Mnaomshauri Rais juu ya Ikulu mpya Chamwino muogopeni Mungu

Una hoja ya maana. Tatizo la watawala wa siku hizi ni umachinga na kushindwa kuwa wabunifu. Ikulu na kumbi za walevi wapi na wapi? Kesho wataingia vyangudoa, wauza madawa na mateja kiasi cha kufanya usalama wa rais kuwa hatarini. Ikulu, kama alivyosema marehemu baba wa taifa, ni mahali patakatifu. Watu wachafu wasiende kule. Kule hakuna biashara. Ni ofisi ya umma. Samia amenikumbusha uhovyo wa mzee Ruhusa na baadaye Njaa Kaya. Sijui hapa tatizo ni malezi au mazingira wala sijui.
Walienda kuchukua ramani ulaya huko sijui nchi gani, na kwa wabongo walivyo wakafikia hotelini wakala bata wakapewa ramani feki, sawa na yule aliyepewa maboksi ya dawa ya korona feki.

Hawa wasomi wetu walishindwa nini kuchora mchoro wa ikulu ?

Ulisikia wapi ikulu ndani mna soko?
Katika nchi yoyote, Ikulu is one of the most, if not the most secure premise. Maana hapo ndio ofisi za madaraka ya juu kabisa.

Pamoja na kupongeza ujenzi wa Ikulu mpya Chamwino, nimeshangazwa sana na mapendekezo mapya ya majengo ya huduma.
Pengine kama sijaelewa maana yake.
-Kutakuwepo na jengo la Samia Complex,
-Ukumbi wa mkutano wa watu 2000 hadi 3000.
-Uwanja wa ndege.
-Jengo la Zanzibar
-Majengo ya East Africa

Sasa hapo nikajiuliza unapokaribisha umati kama huo wa watu ndani ya Ikulu, na wahudumu ambao kazi zao si za moja kwa moja na shughuli za Ikulu, na ukumbi ambao hauna commercial use, maana yake nini kiuhalisia?

Usalama wa Ikulu yenyewe kama hiyo itakuwa na gharama kubwa .
Kwa 98% , majengo pendekezwa yatakuwa hayatumiki kwa day to day business.

Pale Ukumbi wa CCM Jakaya Kikwete, ukumbi uko mjini lakini kuna popo, maana matumizi yake kwa mwezi ni mara moja au mbili.
Kama kuna mikutano mfululizo pengine mara moja ndani ya miezi mitano au sita.

Washauri wa Rais, kwani hamuoni hiyo mis use ya public funds?

Si tu kujenga white ekephants lakini ni kuchezea kodi zetu, ambazo wana Kariakoo wametuwakilisha vema zinavyotuumiza.
Nadhani huyu mama hana mpango na hiyo ikulu kiviile. Mmeshamuona asivyo na vinasaba na Dodoma. Kwahyo ili isikae bure kwa muda mrefu (kama ambavyo tumeshaona), amediversify.

Na kuna ile akili flan ya kusema "mama yuko poa sana, si umeona saivi ikulu tunaingia tuu" hiyo ndo akili wameitarget hapo. Nyinyi watu conscious sio favourite kwa maamuzi ya kisiasa.
 
Nadhani huyu mama hana mpango na hiyo ikulu kiviile. Mmeshamuona asivyo na vinasaba na Dodoma. Kwahyo ili isikae bure tukalalamika, amediversify.

Na kuna ile akili flan ya kusema "mama yuko poa sana, si umeona saivi ikulu tunaingia tuu" hiyo ndo akili wameitarget hapo.
Tutamkumbuka Mwalimu aliyesema , Ikulu si mahali pa mchezo mchezo au pango la walanguzi. Ikulu inatakiwa kuwa mahali patakatifu.
 
Katika nchi yoyote, Ikulu is one of the most, if not the most secure premise. Maana hapo ndio ofisi za madaraka ya juu kabisa.

Pamoja na kupongeza ujenzi wa Ikulu mpya Chamwino, nimeshangazwa sana na mapendekezo mapya ya majengo ya huduma.
Pengine kama sijaelewa maana yake.
-Kutakuwepo na jengo la Samia Complex,
-Ukumbi wa mkutano wa watu 2000 hadi 3000.
-Uwanja wa ndege.
-Jengo la Zanzibar
-Majengo ya East Africa

Sasa hapo nikajiuliza unapokaribisha umati kama huo wa watu ndani ya Ikulu, na wahudumu ambao kazi zao si za moja kwa moja na shughuli za Ikulu, na ukumbi ambao hauna commercial use, maana yake nini kiuhalisia?

Usalama wa Ikulu yenyewe kama hiyo itakuwa na gharama kubwa .
Kwa 98% , majengo pendekezwa yatakuwa hayatumiki kwa day to day business.

Pale Ukumbi wa CCM Jakaya Kikwete, ukumbi uko mjini lakini kuna popo, maana matumizi yake kwa mwezi ni mara moja au mbili.
Kama kuna mikutano mfululizo pengine mara moja ndani ya miezi mitano au sita.

Washauri wa Rais, kwani hamuoni hiyo mis use ya public funds?

Si tu kujenga white ekephants lakini ni kuchezea kodi zetu, ambazo wana Kariakoo wametuwakilisha vema zinavyotuumiza.
Rais anawasikiliza wahuni. Wao wanachojua ni kuzua kandarasi ili wale cha juu na commission. Hata white house marekani haina uwanja wa ndege. Sasa majengo ya zanzibar jengo la EAC ndani ya ikulu ya nini yote? Kuna mji wa serikali sasa mji wa ikulu wa nini tena🤣😂
 
Pesa za serikali huwezi kuzijaza kwenye sandarusi ukakimbia nazo, lazima utazua taharuki kubwa sana.

Chakufanya jenga, jenga, jenga hata visivyo na tija, kwenye kujenga tumia kalamu kukwapua, utakuwa umepata faida mara mbili, kwanza; umekwapua, pili; wanyonge watakupigia makofi, watakushangilia na watakuimbia mapambio bila kujali hilo jengo litawafaidisha wao ama lah!
 
Anzisha mada yako yenye maudhui hayo.
Tukiona makosa ya dhahiri sasa hivi siye tunatwanga tu haijalishi ni nani
Wewe twanga sisi tunapepeta.

Unaonesha hujaupenda ukweli. Swali liko palepale, nani aliyeamuwa makao makuu ya nchi yahamie Dodoma?
 
Rais anawasikiliza wahuni. Wao wanachojua ni kuzua kandarasi ili wale cha juu na commission. Hata white house marekani haina uwanja wa ndege. Sasa majengo ya zanzibar jengo la EAC ndani ya ikulu ya nini yote? Kuna mji wa serikali sasa mji wa ikulu wa nini tena🤣😂
Ikulu complex, siyo? ngozi nyeusi tuna shida sana............kwamba hicho ndo tumeona kipaumbele!
 
Wewe twanga sisi tunapepeta.

Unaonesha hujaupenda ukweli. Swali liko palepale, nani aliyeamuwa makao makuu ya nchi yahamie Dodoma?
Nikikuweka kama mtu mwenye akili kumbe ni wale wale!
Kupeta tunapeta wengi, ila ukinyea kambi kwa gharama za kodi zangu nakufa na wewe, kwa maoni tu!
 
Dua ya kuku.

Wewe kodi ulipe au usilipe, maamuzi ya kuifanya Dodoma makao makuu ya serikali yalishafanyika mwaka 1971. Kumbuka hilo.
 
Wajipange pawe na muonekano wa mpangilio ingawa sijaafiki uamuzi wao wa kuhamia Dodoma lakini ndiyo hivyo tena tayari wamefanya Dodoma ni makao makuu hivyo hata ikulu ramani ya eneo hilo na mji mzima wa Dodoma ufuate mipango miji unaoeleweka kwani tupo mwaka 2023

1684828674425.png

Kama ni "kuchezea kodi" basi aliyeleta wazo la kuhamishia makao makuu Dodoma na kuziasisi CDA ndiye mwenye makando makando hayo. Unamkumbuka ni nani?
Kuna watu mna mentality ya laissez faire!
Bad business as usual!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kwani rais ni adui wa wananchi? Mleta mada, ninyi ndiyo mnaowafanya marais wa Afrika wajione miungu-watu.

Mbona kule ikulu ya Marekani kuna vituo vya redio, maofisi ya makampuni, swimming pool n.k ambapo watu hufanya kazi na kustarehe kama kawaida.
 
Katika nchi yoyote, Ikulu is one of the most, if not the most secure premise. Maana hapo ndio ofisi za madaraka ya juu kabisa.

Pamoja na kupongeza ujenzi wa Ikulu mpya Chamwino, nimeshangazwa sana na mapendekezo mapya ya majengo ya huduma.
Pengine kama sijaelewa maana yake.
-Kutakuwepo na jengo la Samia Complex,
-Ukumbi wa mkutano wa watu 2000 hadi 3000.
-Uwanja wa ndege.
-Jengo la Zanzibar
-Majengo ya East Africa

Sasa hapo nikajiuliza unapokaribisha umati kama huo wa watu ndani ya Ikulu, na wahudumu ambao kazi zao si za moja kwa moja na shughuli za Ikulu, na ukumbi ambao hauna commercial use, maana yake nini kiuhalisia?

Usalama wa Ikulu yenyewe kama hiyo itakuwa na gharama kubwa .
Kwa 98% , majengo pendekezwa yatakuwa hayatumiki kwa day to day business.

Pale Ukumbi wa CCM Jakaya Kikwete, ukumbi uko mjini lakini kuna popo, maana matumizi yake kwa mwezi ni mara moja au mbili.
Kama kuna mikutano mfululizo pengine mara moja ndani ya miezi mitano au sita.

Washauri wa Rais, kwani hamuoni hiyo mis use ya public funds?

Si tu kujenga white ekephants lakini ni kuchezea kodi zetu, ambazo wana Kariakoo wametuwakilisha vema zinavyotuumiza.
Hii nchi kuna wakati unajiuliza hupati jibu. Hivi kwenye maamuzi upande wa Serikali, kuna watu wa namna gani?

Maana hata vile vitu vinavyohitaji tu very basic logical thinking, inakuwa ni tatizo kubwa. Yaani ukaweka ukumbi wa mikutano ikulu, kwaajili ya nini? Tatizo planning zetu zipo hovyo hovyo kabisa. Angalia iliko ofisi ya Waziri mkuu, karibia kilometer 40 toka iliko ikulu ya Rais. Ikulu mpaka ofisi za Serikali karibia kilometer 20. Waziri mkuu akitoka kwenye ofisi ya makazi yake kwenda ikulu, ni kusababisha foleni kubwa za magari. Rais akiitisha kijao cha mawaziri, barabara nzima ni msululu wa magari ya mawaziri.

Ikulu ipo mbali sana kutoka ofisi zote za Serikali, na wamechukua maelfu ya ekari. Sasa ili kusiwe pori wanalazimisha kwenda kuweka majengo huko ili ikulu isiwe hifadhi ya msitu. Lakini hivyo wanavyovipeleka huko, vyote havitakuwa na matumizi, ni utapanyaji wa fedha. Mikutano mingi mikubwa ya kimataifa itaendelea kufanyikia Dar es Salaam na Arusha kwa sababu kuna miundombinu.

Ebu fikiria hao wafanya maamuzi walioamua uwanja wa ndege uwe ndani ya eneo la ikulu, uliwahi kuona wapi? Au ni uwanja wa ndege wa kutumia tu Rais? Na kama uratumika na Rais tu, hivi huo siyo utapanyaji wa fedha za umma?

Hii nchi haitaondokana na umaskini kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Huku Bashe anatapanya pesa kwa kupitia miradi isiyo na uhalisia kwenye kilimo, ikulu nayo inatapanya pesa kupitia ujenzi wa majengo yasiyo na tija, Nape ametapanya pesa nyingi kupitia vibao vya mitaa, January anatapanya pesa kwa kuendelea kuweka nguzo za umeme za miti na alikokwishaweka anaenda anaziondoa na kuweka nguzo za zege. Yaani kila mmoja anajitahidi kutafuta kitu kitakachompa uhalali wa kutapanya pesa ya walipa kodi.
 
Du bibie hivi uliwahi kuwa na akili?
Kinachoongelewa na unachoongea ni vitu viwili tofauti.
Au kama unavyosema mwenyewe , umekaririshwa ujinga!
Kuitatuwa fitna ni lazima tuutafute mzizi wake.

Kuna kipi hapo cha kutumia akili?
 
Katika nchi yoyote, Ikulu is one of the most, if not the most secure premise. Maana hapo ndio ofisi za madaraka ya juu kabisa.

Pamoja na kupongeza ujenzi wa Ikulu mpya Chamwino, nimeshangazwa sana na mapendekezo mapya ya majengo ya huduma.
Pengine kama sijaelewa maana yake.
-Kutakuwepo na jengo la Samia Complex,
-Ukumbi wa mkutano wa watu 2000 hadi 3000.
-Uwanja wa ndege.
-Jengo la Zanzibar
-Majengo ya East Africa

Sasa hapo nikajiuliza unapokaribisha umati kama huo wa watu ndani ya Ikulu, na wahudumu ambao kazi zao si za moja kwa moja na shughuli za Ikulu, na ukumbi ambao hauna commercial use, maana yake nini kiuhalisia?

Usalama wa Ikulu yenyewe kama hiyo itakuwa na gharama kubwa .
Kwa 98% , majengo pendekezwa yatakuwa hayatumiki kwa day to day business.

Pale Ukumbi wa CCM Jakaya Kikwete, ukumbi uko mjini lakini kuna popo, maana matumizi yake kwa mwezi ni mara moja au mbili.
Kama kuna mikutano mfululizo pengine mara moja ndani ya miezi mitano au sita.

Washauri wa Rais, kwani hamuoni hiyo mis use ya public funds?

Si tu kujenga white ekephants lakini ni kuchezea kodi zetu, ambazo wana Kariakoo wametuwakilisha vema zinavyotuumiza.
😀 Hiyo itakuwa siyo Ikulu tena bali ni Chamwino Business Complex Centre.
 
Ni kweli kaka lakini kutokana na unyeti wa ikulu na udhaifu wa ulinzi wetu ulio legezwa na wana siasa watu ndio wanakuwa na mashaka na hilo, kumbuka sasa Dunia imekuwa ina mambo mengi sana hasa ya ugaidia nk.
Ni kweli hoja yako
 
Back
Top Bottom