Mnaoishi Dar, eneo gani unalisikia ila hujawahi kufika?

Mnaoishi Dar, eneo gani unalisikia ila hujawahi kufika?

Mburahati ni jirani na manzese, kama unaelekea magomeni mkono wa kushoto ndanindani huko au kutoka chuo cha usafirishaji kama ubaelekea mjini kule ndio mburahati huko ni uswazi sana.
Dar mimi sijafika chamanzi ,na yombo ila asilimia kubwa ya dsm naifahamu na nimeshafika dar sehemu ambayo sijafika ni njia ya kusini iliishia mbagala zakhem.
Ila sijui ubungo,kimara mbezi napajua,
Mwenge mbezi beach mlalakua, mbezi beach ya chini kule kwa zena, hanghover, target, kidimbwi, ramada, jangwani seabreez, tegeta, kunduchi hadi kunduchi beach hotel, wazo kule kiwanda cha cement hadi bagamoyo napafahamu, kinondoni magomeni,sinza, upanga oysterbay,masaki mikocheni,posta, kariakoo napajua buguruni tandika buza ,kwa mama kibonge kwa lulenge, kinyerezi ukonga napajua ,tabata segerea,senene ,gereza la segerea kilungule, napajua ,udsm,ardhi university changanikeni makongo juu napajua ,kigamboni nishazukuka hadi kulle dar es salaam zoo. mbutu, kibada, chuo kikuu cha wakorea, daraja la nssf, dege village
Kweli wewe ni mwenyeji 🙌
Ukiwa na gari binafsi na unapenda kutembea utazunguka sana dar
Ila hapa wenye macho yao watakuwa wamesoma hiyo sehemu ya "kuwa na gari binafsi" tu 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Huku nako ni wapi?
Haha Bagamoyo moja hiyo ila mi najua Makurunge hiyo kwa kivuzi sijawahi isikia, japo inawezekana ipo maana Bagamoyo nayo ina majina ya ajabu kuna sehemu inaitwa Ukuni, ukiwa mtafutaji wa viwanja hasa ukanda huu wa Dar na Pwani utajua majina ya sehemu nyingi
 
Kila sehemu za jiji umefika kwa shughuli za kikazi au matembezi binafsi?
Matembezi tu, mimi na babe wangu hua na desturi ya kujaza mafuta na kutembelea jiji letu na viunga vyake lakini pia tunaweza kunyoosha goti tukavuka mipaka ya jiji na kuingia miji mingine (RoadTrip) tunaenjoy nature na kuona tamaduni mbali mbali.
 
Haha Bagamoyo moja hiyo ila mi najua Makurunge hiyo kwa kivuzi sijawahi isikia, japo inawezekana ipo maana Bagamoyo nayo ina majina ya ajabu kuna sehemu inaitwa Ukuni, ukiwa mtafutaji wa viwanja hasa ukanda huu wa Dar na Pwani utajua majina ya sehemu nyingi
Kuna mitaa hapo bagamoyo panaitwa nia njema pako vzr sana

Ova
 
Kuruzula muhimu sana unajuwa maeneo mengi na kuna watu wako pembezoni wanaishi bana

Ova
Kuna mwana alikuwa ananizimia sana Tambaza kuna siku akasema wewe leo nakupeleka kwetu Mburahati hujawahi kufika huko.

Tukaenda Mburahati mpaka kwao sikuamini pale ni Dar es salaam wala si mbali na Magomeni.

Nilikuwa sijawahi kufika.
 
Haya ni maeneo ya Dar kweli?
Mkuu kwani we ni mgeni Dar mbona kuna maeneo kataja hapo ni karibu na mjini kabisa hata kama hujawahi fika hayo maeneo, kama ni mwenyeji wa hili jiji basi lazima utayasikia tu mfano hiyo Bombom kijiwe samli iko Kiwalani ila huko Zingiziwa ndio mbali ni karibu na Chanika, huko Kifuru ni karibu na Kinyerezi ndio kuna barabara ya kuenda Mbezi mwisho halafu Mbopo pia nayo ni mbali iko Mabwepande huko
 
Back
Top Bottom