kwenye vijia vya Tehran na miji mingine ya Irani na wanakabiliwa na kifo. Ni watu wa Iran tuwaunge mkono, sio wakandamizaji wao, maana wamejitolea kupiga ukandamizaji hivyo ni washirika wetu wa kweli kwa mustakabali bora.

Mabibi na mabwana, kama wakati wetu ujao utakuwa wa baraka au laana itategemea pia jinsi tunavyoshughulikia labda maendeleo muhimu zaidi ya wakati wetu. Kuongezeka kwa akili ya bandia AI - Artificial intelligence.

Mapinduzi ya AI yanaendelea kwa kasi kubwa ya kama spidi ya mwanga wa radi. Ilichukua karne nyingi kwa ubinadamu kufikia mapinduzi ya kilimo. Ilichukua miongo kadhaa kufikia mapinduzi ya viwanda. Tunaweza kuwa na miaka michache tu ya kukabiliana na mapinduzi ya AI.

Hatari ni kubwa, na ziko mbele yetu. Kuvurugwa kwa demokrasia, ubongo wetu kuchukuliwa na akili bandia , nafasi za kazi kupunguzwa, kuongezeka kwa uhalifu, na udukuzi wa mifumo yote inayowezesha maisha ya kisasa. Bado kinachosumbua zaidi, ni mlipuko unaowezekana wa vita vinavyoendeshwa na Akili Bandia -AI ambavyo vinaweza kufikia kiwango kisichoweza kufikiria.

Na nyuma ya hii labda kuna tishio kubwa zaidi, kilichokuwa simulizi za kusadikika ya mambo ya hadithi za kisayansi, kwamba mashine za kujifundisha zinaweza kudhibiti wanadamu, badala ya sisi watu kudhibiti mashine. Mataifa yanayoongoza duniani, hata yawe na ushindani, lazima yashughulikie hatari hizi. Ni lazima tufanye hivyo haraka. Na lazima tufanye hivyo pamoja. Lazima tuhakikishe kwamba zama za Akili Bandia ya AI utopia haigeuki kuwa tishio la AI.

Tuna mengi ya chanya ya kupata kupitia Akili Bandia . Hebu wazia baraka za hatimaye kubaini muundo wa kanuni za vinasaba chembe za urithi (gene), kurefusha maisha ya mwanadamu kwa miongo kadhaa, na kupunguza sana magonjwa ya uzee. Hebu fikiria huduma ya afya inayolengwa kulingana na muundo wa maumbile ya vinasaba vya kila mtu, na dawa ya kutabiri ambayo huzuia magonjwa muda mrefu kabla ya kutokea. Wazia roboti zinazosaidia kuwatunza wazee. Hebu fikiria mwisho wa msongamano wa magari, huku magari yanayojiendesha yakiwa ardhini, chini ya ardhi na angani. Hebu wazia elimu ya ziada kujifunza kibinafsi ambayo inakuza uwezo kamili wa kila mtu katika maisha yake yote.

Hebu fikiria ulimwengu wenye nishati safi isiyo na kikomo, na maliasili kwa mataifa yote. Hebu fikiria kilimo cha kisasa zaidi na viwanda vya kiotomatiki vinavyotoa chakula na bidhaa kwa wingi vinavyomaliza kabisa tatizo la njaa na upatikanaji chakula.

Najua huu maneno haya unayosikia ni kama mistari ya wimbo wa mwanamuziki nguli mtunzi John Lennon. Lakini yote yanaweza kutokea.

Hebu subiri kwa punde waza , fikiria kwamba tunaweza kufikia mwisho wa uhaba wa kila kitu!. Kitu ambacho kimeshindikana katika hali ya ubinadamu ndani ya historia yote. Haya Yote ni ndani ya uwezo wetu. Na hapa kuna kitu kingine ambacho tunaweza kufikia. Kwa matumizi sahihi ya Akili Bandia- AI, tunaweza kuchunguza mbingu za mbali kuliko hapo awali na kupanua tunachofahamu zaidi ya sayari yetu ya bluu.

Kwa uzuri au ubaya, maendeleo ya Akili Bandia - AI yataongozwa na mataifa machache, na nchi yangu Israeli tayari iko kati yao. Kama vile mapinduzi ya kiteknolojia ya Israeli yalivyoupa ulimwengu ubunifu wa kustaajabisha, nina imani kwamba Akili Bandia AI iliyotengenezwa na Israeli itasaidia tena wanadamu wote.

Natoa wito kwa viongozi wa dunia kuja pamoja ili kuchagiza mabadiliko makubwa yaliyo mbele yetu. Lakini kufanya hivyo kwa njia ya kuwajibika na ya kimaadili. Lengo letu lazima liwe zaidi kulinda kuwa Akili Bandia- AI inaleta uhuru na sio kiduchu, inazuia vita badala ya kuvianzisha na kuhakikisha kuwa watu wanaishi maisha marefu, yenye afya, yenye tija na amani. Ni ndani ya uwezo wetu.

Na tunapotumia nguvu za Akili Bandia -AI, ngoja kwanza tukumbuke kila wakati thamani isiyoweza kubadilishwa ya ubinadamu na hekima ya mwanadamu. Hebu tuthamini na undani wa uwezo wa huruma, ambao hauwezi kuchukuliwa na nafsi ya Akili Bandia AI

Maelfu ya miaka, Musa aliwapa wana wa Israel chaguo lisilo na wakati na la ulimwengu wote. Angalieni, nimesema mbele yenu hivi leo, baraka na laana. Na tuchague kwa busara kati ya laana na baraka zinazosimama mbele yetu leo. Wacha tutumie azimio letu na ujasiri wetu kukomesha laana ya Iran ya nyuklia na kurudisha nyuma ushabiki na uchokozi wake.

Hebu tulete baraka za Mashariki ya Kati mpya ambayo itabadilisha ardhi ambayo iliwahi kuandikwa kwa migogoro na machafuko, kuwa uwanda wa ustawi na amani. Na tuepuke hatari za Akili Bandia - AI kwa kuchanganya utu, nguvu za akili ya binadamu na mashine, ili kuleta mustakabali mzuri wa ulimwengu wetu katika wakati wetu, na kwa siku zote za mbele. Asante.

*Source : FULL TEXT: Benjamin Netanyahu's 2023 UN General Assembly Speech
 
Hivi Israel ilishindwa kuokoa Mateka mikononi mwa Hamas ?🤔
Mkuu ni kwamba Imeshindwa....Watu 260.....ukiwaganya katikati ya watu 2,000,000....unadhani ni rahisi....Hawas walitegemea majadaliano kama miaka mingine......Hawakutegemea hivi.....In short Israel inajua wazi hao 260 kuwapata itakua kazi, mbele ya kadamamnasi wanasema wanataka warudi....Hawana uhakika kama wapo....Lengo ni kuwapiga Hamas tu...Ili Hamas mbeleni ijue approach hii haifanyi kazi.
 
Netanyau lazima angesema hayo kwa sababu za kulinda maslahi ya nchi yake.
 
Kwanini alitekwa , kwanini hawakumuachia baada ya kumuona anatoka nchi rafiki. Au hawaijui bongo . Sisi tunajipendekeza kwao.
Hilo ndio nilikuwa nalifikiri....Baada ya kutekwa lazima walifanyia interrogation ili wawajue ni kina nani hasa.....Maana utekaji ulikuwa ni random tu....Mateka wengine wangekuwa na faida kwao....kama wanajeshi ili upate siri za kijeshi nk! Sawa hawa vijana wetu baada ya mahojiano wangejua kabisa ni weupe tu, wamekwenda kutafuta maisha. In short mtazamo wangu , kwa upande wa Hamas, hata kwenda Israel kusoma ni kosa kubwa, unakua unaunga mkono Israel!

Kuna watumishi wa ndani toka Thailand, Nepal nk.....Hawa wamekwenda kutafuta maisha tu! Kwa Hamas hilo ni kosa....!
Chochote kilichoko Israel ilikuwa ni military target, ndicho ambacho Israel nalaumiwa....Chochote kilichoko Gaza ni military target....Is just tit for tat.....Anyway vitani ni vigumu kuepuka civilian causalities.......Hii ni vita Mkuu.....
 
Ila wizara haijasema kijana wetu msomi amefariki , Kwa kuuwawa,Ku umwa na ongonjwa,

Yan wizara ya mambo ya tz imeficha
Blender ifiche kwa faida ya nani.......Awe amepigwa mabomu na mashambulizi ya Israel au ameuawa na Hamas....haileti tofauti....Kijana alikuwa nasoma Israel, akatekwa na Hamas.......ndio chanzo cha yote....Swali baada ya kutekwa na Hamas kujua kaenda kutafuta maisha, kwa nini Hamas haikumuachia...? In short labda walitaka awe bargaining chip ambayo walitajaria yatatokea kati yao na Israel. Haya ndi matokeo ya Vita.
 
Sasa kwanini hawasemi kilochomua kijana wetu?
 
Blender ifiche kwa faida ya nani.......Awe amepigwa mabomu na mashambulizi ya Israel au ameuawa na Hamas....haileti tofauti....Kijana alikuwa nasoma Israel, akatekwa na Hamas.......ndio chanzo cha yote....Swali baada ya kutekwa na Hamas kujua kaenda kutafuta maisha, kwa nini Hamas haikumuachia...? In short labda walitaka awe bargaining chip ambayo walitajaria yatatokea kati yao na Israel. Haya ndi matokeo ya Vita.

Magaidi wa HAMAS wana roho mbaya wauaji wa raia.

Israel imefanya mambo mengi mazuri kwa jamii ikiwemo Tanzania

WATOTO SITA WENYE MATATIZO YA MOYO WAENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

MICHUZI BLOG AT MONDAY, DECEMBER 11, 2017 HABARI,

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka watoto sita (6) wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka kumi na tatu nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto, wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana tarehe 10/12/12. Baada ya matibabu ya watoto kukamilika Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.

Taasisi yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto kupitia wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu.Aidha Daktari wetu mmoja bado anaendelea na masomo nchini humo.

Hili ni kundi la tano la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
11/12/2017
 
Naibu Balozi wa Israel nchini Mhe. David Eyal atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)​

07 Nov 2018 -
Naibu Balozi wa Israel nchini Mhe. David Eyal atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya.

Mhe. Eyal David alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.
 
Magaidi ya HAMAS na Iran wanatafuta upenyo wa kila aina na sababu za kiimla kuangamiza raia.

TOKA MAKTABA :
President's Office and Chairman of Revolutionary Council, Zanzibar

NEWS AND EVENTS​

Ujio wa Madaktari kutoka Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya ‘Save a Child’s Heart’ ya nchini Israel unaisaidia sana Serikali kuondokana na gharama kubwa ya matibabu ya Ugonjwa wa moyo 19 Sep 2022​

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Ujumbe wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Nchini Israel, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ujio wa Madaktari kutoka Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya ‘Save a Child’s Heart’ ya nchini Israel unaisaidia sana Serikali kuondokana na gharama kubwa ya matibabu ya Ugonjwa wa moyo unaowakabili watoto hapa nchini.

Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na timu ya Madaktari wa Upasuaji wa magonjwa ya moyo kutoka Israel, ulioongozwa na Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo Tamar Shapira.

Amesema hatua ya Madaktari hao ya kuja nchini kila mwaka na kuwachunguza watoto wanaotatizwa na ugonjwa wa moyo na hatimae kusafirishwa hadi Israel kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji, imeisadia sana Serikali kuondokana na gharama kubwa ya matibabu ya wagonjwa hao.

Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru madaktari hao kwa kushirikiana na Serikali na kufanya kazi kubwa wanayofanya ya kunusuru maisha ya watoto wa Zanzibar wanaokabailiwa na ugonjwa wa moyo.

Alisema Serikali haina uwezo wa kutosha wa kuwahudumia watoto wote wanaokabiliwa na changamoto ya ugonjwa huo kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo hilo linalowakabiliwa watoto wengi.

Aidha, alisema mradi unaolengwa kutekelezwa wa ujenzi wa kitengo cha matibabu ya moyo kwa watoto , utasaidia juhudi za Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuzingatia kuwa hatua hiyo utatoa fursa kwa wataalamu kutoka nje kuja kufanya operesheni ndogo ndogo pamoja na kuwajengea uwezo watendaji.

Aliiomba Jumuiya hiyo kusaidia upatikanaji wa taaluma kwa madaktari ili hatua hiyo iende sambamba na uwepo wa kitengo hicho pale kitakapokamilia.

Naye, Mkurugenzi wa Jumuiya ya ‘ Save a Child’s Heart’ Tamar Shapira aliahidi Jumuiya hiyo kuendelea kushirikiana na Serikali kwa lengo la kuhakikisha inakabiliana na tatizo la ugonjwa wa moyo linalowakabili watoto wa Zanzibar.

Mkurugenzi huyo amepongeza mashirikiano makubwa waliyoyapata kutoka Uongozi wa Wizara ya Afya katika kipindi chote wakiwa nchini na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliowasilishwa kwao.

Mapema, Waziri wa Afya Ahmeid Nassor Mazrui alisema Madaktari wa Jumuiya hiyo wamekuwa na utaratibu wa kuja nchini kila mwaka na kushirikiana na Wizara Afya kwa ajili ya kuwachunguza watoto wanaokabiliwa na ugonjwa wa moyo, kufuatilia maendeleo yao pamoja na kuwafanyia upasuaji.

Alisema Wizara Afya kwa kushirikiana na Serikali ya Norway ina azma ya kujenga Kitengo cha Matibabu ya moyo, katika jengo litakalokuwa na mahitaji yote muhimu ikiwemo vifaa, ikiwa ni hatua ya kuyahami maisha ya watoto wa Zanzibar wanaokabiliwa na ugonjwa huo.

Madaktari wa Upasuaji kutoka Jumuiya ya ‘Save a Child’s Heart’ wamekuwa na utaratibu wa kuja nchini kila mwaka kwa ajili ya kuwachunguza watoto wanaokabiliwa na ugonjwa wa moyo, wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi 17, ambapo tangu utaratibu huo kuanza mnamo mwaka 1999, jumla ya watoto 780 wamefanyiwa upasuaji
 
Ni aibu Sana serikali yetu ,kukaa kimya,
Watoto wetu wametekwa , na mmoja tayar kafariki
 
"Wizara itaendelea kuwaailiana na Israel ili kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa salama"
Nje ya mada: Kijana alifia Gaza au Israel?
Kifo chake kimetokea lini na sababu ya kifo ni nini?

Off course ni ugaidi wa hamas ndio umesababisha haya. Bila hamas kuteka raia na kukimbilia huko Gaza hii vita isingetokea
 
Back
Top Bottom