Mnaofanya mazoezi ya kukimbia kuna mambo mnadanganya

Uzito haupungui kwa kufanya mazoezi.Uzito unapungua kwa kupunguza sana wanga na idadi ya milo kwa siku.Kula angalau mara moja kwa siku( 24Hrs) mlo sahihi.Ukiweza kula milo mitano kwa wiki.
Achana na soda,juice na pombe.
Kula matunda yasiyo na sukari nyingi kwa kiasi sana.
Ukiweza achana na wanga kama vile ugali,wali,chapati na ndugu zake,mihogo na viazi vyote.Kula mboga za majani na protini.
Ukishindwa kufanya hivyo hutaweza kupungua.
Njia iliyobaki shika jembe ukalime - hapa lazima upungue.Hili zoezi la jembe ndilo aerobic ya ukweli kuliko zote
 
Hilo la vyakula inatakiwa wenye maisha mazuri. Sisi wengine tunakula kuzuia tu misiba. Ni watanzania wachache sana wanaoweza kuachana na wanga.
 

Ukitaka kupungua inabidi ujinyime kula.
 
Huwezi kuanza na kukimbia 10+km Siku ya kwanza. Tunaanza taratibu hadi kufikia hizo km, mimi saivi nakimbia 7km ila lengo ni kufikia 15 km. Nataka niwe nakimbia km 60 kwa wiki hivyo nikifikia 15km kwa siku nitakua nakimbia siku nne tu kwa wiki.
Kingine consistency wakimbiaji wengine ni wa mchongo anakimbia siku tatu anapumzika miezi miwili sasa hizo km 10+ utaendelea kuzisikia tu na wala hutapungua.
 
Ni kweli mkuu. Mimi sasa hivi nimefikia uwezo wa 2.25km kwa 15 minutes leo jioni nikienda tena nataka niende zaidi ya hapo.
 
HUWEZI kufika Darasa la Saba kama hujaanza Darasa la kwanza.

Ili Ufike Darasa la Saba Lazima upite Darasa Moja Baada ya jingile.
Uhesabu 1,2,3,4,5,6,7..... Nk
HUWEZI ukaanza 100
Bila kuanza na Moja

Darasa la kwanza.
Darasa la Pili.
Dara sa la Tatu.
Darasa la Nne.
Tano, SITA, Saba
Form one
Two , three na four.

Form five six Hadi chuo.

Anza KUKIMBIA MITA 10
Then 20.
Halafu 30.

Baadaye kilomita 1,2,3. ....... Hadi 50
HUWEZI ukafika miaka mia bila kuwa na Miaka 1,2,3,4,5
Hakuna kuruka stage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…