MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hamieni Burundi kama mnaona Rais Samia hafai.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Midahalo ina faida zipi ikiwa haina uwezo wa kuja na ubunifu wenye kuongeza pato mifukoni mwa watu?.Naomba tuhuma zao za ufisadi, kumteua mtu kwa uwezo wake siyo kosa, Nyerere angekuwa na upendeleo wa kwao angeacha Musoma kuna lami, chuo kikuu na mengine mengi. Ndiyo alikuwa na madhaifu yake lakini siyo kama hawa, kwanini madini hakugusa wala kuuza mali za taifa? ndiyo Rais pekee aliweza kupunguza mshahara wake na alikuwa anaenda kwenye midahalo UDSM sasahivi hata DC hawezi kuandaa mdahalo, nchi gani inaweza kuendelesha bila mijadala/midahalo?
Umewahi kuona Warioba hata ana shelly? bila midahalo utawajuaje wasomi wenye uwezo mkubwa ambao siyo ndugu za wakubwa? ukitaka kuteua TISS wanaleta majina ya ndugu zao, kuna nafasi ya Tanzania unaweza kuipata kwa uwezo wako ya uteuzi bila rushwa, ushirikina au kujuana? Nyerere aliuza mali gani ya kitanzania? sikatai naye alikuwa ni binadamu ndiyo maana alikiri watu walikuwa wanamzuka walikuwa wanamdanya mambo mengi sn na aliomba msamaha, kwenye utawala wa Nyerere hapakuwa na mtu anaitwa Mhe/CPA/Wakili msomi/Prof/Dr wote ilikuwa ni ndugu kudumisha umojaMidahalo ina faida zipi ikiwa haina uwezo wa kuja na ubunifu wenye kuongeza pato mifukoni mwa watu?.
Huwezi kusikia tuhuma zao za ufisadi kwa sababu vyombo vyote vya habari alivitawala yeye Mwalimu Nyerere, aliwateua wakurugenzi wa habari Maelezo na hakuna mwenye kuteuliwa na rais akaweza kwenda kinyume na amri zake.
Nyerere ndiye aliyeanzisha uchawa Tanzania hii, mikutano ya hadhara pale ikulu tulikuwa na mtindo wa kuamkiana ambapo wananchi tulisema kwa sauti zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa Chama na wengine wanaitikia zidumuuu!.
Ule ulikuwa ni mwanzo wa siasa za kichawa Tanzania, siasa za kumtukuza Mwenyekiti wa CCM aliye pia rais wa JMT.
Naweza kuelewa kuhusu ule ukweli kwamba hakuwa na bahati ya kuongoza nchi yenye wasomi wengi kama hawa kina JPM na SSH alihangaika kupandisha hadhi ya taifa lililojaa wajinga wengi.
Leo robo karne baada ya Nyerere kufariki, vyombo vya habari vipo vya kutosha, mnashindwa kuzitaja tuhuma za ufisadi wake? Utakuwa na tatizo la afya ya akili.Huwezi kusikia tuhuma zao za ufisadi kwa sababu vyombo vyote vya habari alivitawala yeye Mwalimu Nyerere, aliwateua wakurugenzi wa habari Maelezo na hakuna mwenye kuteuliwa na rais akaweza kwenda kinyume na amri zake.
Ungeweka na misaada aliyopokea toka kila kona ya dunia,idadi ya watz na shule alizojengaKuna watu wamekuwa kero kama kelele za mbu karibu na sikio. Wanalinganisha mafanikio ya Raisi Samia na yale aliyofanya Raisi Nyerere enzi za uraisi wake. Wanashindwa kabisa kutambua Nyarere kama Raisi hawakuwa na wigo wa serikali kupata mapato alionao Samia hivi sasa. Leo hii ukilinganisha hela aliyokuwa nayo Nyerere kwa ajili ya miradi ya maendeleo huenda ni 15% tu ya fedha alizo nazo Raisi Samia.
Fikiria miradi michache tu ya Nyerere katika hali duni ya uchumi enzi hizo; TAZARA; bomba la mafuta kwenda Zambia; uanzishaji wa viwanda vya umma kama vya chai, viatu, nguo kama Urafiki, Mwatex, vinu vya pamba, vifaa vya kilimo, cement, nk; benki ya CRDB, NBC; ujenzi wa nyumba za National Housing nchi nzima; barabara ya Tanzam Dar es Salaam hadi Zambia; mpango wa elimu ya msingi kwa watoto wote UPE; Miradi ya umeme ya maji ya Mtera, Hale, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Uwemba, Pangani; ujenzi wa Chuo Kikuu cha DSM; Chuo Kikuu cha Sokoine; Mzumbe IDM; Chuo Cha Ardhi, meli na vivuko vya taifa.
Pia ujenzi wa mahoteli ya Taifa kama Kilimanjaro; vyuo vya Elimu kama Chang'ombe, Tabora nk; IFM Dar; vyuo vya Kilimo kama Uyole na Tabora; vyuo utabibu; Shirika la Elimu Kibaha; Shirika la Ndege ATC; Shirika la Reli TRC na treni za abiria za kila siku; elimu bure hadi Chuo Kikuu; matibabu bure kwa watanzania wote; bomba za maji za jumuia bure (gati); wanafunzi kula bure shuleni na kusafiri bure kwenda likizo hadi Chuo Kikuu; serikali kumudu gharama za wote wanaostahili kwenda JKT kwa kujitolea au mujibu wa sheria; Kila Mbunge kupewa gari ya serikali; kumudu gharama za vita ya Kagera; Kumudu gharama za kusaidi Ukombozi wa Afrika, nk.
Sasa bado unataka kusema Raisi Nyerere hakufanya kitu japo yote haya kwa zile fedha ndogo za kodi na mikopo alizokuwa nazo?
Na ukitaka kujua kwamba Nyerere bado angemzidi sana Samia, leo hii katika mapatao tunayopata kama nchi, mweke Nyerere kama raisi wa nchi ndio ungefikiria tungekuwa wapi, ukitambua kwamba karibu 40% ya mapato ya nchi inapotelea kwenye mifuko ya viongozi kwa ufisadi.
Na kabla hujamlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere kwa miradi ya Taifa, kumbuka utekelezaji huo wa miradi ni deni la taifa, na jiulize tumefikia wapi kwenye deni la taifa, na linganisha na Nyerere kama yale aliyofanya yaliathiri vipi deni la taifa. Kwani nani ambae akipewa mkopo wa shilingi Bilioni mia moja, atashindwa kujenga vituo kumi vya afya ili watu wamsifie anapiga mwingi?
Badala ya kuwasifia wananchi kwa uvumilivu kutokana na mzigo wa kodi wanazotozwa na deni la taifa wanalotwishwa kila mwaka, tunawezaje kuimba kupita kiasi nyimbo za kumsifia sifia mtu ambae anatumia hizo kodi na fedha zetu kuwa anatuletea miradi mingi? Kwa nini watu wanashindwa kuelewa jambo dogo kama Raisi Samia anatoa wapi hizo fedha za hiyo miradi? Zinatoka kwenye biashara ya familia yake?
Hatuna tatizo kama watu mmeamua kuwa chawa, lakini msiwe chawa wajinga wa kumlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere katika kutekeleza miradi ya taifa. Miradi aliyofanya Nyerere ndani ya miaka 23 ya utawala wake kwa fedha ndogo alokuwa nayo, si rahisi kwa Raisi Samia kuitekeleza hata kwa fedha ya kodi na mikopo aliyonayo hata tukimpa miaka 30 ya kuwa raisi wa Tanzania bara!
Angalau ilikuwa misaada, sio mikopo. Na pia ukiwa kiongozi makini mataifa makubwa yatajipendekeza tu kukupa misaada. Niliona misaada kuja Tanzania ilikauka Nyerere alipoondoka madarakaniUngeweka na misaada aliyopokea toka kila kona ya dunia,idadi ya watz na shule alizojenga
Yatajeni madhambi yake, mbona ya Magufuli yanatajwa baada ya kufa? Mbona ya Mkapa yalitajwa alipoacha uraisi? Na yatakuwa madhambi yepi, maana kama ni ya ufisadi kina Makongoro, Madaraka Andrew nk tunaona wakisota tu kuitafuta hela ya kula kama sisi wengine. Unategemea Samia atakapomaliza uraisi wake kina Abdul watakuwa wameachwa walivyoachwa kina Andrew Nyerere na baba yao? Au unafikiri Kikwete aliwaacha kina Ridhiwani hivyo? Au Mwinyi na wanawe? Mkapa?Huyo Nyerere wakati wake magazeti yalikuwa matatu tu, uhuru wa habari ungekuwa sawa na leo tungeyajua madhambi yake mengi.
Watukome kabisaaa.Huwezi linganisha vitu vya hovyo na Mh Hayati Julius Nyerere.Kuna watu wamekuwa kero kama kelele za mbu karibu na sikio. Wanalinganisha mafanikio ya Raisi Samia na yale aliyofanya Raisi Nyerere enzi za uraisi wake. Wanashindwa kabisa kutambua Nyarere kama Raisi hawakuwa na wigo wa serikali kupata mapato alionao Samia hivi sasa. Leo hii ukilinganisha hela aliyokuwa nayo Nyerere kwa ajili ya miradi ya maendeleo huenda ni 15% tu ya fedha alizo nazo Raisi Samia.
Fikiria miradi michache tu ya Nyerere katika hali duni ya uchumi enzi hizo; TAZARA; bomba la mafuta kwenda Zambia; uanzishaji wa viwanda vya umma kama vya chai, viatu, nguo kama Urafiki, Mwatex, vinu vya pamba, vifaa vya kilimo, cement, nk; benki ya CRDB, NBC; ujenzi wa nyumba za National Housing nchi nzima; barabara ya Tanzam Dar es Salaam hadi Zambia; mpango wa elimu ya msingi kwa watoto wote UPE; Miradi ya umeme ya maji ya Mtera, Hale, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Uwemba, Pangani; ujenzi wa Chuo Kikuu cha DSM; Chuo Kikuu cha Sokoine; Mzumbe IDM; Chuo Cha Ardhi, meli na vivuko vya taifa.
Pia ujenzi wa mahoteli ya Taifa kama Kilimanjaro; vyuo vya Elimu kama Chang'ombe, Tabora nk; IFM Dar; vyuo vya Kilimo kama Uyole na Tabora; vyuo utabibu; Shirika la Elimu Kibaha; Shirika la Ndege ATC; Shirika la Reli TRC na treni za abiria za kila siku; elimu bure hadi Chuo Kikuu; matibabu bure kwa watanzania wote; bomba za maji za jumuia bure (gati); wanafunzi kula bure shuleni na kusafiri bure kwenda likizo hadi Chuo Kikuu; serikali kumudu gharama za wote wanaostahili kwenda JKT kwa kujitolea au mujibu wa sheria; Kila Mbunge kupewa gari ya serikali; kumudu gharama za vita ya Kagera; Kumudu gharama za kusaidi Ukombozi wa Afrika, nk.
Sasa bado unataka kusema Raisi Nyerere hakufanya kitu japo yote haya kwa zile fedha ndogo za kodi na mikopo alizokuwa nazo?
Na ukitaka kujua kwamba Nyerere bado angemzidi sana Samia, leo hii katika mapatao tunayopata kama nchi, mweke Nyerere kama raisi wa nchi ndio ungefikiria tungekuwa wapi, ukitambua kwamba karibu 40% ya mapato ya nchi inapotelea kwenye mifuko ya viongozi kwa ufisadi.
Na kabla hujamlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere kwa miradi ya Taifa, kumbuka utekelezaji huo wa miradi ni deni la taifa, na jiulize tumefikia wapi kwenye deni la taifa, na linganisha na Nyerere kama yale aliyofanya yaliathiri vipi deni la taifa. Kwani nani ambae akipewa mkopo wa shilingi Bilioni mia moja, atashindwa kujenga vituo kumi vya afya ili watu wamsifie anapiga mwingi?
Badala ya kuwasifia wananchi kwa uvumilivu kutokana na mzigo wa kodi wanazotozwa na deni la taifa wanalotwishwa kila mwaka, tunawezaje kuimba kupita kiasi nyimbo za kumsifia sifia mtu ambae anatumia hizo kodi na fedha zetu kuwa anatuletea miradi mingi? Kwa nini watu wanashindwa kuelewa jambo dogo kama Raisi Samia anatoa wapi hizo fedha za hiyo miradi? Zinatoka kwenye biashara ya familia yake?
Hatuna tatizo kama watu mmeamua kuwa chawa, lakini msiwe chawa wajinga wa kumlinganisha Raisi Samia na Raisi Nyerere katika kutekeleza miradi ya taifa. Miradi aliyofanya Nyerere ndani ya miaka 23 ya utawala wake kwa fedha ndogo alokuwa nayo, si rahisi kwa Raisi Samia kuitekeleza hata kwa fedha ya kodi na mikopo aliyonayo hata tukimpa miaka 30 ya kuwa raisi wa Tanzania bara!
Kwamba serikali ya nyerere haikukopa!?..kuna deni la nyerere alilipa kikwete,misaada ilikata kwa kuwa kambi ya ujamaa ilikua hoi kasoro sweden,kaka mkuu mwenyewe alikua hoi,wahuni wa kukopesha wakaingia mzigoni na masharti yaliyomshinda mjamaa,akang'atukaAngalau ilikuwa misaada, sio mikopo. Na pia ukiwa kiongozi makini mataifa makubwa yatajipendekeza tu kukupa misaada. Niliona misaada kuja Tanzania ilikauka Nyerere alipoondoka madarakani
Utakuwa unaamini unayosimuliwa na ndugu zako labda machawa au mafisadi.Kwamba serikali ya nyerere haikukopa!?..kuna deni la nyerere alilipa kikwete,misaada ilikata kwa kuwa kambi ya ujamaa ilikua hoi kasoro sweden,kaka mkuu mwenyewe alikua hoi,wahuni wa kukopesha wakaingia mzigoni na masharti yaliyomshinda mjamaa,akang'atuka
Huyo Steven Joel Ntamusano ni mwehu!Leo robo karne baada ya Nyerere kufariki, vyombo vya habari vipo vya kutosha, mnashindwa kuzitaja tuhuma za ufisadi wake? Utakuwa na tatizo la afya ya akili.
Huo ufisadi wa waliomfuatia katika kiti cha urais haifuti mengi mema wanayoyafanya wakiwa marais.Yatajeni madhambi yake, mbona ya Magufuli yanatajwa baada ya kufa? Mbona ya Mkapa yalitajwa alipoacha uraisi? Na yatakuwa madhambi yepi, maana kama ni ya ufisadi kina Makongoro, Madaraka Andrew nk tunaona wakisota tu kuitafuta hela ya kula kama sisi wengine. Unategemea Samia atakapomaliza uraisi wake kina Abdul watakuwa wameachwa walivyoachwa kina Andrew Nyerere na baba yao? Au unafikiri Kikwete aliwaacha kina Ridhiwani hivyo? Au Mwinyi na wanawe? Mkapa?
Kwann mkuuLeo Kagame akituvamia kama Amin alivyofanya 1978 sina hakika kama tunaweza kuhimili.
Mwehu ni wewe mkuu, sijasema kwamba Nyerere alikuwa fisadi kama waliomfuatia, nachosema alikuwa na udhaifu wa kibinadamu na tuliuona miaka ile.Huyo Steven Joel Ntamusano ni mwehu!
Mkuu, udhaifu wa kibinadamu kuna mtu, au maraisi waliofuatia ambae hakuwa nao? Hata hivyo, tusije tukaanza kuita ufisadi ni udhaifu wa kibinadamu!Mwehu ni wewe mkuu, sijasema kwamba Nyerere alikuwa fisadi kama waliomfuatia, nachosema alikuwa na udhaifu wa kibinadamu na tuliuona miaka ile.