Mnaomshambulia RC wa Arusha, mnafurahia kiongozi wetu kutukanwa?

Mnaomshambulia RC wa Arusha, mnafurahia kiongozi wetu kutukanwa?

Kinachosanabisha matusi ni hali halisi ya yanayoendelea huku mtaani. Kama mambo yangekuwa yapo sawa haya matusi yasingethiri halafu kumbuka haya matusi yapo toka enzi za Mitume. Ni kawaida sana na hauwezi ukazuia mihemko ya watu.wacha tuone hao watu wakitajwa kama matusi yatakoma
Mihemko ya wananchi mitandaoni hiyo Si serious sana,

Mbaya ni kutukanwa Kwa Siri na viongozi uliowateua mwenyewe,

Huoni tatizo hapo?
 
Wanajitoa ufahamu,

Kibri Cha kutofuata Katiba linatokana na Kinga na mamlaka ya juu na kutoshtakiwa.

Rais ni sehemu ya bunge, bunge linaanzaje mchakato wa kupeleka HOJA ya kutokuwa na Imani naye?
Ni vigumu kabisa, hivyo Kuna kila sababu ya katiba mpya
 
Katiba ni kijitabu tu.

Kinachoipa katiba nguvu ni watu watakaoisimamia.

Kama una katiba nzuri sana lakini watu hawajui na hawataki kuisimamia, wanaipotezea, katiba hiyo itakuwa haina impact, itabaki kuwa kijitabu tu ambacho hakina impact.

Watu ndio wanaipa katiba uhai.

Usichoelewa ni kipi hapo?

USA watu wanachoma moto bendera yao, wanachoma moto katiba, hizo ni symbols tu, kitu muhimu zaidi ya symbols ni watu wenyewe na impementation ya ideals.

Wanaelewa katiba ni kijitabu tu. Bendera ni kitambaa tu.

Wanachoma moto bendera na katiba kwenye protests kama sehemu ya free speech.

Sasa wewe umeweka mbele symbols kuliko the actual implementation of ideals.
Mkuu nakuunga mkono. Usemalo ni kweli Mkuu, hata DRC Congo inakaba moja nzuri sana ila usimamizi wake sasa ndio mtihani, hapo ni suala wananchi.

Kenya ilikuwa na katiba mbovu kuliko hata ya kwetu lakini kwa sababu ya uelewa na msimamo wao walitoboa.
 
Mkuu nakuunga mkono. Usemalo ni kweli Mkuu, hata DRC Congo inakaba moja nzuri sana ila usimamizi wake sasa ndio mtihani, hapo ni suala wananchi.

Kenya ilikuwa na katiba mbovu kuliko hata ya kwetu lakini kwa sababu ya uelewa na msimamo wao walitoboa.
Uongo,

Kenya wametoboa baada ya Katiba mpya, Si kabla ya Katiba mpya.
 
Unaanzaje kumchukulia hatua au kumuwajibisha aliyekufinyanga akakuweka ulipo.
Kama una utamaduni wa kuheshimu kanuni hata mama yako aliyekuzaa akivunja kanuni unamueleza na kumrejesha mstarini kikanuni tu.Bila hata kuvunja heshima yake kama mama mzazi.

Sdmbuse huyo "Mama" wa kuchongwa?

Tatizo hatuna utamaduni wa kufikiri kidhahania na kimantiki, hivyo hatuheshimu katiba.
 
Hivi ni kina nani walikuwa wanatoa siri za ikulu na kumpa huyo binti wa Marekani na upinzani wakati wa JPM, kuna taarifa ni Samia na hao vijana wake ndio walikuwa wahusika wakuu. Kwahiyo nafikiri ni sahihi kusema wanajuana.

Samia alipoingia tu kwenye kiti waliacha kuvujisha taarifa za ikulu.
🤔🙄👌
 
Uongo,

Kenya wametoboa baada ya Katiba mpya, Si kabla ya Katiba mpya.
Mkuu naona unabisha for the sake of it ila hujaamua kuelewa hoja ya ndugu Kiranga.

Fuatilia mchakato wa utafutaji wa katiba mpya ya Kenya na ushiriki wa wananchi wake ndio utaelewa zaidi anacho maanisha ndugu Kiranga.
 
Unaanzaje kumchukulia hatua au kumuwajibisha aliyekufinyanga akakuweka ulipo.
Katiba si inakuruhusu kufanya hivyo?

Umeona sasa, watu walijua fika kwamba katiba inaweza kutumika kupinga lile agizo la Magufuli kufungia mikutano ya kisiasa, Lakini wakakaa kimya kulinda ulaji wao.

Je watu hawahawa watakuwa na nia kweli ya kutaka katiba mpya itakayo dhibiti ulaji wao?
 
Uongo,

Kenya wametoboa baada ya Katiba mpya, Si kabla ya Katiba mpya.
Mkuu,

Hata ikiwa Kenya kweli wametoboa baada ya katiba mpya (this is debatable, but lets grant that for the sake of argument), ule utamaduni wao wa kutaka mabadiliko, kutaka katiba mpya, kutaka kuishi kisheria zaidi ndiyo umewapa hiyo katiba mpya.

Kwa maneno mengine, utamaduni wa Wakenya ndio umewapa katiba mpya, na kupelekea huko kutoboa unakokusema.

Katiba mpya haikuwapa Wakenya utamaduni wao.

Sisi mara nyingine tunataka kufanya vitu backwards. Tunafikiri tukiwa na katiba mpya katiba mpya itamaliza matatizo yetu.

Ni kama vile tuna uvivu fulani wa kufikiri na kutatua matatizo, tunapenda kutoa jibu rahisi kwa kila tatizo. Jibu la tatizo lolote ni "katiba mpya" tu.

Katiba mpya itamalizaje matatizo ikiwa kuna tatizo la kiutamaduni la kutoheshimu katiba iliyopo na hata hiyo mpya watu hawataiheshimu na hawataitumia?

Don't get me wrong. Katiba mpya ni muhimu, hata mimi naitaka.

Lakini, utamaduni wa watu kusimamia haki zao za kikatiba ni muhimu zaidi. Bila huu utamaduni katiba mpya haitakuwa na maana.

Kwanza hamuwezi hata kupata katiba mpya nzuri. Mkipata mpya mtagundua mapungufu na kudai mpya zaidi. Kwa sababu hata hiyo mpya hamtaipata kwa umakini, kwa sababu ya kukosa utamaduni wa kuishi kikatiba.

Lets say maximum efficiency ya katiba ni 100%. Tuiite katiba inayofikia hii maximum efficiency katiba A.

Let's say katiba yetu ya sasa, katiba B, haifiki hiyo 100% maximum, maximum efficiency ya katiba yetu sasa, katiba B, ni 50% ya katiba A.

Tukiweza kuitumia katiba yetu B kwa 100% efficiency tutapata 50% efficiency ya katiba A.

Katiba B si nzuri sana, ina efficiency ya 50% tu, lakini tumeweza kuitumia hiyo hiyo mbaya fully, tukapata efficiency 50%.

Halafu, watu wanaotumia katiba A, yenye potential efficiency ya 100%, wanaitumia kwa level ya efficiency 20% tu.

Hapo utaona hao wenye katiba bora maradufu zaidi yetu wanaitumia vibaya na kupata efficiency ya 20%, wakati sisi tuna katiba mbaya zaidi yao lakini tunaitumia vizuri zaidi na kupata efficiency ya 50%.

Kwa hivyo, mabadiliko ya katiba ni muhimu, tunayahitaji, lakini kitu muhimu zaidi ni uwezo wa watu kuisimamia katiba, utamaduni wa kuheshimu na kuisimamia katiba ni kitu muhimu zaidi ya kuwa na katiba mpya tu.
 
Asingekuwa na Kinga ya kutoshtakiwa,

Asingediriki kuzuia mikutano ya hadhara.

Mamlaka ya Rais makubwa, ndiyo chanzo Cha matatizo yetu nchini.
Kwa nini wabunge na wananchi hamkukemea na kupinga agizo lake kwa kutumia katiba iliyopo?

Watanzania ni keyboard warriors lakini likija kwenye kuchukua actions kila mtu anabaki kutetea maslahi na ulaji wake kwa bosi wake.

Hata hiyo katiba mpya ikija itavunjwa na hakuna hatua zozote zitakazo chukuliwa watu watafocus kwenye maslahi yao na ulaji wao.

Asili ya mtanzania ni upigaji, Black people cannot rule themselves.
 
Mkuu nakuunga mkono. Usemalo ni kweli Mkuu, hata DRC Congo inakaba moja nzuri sana ila usimamizi wake sasa ndio mtihani, hapo ni suala wananchi.

Kenya ilikuwa na katiba mbovu kuliko hata ya kwetu lakini kwa sababu ya uelewa na msimamo wao walitoboa.
Mkuu,

Tanzania kwenye mipango sehemu nyingi tuko vizuri sana kitambo.

Ukiisoma hii nchi kwenye makaratasi, hata kwa katiba yetu ya sasa hii, nchi ina haki za binadamu, ina sheria nyingi tu nzuri, ina mipango kibao mizuri sana.

Tatizo, sisi ni watu wa kuandika vitu na kuviweka maktaba vipigwe na vumbi, utekelezaji ni mdogo sana.

Mipango ni muhimu. Katiba ni muhimu. Katiba mpya hata mimi naelewa sana umuhimu wake.

Lakini, inatubidi tuelewe kuwa katiba mpya pele yake haitabadikisha nchi.

Magufuli alipiga marufuju mikutano ya hadhara ya kisiasa kinyume na katiba, na hakuna aliyemfanya kitu.

Kwa sababu hatuna utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria, hatuheshimu katiba.

Sasa kama rais kavunja katiba ya sasa, tukioata mpya tutamzuia vioi asiivunje na hiyo?

Hapa naona tunaitegea katiba. Kuna kazi ya kufanya. Kazi hii inatakiwa kufanywa na wananchi. Kazi ya kufungua kesi mahakamani, kuandamana, kupinga uvunjwaji wa katiba.

Wananchi wanazembea kufanya kazi ya kusimamia haki zao za kikatiba.

Badala yabkufanyabkazi hiyo, wanasema tu "solutiin ni katiba mpya".

Yaninkama vike tukiwa na katiba mpya itakayoandika vifungu vya kuwabana zaidi viongozi, viongozi wataiogopa katiba na kujirekebisha.

Viongozi hawaiogopi katiba ya sasa, wataiogopa vipi mpya ikiwa hatutabadilisha utamaduni na kufanya kazi ya kusimamia katiba?
 
Back
Top Bottom