Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mamlaka makubwa kwa rais asiye mfuatiliaji ni irrelevant. Si advantage wala disadvantage. Kwa sababu rais hatayatumia.Ndio maana nasema, huo uwezo wa Rais kufanya vetting unategemeana na Rais mwenyewe,
Ikiwa Rais anapenda safari, hatulii nchini, hapati muda mrefu kukaa Ofisini, atawezaje kupata ufanisi unaotakiwa?
Huoni kuwa mamlaka makubwa Kwa Rais asiye mfuatiliaji ni DISADVANTAGE?
Bado huoni umuhimu wa kupunguza mamlaka ya Rais, Ili Taasisi Imara ichukue KAZI hiyo?
Bado nabaki na msimamo kuwa, matatizo yetu, chanzo ni Katiba!!
Ni sawa na access ya gari lenye engine kubwa kwa mtu asiyejua kuendesha wala akili ya kulitumia.
Utasemaje hiyo access kwa gari hilo ni advantage au disadvantage kama mtu hawezi hata kuitumia?
Ukishakubali habari za kumtegemea rais mwenyewe, maamuzi kuwa arbitrary kwa kutegemea nature ya raus, habari za kutatua matatizo kwa kubadili katiba zinakuwa kisingizio tu.
Magufuli kavunja vifungu vingi sana vya katiba, katiba hii hii tuliyo nayo. Kapiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa ambayo inaruhusiwa kikatiba, ambayo nibhaki ya kikatiba, ni haki ya kibinadamu, Tanzania tumesaini mpaka mikataba ya kimataifa kukubali haki hii.
Na hakuna mtu aliyemuwajibisha. Kwa sababu nchi nzima haina utamaduni wa kuheshimu katiba. Tatizo hapo nibutamaduni, si katiba. Huelewi wapi?
Sasa unaposhikilia kila tatizo litatuliwe na katiba mpya, hata matatizo ya kiutamaduni, tukipata hiyo katiba mpya halafu rais akikataa kuifuata kama alivyofanya Magufuli, na wananchi wakapotezea mambo ya katiba kama walivyopotezea kwa Magufuki, hiyo katiba mpya itatusaidiaje?
Don't get me wrong, hata mimi katiba mpya naitaka.
Lakini je, mnaelewa limitations za katiba? Mnaelewa kuwa matatizo mengine ni ya kiutamaduni na hayatatuliki kwa katiba mpya tu? Mnaelewa kuwa katiba iwe mpya au hii ya sasa inahitaji watu wa kuisimamia ili iwe na maana, vinginevyo inabaki kuwa "kijitabu tu" kama alivyosema rais Samia?