Mnaolinganisha mafanikio ya Rais Samia na Rais Nyerere, huenda mna tatizo la afya ya akili kwa kutozingatia ukweli huu hapa

Naomba tuhuma zao za ufisadi, kumteua mtu kwa uwezo wake siyo kosa, Nyerere angekuwa na upendeleo wa kwao angeacha Musoma kuna lami, chuo kikuu na mengine mengi. Ndiyo alikuwa na madhaifu yake lakini siyo kama hawa, kwanini madini hakugusa wala kuuza mali za taifa? ndiyo Rais pekee aliweza kupunguza mshahara wake na alikuwa anaenda kwenye midahalo UDSM sasahivi hata DC hawezi kuandaa mdahalo, nchi gani inaweza kuendelesha bila mijadala/midahalo?
Midahalo ina faida zipi ikiwa haina uwezo wa kuja na ubunifu wenye kuongeza pato mifukoni mwa watu?.

Huwezi kusikia tuhuma zao za ufisadi kwa sababu vyombo vyote vya habari alivitawala yeye Mwalimu Nyerere, aliwateua wakurugenzi wa habari Maelezo na hakuna mwenye kuteuliwa na rais akaweza kwenda kinyume na amri zake.

Nyerere ndiye aliyeanzisha uchawa Tanzania hii, mikutano ya hadhara pale ikulu tulikuwa na mtindo wa kuamkiana ambapo wananchi tulisema kwa sauti zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa Chama na wengine wanaitikia zidumuuu!.
Ule ulikuwa ni mwanzo wa siasa za kichawa Tanzania, siasa za kumtukuza Mwenyekiti wa CCM aliye pia rais wa JMT.

Naweza kuelewa kuhusu ule ukweli kwamba hakuwa na bahati ya kuongoza nchi yenye wasomi wengi kama hawa kina JPM na SSH alihangaika kupandisha hadhi ya taifa lililojaa wajinga wengi.
 
Umewahi kuona Warioba hata ana shelly? bila midahalo utawajuaje wasomi wenye uwezo mkubwa ambao siyo ndugu za wakubwa? ukitaka kuteua TISS wanaleta majina ya ndugu zao, kuna nafasi ya Tanzania unaweza kuipata kwa uwezo wako ya uteuzi bila rushwa, ushirikina au kujuana? Nyerere aliuza mali gani ya kitanzania? sikatai naye alikuwa ni binadamu ndiyo maana alikiri watu walikuwa wanamzuka walikuwa wanamdanya mambo mengi sn na aliomba msamaha, kwenye utawala wa Nyerere hapakuwa na mtu anaitwa Mhe/CPA/Wakili msomi/Prof/Dr wote ilikuwa ni ndugu kudumisha umoja
 
Huwezi kusikia tuhuma zao za ufisadi kwa sababu vyombo vyote vya habari alivitawala yeye Mwalimu Nyerere, aliwateua wakurugenzi wa habari Maelezo na hakuna mwenye kuteuliwa na rais akaweza kwenda kinyume na amri zake.
Leo robo karne baada ya Nyerere kufariki, vyombo vya habari vipo vya kutosha, mnashindwa kuzitaja tuhuma za ufisadi wake? Utakuwa na tatizo la afya ya akili.
 
Kuna watu wamekuwa kero kama kelele za mbu karibu na sikio. Wanalinganisha mafanikio ya Raisi Samia na yale aliyofanya Raisi Nyerere enzi za uraisi wake. Wanashindwa kabisa kutambua Nyarere kama Raisi hawakuwa na wigo wa serikali kupata mapato alionao Samia hivi sasa. Leo hii ukilinganisha hela aliyokuwa nayo Nyerere kwa ajili ya miradi ya maendeleo huenda ni 15% tu ya fedha alizo nazo Raisi Samia.

Fikiria miradi michache tu ya Nyerere katika hali duni ya uchumi enzi hizo; TAZARA; bomba la mafuta kwenda Zambia; uanzishaji wa viwanda vya umma kama vya chai, viatu, nguo kama Urafiki, Mwatex, vinu vya pamba, vifaa vya kilimo, cement, nk; benki ya CRDB, NBC; ujenzi wa nyumba za National Housing nchi nzima; barabara ya Tanzam Dar es Salaam hadi Zambia; mpango wa elimu ya msingi kwa watoto wote UPE; Miradi ya umeme ya maji ya Mtera, Hale, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Uwemba, Pangani; ujenzi wa Chuo Kikuu cha DSM; Chuo Kikuu cha Sokoine; Mzumbe IDM; Chuo Cha Ardhi, meli na vivuko vya taifa.

Pia ujenzi wa mahoteli ya Taifa kama Kilimanjaro; vyuo vya Elimu kama Chang'ombe, Tabora nk; IFM Dar; vyuo vya Kilimo kama Uyole na Tabora; vyuo utabibu; Shirika la Elimu Kibaha; Shirika la Ndege ATC; Shirika la Reli TRC na treni za abiria za kila siku; elimu bure hadi Chuo Kikuu; matibabu bure kwa watanzania wote; bomba za maji za jumuia bure (gati); wanafunzi kula bure shuleni na kusafiri bure kwenda likizo hadi Chuo Kikuu; serikali kumudu gharama za wote wanaostahili kwenda JKT kwa kujitolea au mujibu wa sheria; Kila Mbunge kupewa gari ya serikali; kumudu gharama za vita ya Kagera; Kumudu gharama za kusaidi Ukombozi wa Afrika, nk.

Sasa bado unataka kusema Raisi Nyerere hakufanya kitu japo yote haya kwa zile fedha ndogo za kodi na mikopo alizokuwa nazo?

Na ukitaka kujua kwamba Nyerere bado angemzidi sana Samia, leo hii katika mapatao tunayopata kama nchi, mweke Nyerere kama raisi wa nchi ndio ungefikiria tungekuwa wapi, ukitambua kwamba karibu 40% ya mapato ya nchi inapotelea kwenye mifuko ya viongozi kwa ufisadi.

Na kabla hujamlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere kwa miradi ya Taifa, kumbuka utekelezaji huo wa miradi ni deni la taifa, na jiulize tumefikia wapi kwenye deni la taifa, na linganisha na Nyerere kama yale aliyofanya yaliathiri vipi deni la taifa. Kwani nani ambae akipewa mkopo wa shilingi Bilioni mia moja, atashindwa kujenga vituo kumi vya afya ili watu wamsifie anapiga mwingi?

Badala ya kuwasifia wananchi kwa uvumilivu kutokana na mzigo wa kodi wanazotozwa na deni la taifa wanalotwishwa kila mwaka, tunawezaje kuimba kupita kiasi nyimbo za kumsifia sifia mtu ambae anatumia hizo kodi na fedha zetu kuwa anatuletea miradi mingi? Kwa nini watu wanashindwa kuelewa jambo dogo kama Raisi Samia anatoa wapi hizo fedha za hiyo miradi? Zinatoka kwenye biashara ya familia yake?

Hatuna tatizo kama watu mmeamua kuwa chawa, lakini msiwe chawa wajinga wa kumlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere katika kutekeleza miradi ya taifa. Miradi aliyofanya Nyerere ndani ya miaka 23 ya utawala wake kwa fedha ndogo alokuwa nayo, si rahisi kwa Raisi Samia kuitekeleza hata kwa fedha ya kodi na mikopo aliyonayo hata tukimpa miaka 30 ya kuwa raisi wa Tanzania bara!
Ungeweka na misaada aliyopokea toka kila kona ya dunia,idadi ya watz na shule alizojenga
 
Ningependa sana yale maviwanda yote aliyofungua JKN kila corner ya Tanzanaia yarudi, sijui nani angekosa ajira kwa sasa... hata hilo bwawa la Nyerere Mbunifu ni yeye, wengine wanapitia tu humo humo kujimwambafai na kupata ujiko.
Hivi sasa tabu tupu na ni kama vile tumeshikiwa akili na wageni, tukisema tu haya mambo, watu wanakasirika ingawaje ndio ukweli wenyewe. Sasa hivi kila kitu kilio ni "hatuwezi, hatuwezi, wawekezaji wawekezaji", yaani ni aibu tupu hata tooth pick ni ngumu kutengeneza. Yule Mzee kwa kweli Mungu amuweke mahali pema pema peponi. Amina
 
Huyo Nyerere wakati wake magazeti yalikuwa matatu tu, uhuru wa habari ungekuwa sawa na leo tungeyajua madhambi yake mengi.
Yatajeni madhambi yake, mbona ya Magufuli yanatajwa baada ya kufa? Mbona ya Mkapa yalitajwa alipoacha uraisi? Na yatakuwa madhambi yepi, maana kama ni ya ufisadi kina Makongoro, Madaraka Andrew nk tunaona wakisota tu kuitafuta hela ya kula kama sisi wengine. Unategemea Samia atakapomaliza uraisi wake kina Abdul watakuwa wameachwa walivyoachwa kina Andrew Nyerere na baba yao? Au unafikiri Kikwete aliwaacha kina Ridhiwani hivyo? Au Mwinyi na wanawe? Mkapa?
 
Kuna watu wamekuwa kero kama kelele za mbu karibu na sikio. Wanalinganisha mafanikio ya Raisi Samia na yale aliyofanya Raisi Nyerere enzi za uraisi wake. Wanashindwa kabisa kutambua Nyarere kama Raisi hawakuwa na wigo wa serikali kupata mapato alionao Samia hivi sasa. Leo hii ukilinganisha hela aliyokuwa nayo Nyerere kwa ajili ya miradi ya maendeleo huenda ni 15% tu ya fedha alizo nazo Raisi Samia.

Fikiria miradi michache tu ya Nyerere katika hali duni ya uchumi enzi hizo; TAZARA; bomba la mafuta kwenda Zambia; uanzishaji wa viwanda vya umma kama vya chai, viatu, nguo kama Urafiki, Mwatex, vinu vya pamba, vifaa vya kilimo, cement, nk; benki ya CRDB, NBC; ujenzi wa nyumba za National Housing nchi nzima; barabara ya Tanzam Dar es Salaam hadi Zambia; mpango wa elimu ya msingi kwa watoto wote UPE; Miradi ya umeme ya maji ya Mtera, Hale, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Uwemba, Pangani; ujenzi wa Chuo Kikuu cha DSM; Chuo Kikuu cha Sokoine; Mzumbe IDM; Chuo Cha Ardhi, meli na vivuko vya taifa.

Pia ujenzi wa mahoteli ya Taifa kama Kilimanjaro; vyuo vya Elimu kama Chang'ombe, Tabora nk; IFM Dar; vyuo vya Kilimo kama Uyole na Tabora; vyuo utabibu; Shirika la Elimu Kibaha; Shirika la Ndege ATC; Shirika la Reli TRC na treni za abiria za kila siku; elimu bure hadi Chuo Kikuu; matibabu bure kwa watanzania wote; bomba za maji za jumuia bure (gati); wanafunzi kula bure shuleni na kusafiri bure kwenda likizo hadi Chuo Kikuu; serikali kumudu gharama za wote wanaostahili kwenda JKT kwa kujitolea au mujibu wa sheria; Kila Mbunge kupewa gari ya serikali; kumudu gharama za vita ya Kagera; Kumudu gharama za kusaidi Ukombozi wa Afrika, nk.

Sasa bado unataka kusema Raisi Nyerere hakufanya kitu japo yote haya kwa zile fedha ndogo za kodi na mikopo alizokuwa nazo?

Na ukitaka kujua kwamba Nyerere bado angemzidi sana Samia, leo hii katika mapatao tunayopata kama nchi, mweke Nyerere kama raisi wa nchi ndio ungefikiria tungekuwa wapi, ukitambua kwamba karibu 40% ya mapato ya nchi inapotelea kwenye mifuko ya viongozi kwa ufisadi.

Na kabla hujamlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere kwa miradi ya Taifa, kumbuka utekelezaji huo wa miradi ni deni la taifa, na jiulize tumefikia wapi kwenye deni la taifa, na linganisha na Nyerere kama yale aliyofanya yaliathiri vipi deni la taifa. Kwani nani ambae akipewa mkopo wa shilingi Bilioni mia moja, atashindwa kujenga vituo kumi vya afya ili watu wamsifie anapiga mwingi?

Badala ya kuwasifia wananchi kwa uvumilivu kutokana na mzigo wa kodi wanazotozwa na deni la taifa wanalotwishwa kila mwaka, tunawezaje kuimba kupita kiasi nyimbo za kumsifia sifia mtu ambae anatumia hizo kodi na fedha zetu kuwa anatuletea miradi mingi? Kwa nini watu wanashindwa kuelewa jambo dogo kama Raisi Samia anatoa wapi hizo fedha za hiyo miradi? Zinatoka kwenye biashara ya familia yake?

Hatuna tatizo kama watu mmeamua kuwa chawa, lakini msiwe chawa wajinga wa kumlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere katika kutekeleza miradi ya taifa. Miradi aliyofanya Nyerere ndani ya miaka 23 ya utawala wake kwa fedha ndogo alokuwa nayo, si rahisi kwa Raisi Samia kuitekeleza hata kwa fedha ya kodi na mikopo aliyonayo hata tukimpa miaka 30 ya kuwa raisi wa Tanzania bara!
Watukome kabisaaa.Huwezi linganisha vitu vya hovyo na Mh Hayati Julius Nyerere.
 
Angalau ilikuwa misaada, sio mikopo. Na pia ukiwa kiongozi makini mataifa makubwa yatajipendekeza tu kukupa misaada. Niliona misaada kuja Tanzania ilikauka Nyerere alipoondoka madarakani
Kwamba serikali ya nyerere haikukopa!?..kuna deni la nyerere alilipa kikwete,misaada ilikata kwa kuwa kambi ya ujamaa ilikua hoi kasoro sweden,kaka mkuu mwenyewe alikua hoi,wahuni wa kukopesha wakaingia mzigoni na masharti yaliyomshinda mjamaa,akang'atuka
 
Utakuwa unaamini unayosimuliwa na ndugu zako labda machawa au mafisadi.

Sikiliza. Nyerere alikopa. Mfano reli ya Tazara tulikopa. Bimba la Tanzam tulikopa. Barabara ya Zambia tulikopa. Vita ya Kagera tulikopa. Lakini hatukukukopa kwa sababu tulikuwa na nafasi ya kukopa.

Na kuhusu deni la Nyerere kulipwa na Kikwete, sio rahisi kuwa hivyo. Angalau hata ungesema deni la Mkapa, kwa sababu Mkapa ndio alitumia fedha nyingi sana kulipa madeni ya serikali, baadhi ya Nyerere na mengine ya Mwinyi, hadi akasema tumeweza ku-clear. Sasa kama Kikwete alilipa madeni basi una maana ya Mkapa, jambo ambalo sidhani nitakubali kirahisi hivyo. Mkapa alichukia serikali kuwa na madeni, hakupenda kabisa. Alisema tusiwe na madeni ili pale inapobidi tuwe na uwezo mkubwa wa kukopa, na watu hatukumuelewa lojiki yake.
 
Yatajeni madhambi yake, mbona ya Magufuli yanatajwa baada ya kufa? Mbona ya Mkapa yalitajwa alipoacha uraisi? Na yatakuwa madhambi yepi, maana kama ni ya ufisadi kina Makongoro, Madaraka Andrew nk tunaona wakisota tu kuitafuta hela ya kula kama sisi wengine. Unategemea Samia atakapomaliza uraisi wake kina Abdul watakuwa wameachwa walivyoachwa kina Andrew Nyerere na baba yao? Au unafikiri Kikwete aliwaacha kina Ridhiwani hivyo? Au Mwinyi na wanawe? Mkapa?
Huo ufisadi wa waliomfuatia katika kiti cha urais haifuti mengi mema wanayoyafanya wakiwa marais.

Na nyingi zinakuwa ni tuhuma za kubuniwa vichwani mwetu, hayawi ni maneno yenye kuweza kuwa na ushahidi halisi.

Mama Siti tuliambiwa ndio mmiliki wa lile jengo linalotazamana na mahakama ya kisutu pale azikiwe, zilikuwa ni habari za kubuni tu.

Chuki za watu zinatokana na umaskini wa kukosa pesa mifukoni, hivyo wanaopenda kutunga hadithi za uongo wanao uhuru wa kufanya hivyo kadri wanavyojisikia.
 
Mwehu ni wewe mkuu, sijasema kwamba Nyerere alikuwa fisadi kama waliomfuatia, nachosema alikuwa na udhaifu wa kibinadamu na tuliuona miaka ile.
Mkuu, udhaifu wa kibinadamu kuna mtu, au maraisi waliofuatia ambae hakuwa nao? Hata hivyo, tusije tukaanza kuita ufisadi ni udhaifu wa kibinadamu!
 
Back
Top Bottom