Mnaomshauri Rais juu ya Ikulu mpya Chamwino muogopeni Mungu

Eneo lenyewe ekari 8,473 wajenge tu facilities zote.

Who knows? Ipo siku hata Mimi naweza jikuta naogelea swimming pool la Ikulu na kucheza golf huku Rais yupo mafichoni kama ilivyokuwa kwa waandamanaji nchini Sri Lanka.😁



BTW:Akiharibu lawama mnawatwisha washauri,akifanya vyema hatuwasikii washauri wakitajwa.
 
yuko afande(kwa kadri ya simulizi) mmoja wa jeshi kipindi cha Idd Amin alikuwa anawaambia watu wake na kikosi chake wasonge mbele kwa kidole lakini akitumia matamshi yafuatayo Bantu ba mkaya mkiogo huku akionyesha kidole mbele kwa hiyo natumaini mnanielewa pia.
 
Tupo wadau, tunaendelea kuwafuatilia wajuzi wa jf wakiendelea kudadavua wanachokijua......πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Complex ya Samia. Ana tabia kama za Kenya, kila kitu kiliitwa Kenyatta na Moi kana kwamba wangeiishi milele. Shame on them and her
Jamani ikulu zote dunia zinahitajika kuwa self sufficient kwa mahitaji yote muhimu. Kumbi za mikutano, migahawa au hoteli kwa ajili ya wafanyakazi, makazi ya rais na wafanyakazi muhimu ambao ni wasaidizi wa rais, kwa kutaja kwa uchache!

Ikulu ni taasisi inayojitosheleza kwa kila kitu katika kuendesha nchi na kufanya maamuzi.
 
Most protected, Highly protected. Usitumie secure! Inaweza ikawa protected lkn isiwe secure.
 
Tupo wadau, tunaendelea kuwafuatilia wajuzi wa jf wakiendelea kudadavua wanachokijua......πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
Poa mkuu, saidieni kuwaeleza vijana wa kileog, hata handaki hawajui linafananaje!
 
Kwani rais ni adui wa wananchi? Mleta mada, ninyi ndiyo mnaowafanya marais wa Afrika wajione miungu-watu.

Mbona kule ikulu ya Marekani kuna vituo vya redio, maofisi ya makampuni, swimming pool n.k ambapo watu hufanya kazi na kustarehe kama kawaida.
UONGO
 
Eneo la Ikulu ni kubwa mno. Kilometa za mraba 34 sio mchezo. Wanaweza kuweka kila kitu humo na likabaki eneo kubwa kama la Dar nzima na zaidi. 34km ni kama kutoka posta mnara wa Askari hadi Kiluvya. Au kutoka Arusha Mianzini hadi Kikatiti. Acheni Rais atengeneze Legacy
 
Ni kweli kaka lakini kutokana na unyeti wa ikulu na udhaifu wa ulinzi wetu ulio legezwa na wana siasa watu ndio wanakuwa na mashaka na hilo, kumbuka sasa Dunia imekuwa ina mambo mengi sana hasa ya ugaidia nk.
Karibu na ikulu ya Dar hakuna Kambi za mikutano?
 
Hivi na yeye akujua alichoongea si kitu kizuri hadi aseme public

Kasuku style....
 
Kwani rais ni adui wa wananchi? Mleta mada, ninyi ndiyo mnaowafanya marais wa Afrika wajione miungu-watu.

Mbona kule ikulu ya Marekani kuna vituo vya redio, maofisi ya makampuni, swimming pool n.k ambapo watu hufanya kazi na kustarehe kama kawaida.
Ha ha ha!
Acha ndoto za kufikirika.
Mimi nimefika Pennsylvania Avenue na kupiga picha mbele ya fence ya White House.
Hicho unachoongelea ni imagination yako!
 
Habari nzima ya kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma ni white elephant project, si Ikulu tu.

Tumetatua tatizo ambalo hatuna, wakati matatizo ambayo hatuna hatujayatatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…