Mnaoamini kuwa uchawi upo mnatumia vigezo gani?

Mnaoamini kuwa uchawi upo mnatumia vigezo gani?

Biblia haiwezi kuandika kitu ambacho hakipo.

Vitabu vya dini vimetaja uchawi mara nyingi sana

Unasema Biblia haiwezi kuandika kitu ambacho hakipo ila biblia hiyo hiyo imeandika nyoka anaongea. Je ni kweli nyoka huwa anaongea ?
 
Uchawi upo au haupo??

Kuna kesi ilitokea hapa Zanzibar, jamaa wakaenda kwa mtaalamu ili awasaidie.Mtaalamu akasema aletwe ngamia!

Mtaalamu akaanza kumsomea yule ngamia, ngamia akaanza kuzama chini ya ardhi kisha akapotea kabisa! Namaanisha alizama na kupotea.Mimi ni shuhuda mwenyewe!

Unakumbuka mkasa wa nyumba kuzama yenyewe hapa Zanzibar?? Unaifahamu ardhi ya Zanzibar?? Imejaa miamba, lakini nyumba ilizama!

Hivi visa ni maarufu huku Zanzibar! Ni uchawi au miujiza??Utajua mwenyewe!

Hii dunia ina mengi ambayo mimi na wewe hatuyafahamu na hatuwezi kuyafahamu mpaka tunakufa. Elimu ni bahari.

Ukipata kishahada chako unajihisi kama unaifahamu dunia, kumbe ni ushamba, ulimbukeni, kiburi, majivuno, mhemko, papara, dharau n.k ndivyo vimekutawala!

Nb: Toa elimu kuhusu huyo ngamia kuzama ardhini au nyumba kuzama kwenye miamba wakati wa kiangazi!Kwa taarifa yako wataalamu walikuja na hawakupata majibu.Ebu wewe tueleze ni kitu gani hiki!

Wahenga wenzangu watakuwa wanakumbuka kuhusu hii nyumba kuzama kwani ilitikisa vyombo vya habari!

Weka ushahidi ulionyooka kuhusu hilo tukio la ngamia kuzama.

Taja jina la mtaa, kijiji, kata, wilaya na mkoa ambao hilo tukio lilitokea. Na namba ya nyumba kisomo kilipofanyika

Taja tarehe ambayo tukio lilitokea

Taja jina la mganga aliekuwa anamsomea ngamia mpaka akazama.

Pia Taja mmiliki wa nyumba iliyozama ardhini, mtaa , wilaya, na mkoa. Na tarehe ambayo nyumba hiyo ilizama.

Toa hizo taarifa zote ili tupeleleze tuthibitishe kama ni kweli ama uongo
 
Uchawi upo, narudia tena upo. Yamkini umekulia maisha yako yote mjini afu haujawai kujua shida yoyote. Uchawi upo narudia tena, dhana ya kwenda benki kuiba sidhani kama umeishughulisha akili yako kufikiria vizuri. Uchawi ni suala la kiroho.
 
Kama huamini uchawi basi wewe ndo mchawi mwenyew au huishi hapa Duniani.

Hapo majuzi tumesikia mtoto mwenye uarobino kayliwa kikatili na kutolewa baazi ya viungo.

Je unadhani hao waliofanya hivo wanajiburudisha tu? Au huyo anayevihitaji hivo vitu anajiburudisha tu mwenyew?
 
Katika miaka niliyo nayo mpaka sasa sijawahi kukubali kuwa eti kuna uchawi sijui mtu anaweza kuloga sijiui mambo yako yasiende.

Kama kweli uchawi upo kwanini hao wachawi wasiende benki wakaloga wakachukua pesa.

Kama kuna mtu humu ndani alishawahi kulogwa njoo utupe mrejesho ilikuwaje.

Pia, kama kuna mtu anajiamini anaweza kuniloga njoo uniloge we taja unachotaka kutoka kwangu nitakupa we niloge kama kweli unaweza😂😂

Mwisho hakuna uchawi ni dhana za kufikilika tu.
Ukipata jibu la kueleweka kimantiki ni tag mkuu.
 
Kama huamini uchawi basi wewe ndo mchawi mwenyew au huishi hapa Duniani.

Hapo majuzi tumesikia mtoto mwenye uarobino kayliwa kikatili na kutolewa baazi ya viungo.

Je unadhani hao waliofanya hivo wanajiburudisha tu? Au huyo anayevihitaji hivo vitu anajiburudisha tu mwenyew?
Uchawi ni nini?

Unakubali kuwa inawezekana kukawa na imani ya kitu bila ya hicho kitu kwapo?

Mfano, mtu anaweza kuamini kuna pembetatu duara, wakati pembetatu duara haipo?

Kama hilo linawezekana, kuamini pembetatu duara ipo kunaifanya iwepo kweli?

Wewe ukiamini kuwa ni bilionea wa kwanza kwa utajiri duniani, imani hiyo inakufanya uwe bilionea wa kwanza duniani?
 
Kama huamini uchawi basi wewe ndo mchawi mwenyew au huishi hapa Duniani.

Hapo majuzi tumesikia mtoto mwenye uarobino kayliwa kikatili na kutolewa baazi ya viungo.

Je unadhani hao waliofanya hivo wanajiburudisha tu? Au huyo anayevihitaji hivo vitu anajiburudisha tu mwenyew

Hizo bangi unazovutaga pumzika kwanza ndio maana serkali inakatza kulima bangi Kwa watu kama wewe
 
Bangi ni dawa iliyohalalishwa na serikali huku nchi zilizoendelea.

Ni wewe tu masikini wa akili unayeishi kwa kukariri unaona kumsema mtu mvuta bangi ni kejeli.

Thibitisha uchawi upo kweli.
 
Sijasoma hiyo link.

Nataka nikuambie tu kuwa hata wazungu zamani walikuwa wanaamini ushirikina.

Walikuwa kuevolve fasta wakaachana na hizo imani.

Hizo mnazoona nyie ni mazingaombwe sijui miujiza kule china wanasoma kama kozi mtu anagraduate.
Kwa hiyo uchawi upo ikiwa mpaka unasomewa!?.. tofauti na mnavyodai 'mliostaarabika' kwamba haupo?
 
Acha uongo wa kijinga wewe. Humu kuna watu wazima wengi.

Taja jina la benk, taja siku ya tukio. Watu tukapeleleze.

Acha story za kutunga tunga tu
Ni kwa sababu siku hizi watu mnaamini Sana uongo kuliko ukweli kiasi hata mkiambiwa ukweli hamuukubali especially kama unahusu mlengo usioufuatilia.

Siku zote ujue kwamba katika Yale unayojua yapo mengine usiyojua, ndo hayo sasa. Endelea kujifunza
 
Huna SPIRITUAL POTENTIAL.

Si ajabu wewe ni BOKSI TUPU kwa ndani na kwa nje, AN EMPTY SHELL WITH NO SPIRITUAL VALUE.

Wanalogwa waliobeba vitu vizito ndani, na sio MAGARASA.

You cannot BEWITCH a BOX FOR it is devoid of energies and TRUE LIFE FORCE.

Cc: Pascal Mayalla Namba Moja ajaye nchini DR Mambo Jambo min -me mimi_ni_mshamba Kapeace

Another goal post move. Y'all come with all types of excuses but proof.

Nimesema naomba uthibitisho wa ushirikia, mloge mwenye potential kama mimi hamuniwezi maana ni dhahiri sasa uchawi wenu hauna nguvu. Paa na ungo, penya ukutani kila mtu aone to prove your point yote hamuwezi, sasa mnaweza nini?

Mimi nachotaka ni proof in any way, shape, or form.

Mna story nyingi sana ila vitendo sifuri. Inabidi uwe zwazwa pro kuamini ushirikia upo.
 
Hakuna proof yoyote wala siwajibiki kutoa proof popote.

Haya ni maelezo matupu yasiyo na uthibitisho wowote, unaweza kuyapuuza kwa wakati wowote ukitaka. Huwajibiki kuyaamini kwa namna yoyote.

Ndio demokrasia. HAKI ZA BINADAMU.

Hata ukichagua kuwa MJINGA ni HAKI YA BINADAMU pia.
 
Weka ushahidi ulionyooka kuhusu hilo tukio la ngamia kuzama.

Taja jina la mtaa, kijiji, kata, wilaya na mkoa ambao hilo tukio lilitokea. Na namba ya nyumba kisomo kilipofanyika

Taja tarehe ambayo tukio lilitokea

Taja jina la mganga aliekuwa anamsomea ngamia mpaka akazama.

Pia Taja mmiliki wa nyumba iliyozama ardhini, mtaa , wilaya, na mkoa. Na tarehe ambayo nyumba hiyo ilizama.

Toa hizo taarifa zote ili tupeleleze tuthibitishe kama ni kweli ama uongo

Mkuu, utapigwa chenga zaidi ya Messi hawezi kutaja jina la mtaa tu. Hawa watu wanaamini story za hearsay ukiwauliza uthibitisho ni maneno tu hata kitu kidogo tu kama jina la mtaa hawawezi.

Mwaka juzi kuna mtu alileta uzi hapa hapa jukwani kwamba kuna DIWANI Kigoma alifanywa msukule. Kama kawaida nyumbu wa JF wakaamini ile story pale pale, mimi niliomba kitu kimoja tu jina la huyo diwani. Nilisema yeyote atayenipa jina la diwani nitampa 500k TSH. Hadi leo jina tu la diwan sijapata na diwani ni ofisi ya umma mtu kufanya jina siri.

Hakuna proof yoyote wala siwajibiki kutoa proof popote.

Haya ni maelezo matupu yasiyo na uthibitisho wowote, unaweza kuyapuuza kwa wakati wowote ukitaka.

Ndio demokrasia. HAKI ZA BINADAMU.

Hata ukichagua kuwa MJINGA ni HAKI YA BINADAMU pia.

Huo ujinga wa kuamini bila proof ndo watu wenye akili timamu hatuutaki. Kuaminishana story za hearsay ni uzwazwa.
 
Back
Top Bottom