- Thread starter
- #41
Mbona unajipinga mwenyewe?Mamlaka makubwa ya rais yanatakiwa kumpa control kubwa zaidi rais katika kufanya vetting kuchuja watu wa ovyo.
Mimi si mtetezi wa rais kuwa na mamlaka makubwa, lakini nitakuonesha jinsi mamlaka makubwa ya rais yalivyo advantage na si disadvantage kwa rais hapa.
Rais Mkapa alikuwa anataka kuteua mtu wa kuongoza PSRC (Parastatal Sector Reform Commission). Nafikiri Mzee George Mbowe alikuwa anaondoka, mwaka 1998. Kwa kuelewa umuhimu wa kiongozi wa taasisi hii, rais Mkapa aliwafanyia phone tapping kwa zaidi ya mwaka mzima watu fulani waliokuwa wanaonekana kuweza kufaa kazi hiyo.
Watu walikuwa wanasikilizwa simu zao na serikali ya Mkapa kwa zaidi ya mwaka mzima kama sehemu ya vetting.
Rais alitumia turufu yake ya "usalama wa taifa". Madaraka makubwa ya rais yalimruhusu kufanya hivyo.
Mwishowe, rais Mkapa akajiridhisha kuwa John Rubambe atafaa kushika nafasi hii. Akamteua.
Sasa hapo nguvu kubwa za rais si disadvantage katika kufanya vetting, ni advantage.
In this case, ukikubali anayosema Makonda, kuna tatizo la vetting. Au labda kuna tatizo la rais kuwa na uwezo mdogo. Au labda kuna tatizo la kiutamaduni.
Haya si matatizo ya kutatuliwa na katiba mpya.
Kama rais hafanyi vetting, hana uwezo, au ana utamaduni mbaya, haya matatizo hayatatuliwi na katiba mpya.
Mamlaka makubwa ya rais, kwa rais, hapo ni advantage, si disadvantage.
Kuna tatizo tofauti ambalo hutaki kuliangalia kwa sababu ushajikubalisha na kujikaririsha boilerplate answer ya "katiba mpya".
Ukikubali maneno ya Makonda, kuna matatizo ya utamaduni, vetting, politics, sasa hayo matatizo utayatatuaje kwa katiba mpya?
Samia alisema katiba ni kijitabu tu. Watanzania wengi hawakumuelewa wakamshambulia.
Lakini, kama kuna mambo machache ninayokubaliana na Samia ni kauki ile.
Mimi naheshimu sana utawala wa sheria, napenda sana mabadiliko ya kikatiba.
Lakini, katiba ni kijitabu tu. Maana yake ni kwamba, zike kanuni za kikatiba zinatakiwa kuishi kwenye vichwa vya watu, siyo watu wanataka demokrasia kwenye katiba halafu wao mafashisti madikteta.
Hakuna kifungu cha katiba kinachokubali mawaziri kumtykana rais. Hakuna tatizo la kikatiba hapa.
Tuache kutupia kila tatizo kwenye kichaka cha "katiba mpya".
Sasa kama una mawaziri wa ovyo wanaomtukana rais, kama una rais wa ovyo asiyejua kuchuja watu anaowateua kuwa mawaziri, hapo katiba mpya itakusaidiaje?
Unadai mamlaka makubwa ya Rais ni advantage kwake kufanya vetting, hapo hapo akawarudisha vijana wale wale waliotimuliwa Kwa utovu wa nidhamu wakati wa magu, hapo hapo unasema Rais hafanyi vetting ipasavyo!!
Na nani Hasa hufanya vetting, ni Taasisi ya Urais au Rais?