Mnaoomba Mungu na anawasikiliza uwa mnatumia mbinu gani?

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2019
Posts
331
Reaction score
708
Kuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.

Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.

Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.

Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.

Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.

Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.

Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.

Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.

Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?

Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?

Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?

Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?

Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.
 
Mungu hakujibu maana una mkataba halali na shetani. Huwa haingilii vita visivyomuhusu. Mwanzo ulionewa ila kutafuta suluhisho hukumwamini bali ulijitahidi kumsaidia. Kama unataka msaada wake nenda kwake humbly, mwambie nimechoka nimeshindwa nisaidie. Kwa Mkristo nenda na Damu ya Yesu. Kwa mwislamu sijui aisee. Nenda kwa Imani, Lia uchungu wa ndani yeye anauona moyo wako. Mwambie vunja mikataba yote niliyoingia na waganga kwa niaba ya shetani. Ukishatubu nenda akasome zaburi ya 109 kwa Imani juu ya watesi wako. Lakini, kusamehe, utubu kwa kumaanisha. Ukiiomba kwa Imani ataijibu pia atakufungua vifungo vyako.
 
Riziki mtu hupewa na Mungu au shetani hii ndio kanuni ya kiroho...

Amua kuwa ama moto au baridi lakini usiwe vuguvugu...

Walio wa Mungu wamefanikiwa kwa sababu wamechagua upande huo na wamejishikiza huko kweli kweli na sadaka zao ni huko...

Walio wa shetani nao hivyo hivyo wamefanikiwa kwa sababu wapo huko na wanajitoa kweli kweli...

Tabu ipo kwa wale wa vuguvugu ambao kila upande unataka, na kila upande unakutema...
 
Kuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.

Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.

Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.

Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.

Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.

Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.

Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.

Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.

Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?

Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?

Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?

Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?

Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.
1. Lazima uwe msafi yaani uishi maisha yanayo mdendeza Mungu
2. Jitahidi ufanye maombi yako saa 8 usiku
 
Badilisha mganga, huyo wa kwanza sio mtaalamu kwenye masuala unayo taka.
Nimeroga sana ndugu yangu, hata uzima wangu niliupata kwa mganga wa kipemba. Nilikaa mwaka nadondoka hovyo hospital awaoni ugonjwa nikaponea kwa mganga ila kuna mambo alijaribu ya rizki naona akachemka.
 
Kwanza pole sana expert wangu,nimeguswa sana na changamoto zako,ndio maisha yalivyo wala usijione uko peke yako kuna wenzako wengi hawajapata sehemu ya kusemea

Kwanza ieleweke kwamba Mungu hampi mtu riziki labda kwasababu ni mwema au muovu,ila humpa riziki kubwa amtakaye na humpa ndogo amtakaye

Ndio maana kuna watu waovu hawaendi makanisani wala misikitini lakini wanapata riziki yao vizur sana tena saa nyingine zaidi hata ya wachamungu,ila huko akhera watalipwa mema watu wema

Anza kwa kuomba toba,Mungu anasema haya majanga na mitihani tunayopitia ni kutokana na matendo ya mikono yetu wenyewe

Wakati mwingine kuna mambo ambayo tumeyafanya katika maisha yetu ndio ikawa sababu ya kupata mitihani ambayo tunayo leo

Lakini wakati mwingine ni mitihani tu ambayo mja anapewa na Mola wake,kikubwa ni subira na kuzidi kuomba kwa imani thabiti

Nabii Ayubu aliumwa kwa miaka 18 na ni nabii huyo,lkn alifanya subira na kuomba bila kuchoka

Kwahiyo wa kuelekezwa shida zako sio kanisa fulani au mchungaji fulani bali ni Mola wako,ukienda kanisa fulani kwa imani kwamba mchungaji fulani atakusaidia unafeli,yani hapo unampa huyo mchungaji uungu,ndio maana umekiri umeingia makanisa yote

Kwahiyo endelea kuomba bila kuchoka na amiini shida zako zitatatuliwa na Mola wako basi,hakuna mganga wala jini,wanasema ukiona bado hujafanikiwa basi jua muda wa kuomba bado haujaisha

Kuhusu kazi,usiombe kazi ukiwa na master yako,omba ukiwa na vyeti vyako vya chini halafu piga kazi utabadilikia humo humo ndani ya kazi,waajiri wengi wanaogopa level hizo wanajua pay ni kubwa,lakini ukisha onyesha uwezo wako na thamani yako ikaonekana basi hapo utaweza kunegotiate

Nasisitiza aliyoruhusu mitihani hiyo ni Mungu na yeye pekee wa kuiondoa,omba kwa imani na kuwa mwema kwa tabia na matendo,Msaada wa Mungu upo karibu sana kwa wachamungu

Asante
 
Kuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.

Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.

Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.

Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.

Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.

Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.

Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.

Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.

Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?

Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?

Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?

Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?

Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.
Sema wanao muomba shetani siyo Mungu.
 
"Mimi Mtakatifu" Huitaji Kumuomba Mungu Kwa Cheo Cha Utakatifu Ulionao Wewe Subiri Maagizo Kutoka Kwa Mungu Ni Lipi Atakuagiza Ili Kuwatendea Waja Wake...Sawa..!!!### Mimi Mtakatifu###
 
Pole Mkuu, matatizo ni sehemu ya maisha, kuna mwingine ana zaidi ya hayo yako. Ila tunaishi kwa Imani, sisi ni binadamu tu.

Kwanza ningekuomba ukae upande unaoona amani moyoni mwako. Mimi nitaongelea kwa Mungu, ukiamua kuwa kwake, omba toba kwa yote maovu unayoyajua na usiyoyajua.

Kaa upande huo, usitoke hata mambo yawe magumu kiasi gani. Ni mitihani utaivuka. Usisahau kuogea chumvi ya mawe. Haina shida, Mwenyezi Mungu akutangulie.
 
Back
Top Bottom