Mnaomshambulia RC wa Arusha, mnafurahia kiongozi wetu kutukanwa?

Tusijisahaulishe,

Ilivuja sauti za viongozi wakimnanga Magu, hapo hapo mwingine akachora vikatuni,

Magu aliwaondoa watu hao,

Sa100 kawarudisha akidhani wamejifunza kumbe wapi!!

Kilichobaki awafukuze wote.

Hakuna namna hapo!!
 
Tusijisahaulishe,

Ilivuja sauti za viongozi wakimnanga Magu, hapo hapo mwingine akachora vikatuni,

Magu aliwaondoa watu hao,

Sa100 kawarudisha akidhani wamejifunza kumbe wapi!!

Kilichobaki awafukuze wote.

Hakuna namna hapo!!
Hujaelewa somo ninaloliongelea.

Unaangalia na kuondoa dalili ya ugonjwa bila kuangalia sababu ya ugonjwa.

Tuseme hawa mawaziri wapo kweli na ni watu wa ovyo. For the sake of argument. Tuondoe complexities zote za kisiasa. Tufanye Makonda kasema kweli, Samia kakosewa heshima na mawaziri wake.

Rais kashindwa vipi kuwa na mfumo wa vetting wa kuwagundua hawa ni watu wa ovyo na kuwachuja wasipate uwaziri?

Unasema awafukuze. Sawa. Akiwafukuza bila ya kuwa na mfumo mzuri wa vetting, kuchuja watu anaowateua, unajuaje hao wapya atakaowateua hawatakuwa na matatizo haya haya?
 
Huyo Mange anahitaji speed control haraka sana. Sijui kwa nini hakuna mbinu ya kumalizana na hii tabia yake, she's too much.

Rais akosolewe kwa maneno ya kawaida, sio kutweza utu wake, yeye ni mama, mke na mkuu wa nchi. Akosolewe kwa namna inayofaa, matusi ya Mange ni uchafu uliopitiliza.
 
Mfumo mzuri ni KATIBA mpya iliyoasisiwa na Judge Warioba urudi mezani, yafanyike marekebisho na yaongezwe mapya machache,

Hatimaye tupate Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Lakini kabla ya kufika huko, awatimue wahujumu wote.
 
Umejiuliza kwanini Nape na Makamba hawakumshambulia au kumkemea mtukanaji Kwa wakati ilhali wao ndio wenye dhamana katika jambo Hilo?
 
Mfumo mzuri ni KATIBA mpya iliyoasisiwa na Judge Warioba urudi mezani, yafanyike marekebisho na yaongezwe mapya machache,

Hatimaye tupate Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Lakini kabla ya kufika huko, awatimue wahujumu wote.
Hata hiyo katiba mpya ni jibu rahisi kwa matatizo magumu.

Katiba ya sasa haisemi mawaziri wamtukane rais, in fact imemfanya rais awe kama Mungu mtu.

In fact, tunachotaka kubadilisha kwenye katiba mpya ni kupunguza madaraka ya rais. Innother words, kufanya rais aweze kutukanwa kirahisi zaidi.

Kwa hivyo, hapa hakuna tatizo la kikatiba.

Tuache kuisingizia katiba hata kwenye matatizo yetu mengine ya kiutamaduni tu.

Ukiwa na tatizo la utamaduni, kwa mfano rais kuteua watu bila proper vetting, hilo si tatizo litakalotatuliwa na katiba mpya.

Tuache tabia ya kusingizia katiba mpya kila kitu. Katiba mpya inakuwa kama kichaka cha kutupia uchafu wote.

Viongozi wakizozana kwa kukoseana heshima, rais kuteua bila vetting, hapo katiba mpya inaingiaje?
 
KATIBA inahusika vilivyo.

Mamlaka makubwa ya Rais yanatoa mwanya Sanduku la kura kuchezewa na viongozi wasio na Maadili ambao wao wako tayari kufanya lolote kufanikisha agenda zao.

Mawaziri wangekuwa hawatokani na wabunge ,Bali mchakato wa Taasisi huru na Imara isiyoingiliwa na rais, tusingekuwa na mawaziri ambao chama kimewahi kuwatia MIZIGO!!

Matatizo ya nchi yetu, Yana mahusiano ya Moja Kwa moja na Katiba ya nchi.
 
Binafis naungana na wew kwa asilimia Mia.. Wapewe mshahara usiozid 3M per Month plus na Viposho vya kawaida katika vikao. Bado naamini tutapata wabunge bora zaidi na wanaoweza kuwatetea vyema wananchi. Mawaziri pia ikiwezekana wasitokane na wabunge wawe huru na waliobobea kwenye sector watakazo ziongoza
 
Swali endekevu kuanzia sasa;

"WATANZANIA MNAMTAKA RAIS WA NAMNA NA AINA GANI?"
Watanzania tunataka Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Rais aje baada ya Kupata mambo hayo hapo juu🙄
 
Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya ni sasa kabla ya Uchaguzi wowote.

Rasimu ya Warioba irudi mezani, tufanye marekebisho kidogo, hatimaye tupate Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ndipo tuuingie uchaguzi.
 
Umejiuliza kwanini Nape na Makamba hawakumshambulia au kumkemea mtukanaji Kwa wakati ilhali wao ndio wenye dhamana katika jambo Hilo?
Mange is feared by many, sijajua sababu ila yule mropokaji anaogopeka, hasa kama mtu ana makandokando mengi.
 
Mange is feared by many, sijajua sababu ila yule mropokaji anaogopeka, hasa kama mtu ana makandokando mengi.
Si kwamba wanaogopa kutokana na hujuma waliyomfanyia Magu?
 
Mamlaka makubwa ya rais yanatakiwa kumpa control kubwa zaidi rais katika kufanya vetting kuchuja watu wa ovyo.

Mimi si mtetezi wa rais kuwa na mamlaka makubwa, lakini nitakuonesha jinsi mamlaka makubwa ya rais yalivyo advantage na si disadvantage kwa rais hapa.

Rais Mkapa alikuwa anataka kuteua mtu wa kuongoza PSRC (Parastatal Sector Reform Commission). Nafikiri Mzee George Mbowe alikuwa anaondoka, mwaka 1998. Kwa kuelewa umuhimu wa kiongozi wa taasisi hii, rais Mkapa aliwafanyia phone tapping kwa zaidi ya mwaka mzima watu fulani waliokuwa wanaonekana kuweza kufaa kazi hiyo.

Watu walikuwa wanasikilizwa simu zao na serikali ya Mkapa kwa zaidi ya mwaka mzima kama sehemu ya vetting.

Rais alitumia turufu yake ya "usalama wa taifa". Madaraka makubwa ya rais yalimruhusu kufanya hivyo.

Mwishowe, rais Mkapa akajiridhisha kuwa John Rubambe atafaa kushika nafasi hii. Akamteua.

Sasa hapo nguvu kubwa za rais si disadvantage katika kufanya vetting, ni advantage.

In this case, ukikubali anayosema Makonda, kuna tatizo la vetting. Au labda kuna tatizo la rais kuwa na uwezo mdogo. Au labda kuna tatizo la kiutamaduni.

Haya si matatizo ya kutatuliwa na katiba mpya.

Kama rais hafanyi vetting, hana uwezo, au ana utamaduni mbaya, haya matatizo hayatatuliwi na katiba mpya.

Mamlaka makubwa ya rais, kwa rais, hapo ni advantage, si disadvantage.

Kuna tatizo tofauti ambalo hutaki kuliangalia kwa sababu ushajikubalisha na kujikaririsha boilerplate answer ya "katiba mpya".

Ukikubali maneno ya Makonda, kuna matatizo ya utamaduni, vetting, politics, sasa hayo matatizo utayatatuaje kwa katiba mpya?

Samia alisema katiba ni kijitabu tu. Watanzania wengi hawakumuelewa wakamshambulia.

Lakini, kama kuna mambo machache ninayokubaliana na Samia ni kauki ile.

Mimi naheshimu sana utawala wa sheria, napenda sana mabadiliko ya kikatiba.

Lakini, katiba ni kijitabu tu. Maana yake ni kwamba, zike kanuni za kikatiba zinatakiwa kuishi kwenye vichwa vya watu, siyo watu wanataka demokrasia kwenye katiba halafu wao mafashisti madikteta.

Hakuna kifungu cha katiba kinachokubali mawaziri kumtykana rais. Hakuna tatizo la kikatiba hapa.

Tuache kutupia kila tatizo kwenye kichaka cha "katiba mpya".

Sasa kama una mawaziri wa ovyo wanaomtukana rais, kama una rais wa ovyo asiyejua kuchuja watu anaowateua kuwa mawaziri, hapo katiba mpya itakusaidiaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…