Mnaomshambulia RC wa Arusha, mnafurahia kiongozi wetu kutukanwa?

Mnaomshambulia RC wa Arusha, mnafurahia kiongozi wetu kutukanwa?

Hii ni logical fallacy, inaitwa ad hominem.

Umeshindwa kwenye hoja, unamkashifu mtoa hoja.

Kwa sababu huna hoja.

By the way. Bika watu wabishi usingekuwa na teknolojia hii ya kuwasiliana kwenye internet. Kuna watu waliibishia dunia ya kuwasikiana kwa barua wakaweka teknolojia ya kuwasikiana kwa urahisi zaidi.

Kwa hivyo usiubeze ubishibkama kitu kibaya.

Mara nyingi sana maendeleo yanahitaji watu wabishi wabishie mawazo potofu ya kizamani ili kusogeza jamii mbele.

Kujionheza kwa Hegelian dialectic ya thesis, antithesis na synthesis haiwezekani kufanyika bila ubishi.

Na hiyo ndiyo imebeba maendeleo yote ya kimantiki na kisayansi.

Kwa hiyo, usibeze ubishi.
Sawa,

Ngoja nipate chochote tumboni,

Nakurudia.
 
Sawa,

Ngoja nipate chochote tumboni,

Nakurudia.
Wewe nawe pia ni mbishi.

Inaonekana unapenda ubishi kuliko kuweka kitu tumboni.

Hata unapokwenda kuweka kitu tumboni, unaweka nukta kwenye ubishi na kuukamia kwa kusema "nakurudia" 🤣🤣🤣.
 
Salaam, shalom!!

Nimefuatilia hotuba fupi ya RC wa Arusha, ilijaa utulivu na mtiririko uliopangika kabisa, hivyo kusema kuwa aliropoka, Si Kweli, alidhamiria kusema aliyosema,

Tangu Mropokaji yule achafue Hali ya hewa majuzi, Waziri wa habari hakusema chochote, waziri wa Mambo ya nje kadharika aliamua kukaa kimya, Hilo pekee linatosha kumpa RC ujasiri wa Kutoka kukemea,ukizingatia, ameyasema hayo ndani ya Mkoa wake kimamlaka.

Kwa kuwa watu wale wale waliomtukana Shujaa Magu, ndio hao hao wanaorudi kumtukana Sa100
, ni sawa kabisa RC atoke kukemea.

NB: Kwa kuwa tumekubali kutolewa katika mijadala muhimu kama Tume ya Uchaguzi kubadilishwa Jina,KATIBA mpya, DP world kuanza KAZI bila kutaja wamewekeza Bei Gani, Ripoti ya CAG kuwekwa pembeni Kwa kuibua HOJA hafifu za kujadili matusi, basi tuendelee!!!

Karibuni🙏
Madam President ana machawa kibao Sasa kwanini Wasiwe wanayajibu haya matusi kwa Data
 
CDF hajui, IGP hajui, DG TISS hajui, CM PSU hajui, lakini yeye anajua. Ameona Mawaziri wakituma pesa kwa Mange ili amtukane Rais, lakini wala hakumwambia. Alikaa kimya akaacha mama adhalilishwe karibu wiki nzima, halafu akasubiri leo ndo asemee jukwaani. Ina maana leo asingepewa jukwaa angeendelea kukaa kimya? Kwanini ile siku ya kwanza mama anadhalilishwa asingemwambia kuwa kuna mawaziri wanamlipa Mange kukuchafua? Aisee inahitaji degree nyingi sana za ujinga kumuelewa huyu jamaa. DAB the CDF. DAB the IGP. DAB the DG TISS. DAB the Jack of all trades but the Master of None
👏💐
 
Madam President ana machawa kibao Sasa kwanini Wasiwe wanayajibu haya matusi kwa Data
Matusi hayajibiwi Kwa data,

Kinachotakiwa, ni kutenganisha matusi pembeni, HOJA pembeni, Kisha unajibu HOJA na kupuuza matusi.
 
We ni mbishi sana, kama tu watu wa chigoma[emoji3]
Nimefuatilia mjadala hapo juu, Wewe ndio kichwa maji.

Una ambiwa kama tu katiba iliyopo Magufuli aliweza kwenda kinyume nayo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kumwajibisha, Je unadhani ikija katiba mpya ndio itafatwa?

Kama katiba hii iliyopo haifuatwi, Je unadhani viongozi hawahawa watafuata hiyo katiba mpya?

Hivi unafikiri sawasawa kweli?
 
Mimi Niko sahihi,

Nenda hapo Kenya Pana Katiba mpya inayowalazimisha viongozi waifuate, Si kuwabembeleza kuifuata Kwa hiari na utashi wao.
 
Nimefuatilia mjadala hapo juu, Wewe ndio kichwa maji.

Una ambiwa kama tu katiba iliyopo Magufuli aliweza kwenda kinyume nayo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kumwajibisha, Je unadhani ikija katiba mpya ndio itafatwa?

Kama katiba hii iliyopo haifuatwi, Je unadhani viongozi hawahawa watafuata hiyo katiba mpya?

Hivi unafikiri sawasawa kweli?
Katiba mpya haita mpa madalaka ya kuteua majaji na wengine wote wenye uwezo wa kusimamia Sheria kuhakikisha haipindishwi.
 
Katiba mpya haita mpa madalaka ya kuteua majaji na wengine wote wenye uwezo wa kusimamia Sheria kuhakikisha haipindishwi.
Wanajitoa ufahamu,

Kibri Cha kutofuata Katiba linatokana na Kinga na mamlaka ya juu na kutoshtakiwa.

Rais ni sehemu ya bunge, bunge linaanzaje mchakato wa kupeleka HOJA ya kutokuwa na Imani naye?
 
Kwa hiyo na wewe unaamini kuna watendaji na washauri wa karibu wa Rais (Mawaziri) wanamtukana Bosi wao! Kama ni kweli basi inawezekana huyo Bosi wao atakuwa ana mapungufu mengi ya kiuongozi bila shaka.
Tamaa tu hakuna cha mapungufu mengi.
 
Katiba mpya haita mpa madalaka ya kuteua majaji na wengine wote wenye uwezo wa kusimamia Sheria kuhakikisha haipindishwi.
Katiba iliyopo haimruhusu Raisi kufunguia mikutano ya kisiasa.

Lakini Magufuli aliweza kwenda kinyume na katiba hii iliyopo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kumwajibisha.

Sasa kama katiba hii tu iliyopo haifuatwi na inapindishwa, Je unadhani hiyo katiba mpya itafatwa?
 
Asingekuwa na Kinga ya kutoshtakiwa,

Asingediriki kuzuia mikutano ya hadhara.

Mamlaka ya Rais makubwa, ndiyo chanzo Cha matatizo yetu nchini.
 
Matusi hayajibiwi Kwa data,

Kinachotakiwa, ni kutenganisha matusi pembeni, HOJA pembeni, Kisha unajibu HOJA na kupuuza matusi.
Kinachosanabisha matusi ni hali halisi ya yanayoendelea huku mtaani. Kama mambo yangekuwa yapo sawa haya matusi yasingethiri halafu kumbuka haya matusi yapo toka enzi za Mitume. Ni kawaida sana na hauwezi ukazuia mihemko ya watu.wacha tuone hao watu wakitajwa kama matusi yatakoma
 
Katiba iliyopo haimruhusu Raisi kufunguia mikutano ya kisiasa.

Lakini Magufuli aliweza kwenda kinyume na katiba hii iliyopo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kumwajibisha.

Sasa kama katiba hii tu iliyopo haifuatwi na inapindishwa, Je unadhani hiyo katiba mpya itafatwa?
Unaanzaje kumchukulia hatua au kumuwajibisha aliyekufinyanga akakuweka ulipo.
 
Back
Top Bottom