Mnaonaje tubadili katiba yetu ili Rais Samia aendelee kuongoza Taifa letu baada ya kumaliza muhula wake 2030?

Hilo ndo hitaji la wananchi wengi kwa sasa. Inabidi wabunge wafanye kitu pale kwenye katiba ili Mama aendelee kuongoza angalau hadi 2035.
Mnaweza kubadili katiba ili bimkubwa awe malikia wa milele kwe uchaguzi mkishindwa kuiba kura lisu anakua mfalme wenu wa milele
 
Naona leo unabubujikwa mpaka unajisahau. Hata wenzio wa Chato walisema hivyohivyo bila kujua kuwa Mungu sio athumani.
 
Mimi nimeongea kizalendo
Chunga kauli aisee , ila kweli hakuna jambo au utawala usio na mwisho , wahenga walisema hakuna marefu yasio na ncha , kama Roman, persian na Ottoman Empire zilidondoka kwani hIi empire ya Kijani na utawala wake Dhalim kwa wanyonge isidondoke, ivii unafaham kuna watu mpka sa iz wanaish chini ya Dolla 1, bado wanafunzi wanasoma chini bila madawat hii inatokana na nn, afu mawaziri na wabunge wanakukula mishahara above 5 mill na kutembelea magari yenye thamani sawa na shule moja ya kata , afu mnasema nchi yakizalendo tafakuri kwa hilo....!!!?
 
Kama kikwete angeongezeaa tungempataje Samia ambaye ni bira kuliko JK. Na je hauoni tuna weza kumpata bora zaidi kuliko Samia?
 
Basi tubadili katiba ili tupate katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Na mamlaka ya rais yapunguzwe kwa kiasi kikubwa hasa nafasi za uteuzi kama ilivyokuwa kwenye rasimu ya jaji Warioba.

Waziri asitokane na mbunge.

Vyeo vya kichawa kama ukuu wa mkoa visiwe vya uteuzi bali watu wagombee na kupitia michujo mikali ikiwemo midahalo ya moja kwa moja.

Uwepo mdahalo wa wagombea urais na urushwe moja kwa moja na asitokee mgombea kuukwepa bila sababu za msingi.

Kura zipigwe kwa njia ya kielektroniki na matokeo yawe kwa real time data la si hivyo kura zihesabiwe kwa uwazi kukiwepo na camera huku walio nje wakiona yote yanayoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…