Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Mnaokaa Uswahilini (Wilaya ya Temeke) Mungu awafanyie wepesi ndugu zangu. Jana machozi yalinitoka

Hakuna habari ya fixed budget hapa , jamaa ni choka mbaya ila ni ile ya nyani haoni kundule.
Hata kama hana pesa mfukoni si mabanda ya mawakalanwa huduma za M pesa tigo pesa yapo kila mahala.
Si anageenda kuwatolea hata 5000 watoto wamalize siku vizuri na yeye akapata thawabu kwa Mungu?
Nyie watu 🏃🏃🏃
 
Mimi supu ya miguu ya chair fire sijawai kula.
Na roho nyepesi kongoro haipiti kabisa kwenye koo...japo Jana nimepiga mdudu wa kukausha nikapiga na spirit kidogo siku ikapita
Mzee wangu kwa kipindi Cha 2010' alikuwa butcher man afu pia anajua catering

So kwenye kuandaa ana andaa mwenyewe anajua vizuri

So yeah!! Inakuwa Bomba tuu

Japo mdudu mtamu siku hz simgusi namwona kwa mbali tuu 😂 😝😋😋
 
Mimi ninakaa Wilaya ya Ilala. Jana nilikuwa Wilaya ya Temeke nilishuhudua mida ya mchana badala ya mama kuwapikia watoto (watoto walitoka kucheza wakaja kulalamika njaa) akawapa 500 wote wawili wakanunue bagia na askrimu (ice cream) na ndio imetoka hiyo mpaka Usiku, kulingana na maelezo ya mwenyeji wangu. Sema na mimi nilikuwa majalala, nilibakiwa na nauli tu, laiti kama ningekuwa na kitu chochote ningeweza kuwaongezea hata 500 nyingine aisee.

Kama hauna pesa ya kumsaidia mtoto masikini, basi mkumbuke hata wakati wa sala au swala.

Daah, uswahilini panatisha wadau, hususan kwa watoto wadogo.
Kweli mkuu, mambo magumu,nafuu hata kijijini!
 
Back
Top Bottom