Kwanza naunga mkono yote uliyosema hapa, naomba nami kupitia hapa niongeze machache kuhusu mapungufu ya tukio la uzinduzi wa ikulu ya chamwino...
Moja, Hivi ni kwa nini hakukuwepo watoto wetu yaani wanafunzi wa shule na vyuo, tena pengine ilitakiwa wawepo kuanzia wale pre nursery..kwa sabab ikulu ni urithi wao na si wa hao walioalikana, tunashindwa kuonyesha thamani ya uwepo wa watoto wa Taifa hili kwa nini lakini..kuna faida gani kumualika Mpoto na Bella ili hali kila leo tunawaona na wanayosema wala si mageni masikioni mwetu, wangealikwa wanafunzi shule hata 3 tu wakaimba nyimbo nzuri kwa niaba ya wenzao ingeleta furaha, baraka na faraja, watoto mahali popote wana nafasi ya pekee, hata penye mifarakano watoto huleta mapatano..kama tunawatoa watoto kwenye matukio muhimu kama la jana, hivi ni wapi tena tunaweza kuwafundisha kupenda taifa lao, kujitegemea, utii, kupenda vitu vya kwetu nk, wapi??
Tatizo kubwa la wasaidizi wa viongozi kwanza ni mentality ya anasa, pili uchovu wa akili na ulevi wa kuaminiwa! Mambo mengi sana wanatukosea tena mara kwa mara..hivi kuna mzazi huwa anahangaika wakati wa sherehe za kiimani kuandaa mavazi, chakula, mapambo kwa ajili ya wageni halafu watoto wako wachafu, hawajaandaliwa kushiriki pasaka au idd, ndio hivyo kweli? wageni wanaojitambua wakikuta hali ya namna hiyo watatoa udhuru wa kuondoka mapema wakuachie hayo yote uliyoandaa utumie peke yako! Sababu utakuwa umekosea pakubwa mno! Watoto wanapaswa kuwa waalikwa namba moja!
Kuonyesha uungwana waandaji mtutake radhi tafadhali, sisi hatutoi kodi yetu zitumike kufadhili anasa za watu wazima kama sisi!
Jambo la pili, Mh. Rais alisema itajengwa complex ikulu hadi viwanja vya gofu, hivi jamani kwa nini tuna fikiria sana burudani kuliko kazi? Ikulu ni sehem ya kazi, hayo mengine yote ya nini? Tuna uhakika gani baada ya miaka 40 ijayo watakaokuwepo watatumia? Haina haja kabisa, hivyo ilivyo inatosha, madam nafasi ipo ya kutosha, huko mbele kama wataona hayo ni ya maana wataweka wao, hata mzazi anapojenga nyumba huweka vile vitu vya msingi tu, siku hayupo yule atakayerithi akiona anayotaka yeye yanakosekana ataweka yeye ili pia awe na uchungu wa kutunza, ukiweka kila kitu unaweza jikuta unapoteza nguvu, muda na rasilimali bure sabab siku haupo hakuna atayetumia tena, sasa si bora nguvu ulizotumia ungetoa sadaka zisaidie wahitaji..tusiweke mbele sana mtazamo wa kuonyesha ufahari hata kama haihitajiki..TUJIREKEBISHE!