Mnaojua aina za Roho Mbaya zenye Ukatili na Udhalilishaji wa Kisiasa ndani yake, hii inaitwaje?

Mnaojua aina za Roho Mbaya zenye Ukatili na Udhalilishaji wa Kisiasa ndani yake, hii inaitwaje?

Ni madaktari!

Au kuna tatizo daktari kumsindikiza mgonjwa?

Hujaona kule kwa PM Boris?!!!
Rejea kauli yako hii 👇👇

Huyo atakuwa siyo daktari kitaaluma!

Daktari unapokeaje shinikizo lisilo la kitaaluma?
ambayo ilikuwa majibu ya posti yangu 👇👇

Usijitoe ufahamu bwashee, hakuna daktari mweledi na anayeijua vema kazi yake anaweza kumruhusu mgonjwa aliye katika hali hiyo kuongea na media kama hakukuwa na shinikizo toka juu...

Mitano tena...
 
Wakati mnazusha kafa ,?kwanini asitoke hadharani athibitishe yu hai?,kuondoa sintofahamu kwa wapiga kura wake?
Mkuu kwanza jifunze kujibu hoja bila kujumlisha mtu.

Kupinga Jambo si kwamba mtu anakuwa kashiriki.

Ni ujinga, upumbavu, na kukosa akili kuanza kubishana na watu wanakuzushia umekufa wakati wewe upo hai!! Na ilhali bado unahitaji utulivu wa mwili na akili ili upone vizuri.

Hivi tukiamua kila mtu awe anawaprove wrong wanaomsema vibaya unadhani Kuna Jambo litafanyika?

Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Mzee angetulia apone vizuri tungemuona kwenye shughuli zake.

Hoja ambayo Ina mashiko kidogo ni kusema kalazimishwa Ila sio eti kuwakanusha watu......
 
Kwani pale alikuwa ofisini kwake?
mpango2.jpg
mpango.jpg

HILO lipo wazi hapa ni chumba cha mikutano ofisini kwake, tazama mazingira ya hiyo picha ni mazingira ya home hayo hapana, lakini pia waliomzunguka ni madaktari, hii inathibitisha kuwa bado ni mgonjwa anafaa kuwa hospitari,sasa anaharaka ya nini?
 
Kalazimishwa na Farao.Farao ukikataa jambo lake anakuua.Kuna mambo mengi hujui,huwezi amini kuwa kilichomuua Maalim wala siyo Corona.Farao alitumia loophole ya Corona kumuua Maalim.Farao ni muuaji ambae huwa hana utani.
Only Genius people can understand you.
 
Huyu baba ni mgonjwa tuwe wakweli na tuache kumumunya maneno.
Dr, jipumzishe home kwako hadi afya yako itengamae kaka.
 
Unajuwa uongo ukisemwa sana na pasitokee mtu wa kukanusha watu hufikilia kuwa ndio ukweri huo hivyo kama binaabu ndipo muda mwingine tunaingia ktk kulaumiwa ktk kutafuta kukanusha uongo ulionea
Kwa hiyo Mpango haugui,umemuona hali yake hapo?
 
Dr. Mpango ni mgonjwa. Na Kama akipona atahitaji muda mrefu wa kupumzika huku maendeleo yake yakiwa na close monitoring.

Haukuwa muda wa kusema narudi kazini kufanya kazi za Taifa kwa nguvu. Taifa lipo tu, Ila uhai na afya zetu, Ni vya muda mfupi.

Ningekuwa mimi, neno langu muhimu, ingekuwa Ni kuwaomba wote wenye upendo nami, wazidi kuniombea ili tiba niipatayo ifanye kazi maana hata hiyo tiba Ni kazi ya Mungu kwa kupitia watu wake aliowajalia karama mbalimbali ili tutegemeane.

Hakuna aliye shujaa kwa maradhi au kifo, ndiyo maana huwezi kusema nimekishinda kifo.
 
Kwani BM hospitali hawana chumba cha mkutano?
UKO sahihi yupo chumba cha mikutano hospitali ya BM swali langu la kujiuliza bado halijapoteza maana kulikuwa na sababu ganiza msingi kwa mgonjwa kama kujitokeza mbele ya waandishi wa habari kueleza aliyoeleza,kwa mujibu wa maelezo yake chanzo TBC habari alikuwa anakanusha kuwa yeye mgonjwa yuko fit na ameanza kuchapa kazi,hiyo ni hali ya mtu kuchapa kazi kweli?
 
Back
Top Bottom