Mnaoishi Dar, eneo gani unalisikia ila hujawahi kufika?

Mnaoishi Dar, eneo gani unalisikia ila hujawahi kufika?

Duuh mimi ninavyopenda kuzurura sehemu nyingi sana nimefika hadi Kimbiji kule Kigamboni nimefika yani kama siku siendi kazini na sina ratiba yoyote niko tu home, nikiona nimeboreka nafunga safari naenda tu sehemu yoyote Dar ambayo ni ya mbali natafuta mahali nakaa nakula, nakunywa, nabarizibarizi then huyo narudi zangu home, sehemu ambazo sijafika nyingi ni za manispaa ya Temeke huko sijui Chamazi sijui Kisewe yani kwa kifupi ukanda huo wote huwa naona umekaa kushoto sana
 
Naomba nikija niwe mgeni wako unilee kwa mwezi mzima mana sina mwnyw huko Daslamu
Wewe kijana wa hovyo huchelewi kutongoza mama mwenye nyumba wako.
Na kama si mimi basi ukiondoka dada wangu wa kazi ana ujauzito.
 
Kuna mwana nilisoma naye alikuwa anakaa Oysterbay, nimekutana naye US, alikiwa hapajui Buguruni wapi.

Nilimcheka sana mpaka aliporudi likizo ilibidi aende Buguruni kupaona.

Unakaaje Dar halafu Buguruni hupajui?
Jamani, we chukulia mtu umekulia Oysterbay, unafika Buguruni kivipi na kufanya nini?
 
Kuko shwari mkuu, maeneo mengi dar ule wizi na ukabaji wa kijinga umepungua labda uwafate wahuni kwenye angle zao na mida mibovu hapo utakua unatafuta lawama.

Ila umakini ni muhimu pia.
Kivule uwizi vibaka hakuna
Aise wakikamata mwizi kule anavanikwa
Pale kwa mpemba mbele kdg unaingia kulia kuna mji fulani safi sana watu wamejenga kwa mipango kuko poa sana

Ova
 
Duuh mimi ninavyopenda kuzurura sehemu nyingi sana nimefika hadi Kimbiji kule Kigamboni nimefika yani kama siku siendi kazini na sina ratiba yoyote niko tu home, nikiona nimeboreka nafunga safari naenda tu sehemu yoyote Dar ambayo ni ya mbali natafuta mahali nakaa nakula, nakunywa, nabarizibarizi then huyo narudi zangu home, sehemu ambazo sijafika nyingi ni za manispaa ya Temeke huko sijui Chamazi sijui Kisewe kwa kifupi ukanda huo huwa naona umekaa kushoto sana
Inapendeza sana 🙌 👌
 
Mburahati ndo wapi?
Mburahati ni jirani na manzese, kama unaelekea magomeni mkono wa kushoto ndanindani huko au kutoka chuo cha usafirishaji kama unaelekea mjini kule ndio mburahati huko ni uswazi sana.
Dar mimi sijafika chamanzi ,na yombo ila asilimia kubwa ya dsm naifahamu na nimeshafika dar sehemu ambayo sijafika ni njia ya kusini iliishia mbagala zakhem.
Ila sijui ubungo,kimara mbezi napajua,
Mwenge mbezi beach mlalakua, mbezi beach ya chini kule kwa zena, hanghover, target, kidimbwi, ramada, jangwani seabreez, tegeta, kunduchi hadi kunduchi beach hotel, wazo kule kiwanda cha cement hadi bagamoyo napafahamu, kinondoni, mwanamyamala,makumbusho, kijitonyama, magomeni,sinza, upanga oysterbay,masaki mikocheni,posta, kariakoo napajua buguruni tandika buza ,kwa mama kibonge kwa lulenge, kinyerezi ukonga napajua ,tabata segerea,senene ,gereza la segerea kilungule, napajua ,udsm,ardhi university changanikeni makongo juu napajua ,kigamboni nishazukuka hadi kulle dar es salaam zoo. mbutu, kibada, chuo kikuu cha wakorea, daraja la nssf, dege village
Ukiwa na gari binafsi na unapenda kutembea utazunguka sana dar
 
Back
Top Bottom