Mkuu,
Hata ikiwa Kenya kweli wametoboa baada ya katiba mpya (this is debatable, but lets grant that for the sake of argument), ule utamaduni wao wa kutaka mabadiliko, kutaka katiba mpya, kutaka kuishi kisheria zaidi ndiyo umewapa hiyo katiba mpya.
Kwa maneno mengine, utamaduni wa Wakenya ndio umewapa katiba mpya, na kupelekea huko kutoboa unakokusema.
Katiba mpya haikuwapa Wakenya utamaduni wao.
Sisi mara nyingine tunataka kufanya vitu backwards. Tunafikiri tukiwa na katiba mpya katiba mpya itamaliza matatizo yetu.
Ni kama vile tuna uvivu fulani wa kufikiri na kutatua matatizo, tunapenda kutoa jibu rahisi kwa kila tatizo. Jibu la tatizo lolote ni "katiba mpya" tu.
Katiba mpya itamalizaje matatizo ikiwa kuna tatizo la kiutamaduni la kutoheshimu katiba iliyopo na hata hiyo mpya watu hawataiheshimu na hawataitumia?
Don't get me wrong. Katiba mpya ni muhimu, hata mimi naitaka.
Lakini, utamaduni wa watu kusimamia haki zao za kikatiba ni muhimu zaidi. Bila huu utamaduni katiba mpya haitakuwa na maana.
Kwanza hamuwezinhatabkupatabkatiba mpya nzuri. Mkioata mpya mtagundua mapungufu na kudai mpya zaidi. Kwa sababu hata hiyo mpya hamtaipata kwa umakini, kwa sababu ya kukosa utamaduni wa kuishi kikatiba.
Lets say maximum efficiency ya katiba ni 100%. Tuiite katiba inayofikia hii maximum efficiency katiba A.
Let's say katiba yetu ya sasa, katiba B, haifiki hiyo 100% maximum, maximum efficiency ya katiba yetu sasa, katiba B, ni 50% ya katiba A.
Tukiweza kuitumia katiba yetu B kwa 100% efficiency tutapata 50% efficiency ya katiba A.
Katiba B si nzuri sana, ina efficiency ya 50% tu, lakini tumeweza kuitumia hiyo hiyo mbaya fully, tukapata efficiency 50%.
Halafu, watu wanaotumia katiba A, yenye potential efficiency ya 100%, wanaitumia kwa level ya efficiency 20% tu.
Hapo utaona hao wenye katiba bora maradufu zaidi yetu wanaitumia vibaya na kupata efficiency ya 20%, wakati sisi tuna katiba mbaya zaidi yao lakini tunaitumia vizuri zaidi na kupata efficiency ya 50%.
Kwa hivyo, mabadiliko ya katiba ni muhimu, tunayahitaji, lakini kitu muhimu zaidi ni uwezo wa watu kuisimamia katiba, utamaduni wa kuheshimu na kuisimamia katiba ni kitu muhimu zaidi ya kuwa na katiba mpya tu.