Mnaoomba Mungu na anawasikiliza uwa mnatumia mbinu gani?

Unajiuliza Mungu unamkosea wapi, wakat unashinda kwa waganga, huwezi ukamuomba mtu asiyekuwa na mahusiano naye, tengeneza mahusiano yako na Mungu unayemuomba, sio unaomba huku unaendelea kuhangaika kwa namna nyingine huwezi kusaidia sasa sisi wengine tulifanikiwa kwenye kuomba baada ya kutengeneza mahusiano na Mungu, kibinadamu tu wanasema tengeneza connection sasabunashindwaje kutengeneza hiyo connection kwa Mungu?
Hata kwa mganga nilikuwa namuomba Mungu manuizi yote nilielekezwa nimuombe Mungu... sehemu pekee niliyoambiwa niombe mababu sikutumia zile dawa nilizochoma.
 
Mkuu cha kwanza fanya kuibadili kwanza akili yako, kila kitu huanzia katika mind.....ondoa hizo negativity, kwamba una gundu, haukubaliki n.k n.k iambie tu akili hizo ni nyakati ngumu zitapita.

Angalia na mema pia na ushukuru, u mzima hata unapata nafsi ya kuandika hapa, kuna mwingine yupo hospital hana hata uhakika wa kuiona kesho....kwanini usishukuru??

DR HAYA LAND psychological support inahitajika
Hii mindset imekuja automatically sababu kwa nini ni mimi tu ndio sipati?

MBona kuna watu ni wabaya sana hawajui ibada wala hawathamini utu lakini Mungu anawabariki? Mimi nimemkosea nini mpaka aniache niteseke miaka yote hiyo?
 
Kuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.

Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.

Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.

Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.

Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.

Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.

Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.

Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.

Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?

Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?

Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?

Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?

Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.
Omba Yesu Kristo akutumie Roho Mtakatifu,akujaze Hekima na ufahamu mengine utaona yanajiset yenyewe.
 
Me nakushauri fanya kazi kwa bidii hayo mengine unacheza tu nakupotezamda kinachokufanya uwe ivo huna hela
 
Mungu hayupo na hajawahi kuwepo , wapo wasio omba kabisa wala kuamini Mungu ili icho unachoomba wewe wanacho mara elfu kumi.
Unaweza kuwa unaishi laana za mababu au baraka za mababu
Yani mambo yanaweza kuwa bora bila juhudi zozote au kuwa mabaya pamoja na juhudi nyingi
Mungu yupo mkuu kwa uhakika kabisa me naweza kutoa ushuhuda wa mambo kadhaa yaliyowahi kunitokea
 
Me nakushauri fanya kazi kwa bidii hayo mengine unacheza tu nakupotezamda kinachokufanya uwe ivo huna hela
Nafanya kazi ngumu sana.

Naifanya kwa bidiii kubwa kwa sababu ndio tegemeo langu.

Ila bado naangaika na maisha ni magumu.

Wakati huo Mungu ananitazama anionei huruma mpaka najiuliza mimi nilimkosea nini?
 
Unaweza kuwa unaishi laana za mababu au baraka za mababu
Yani mambo yanaweza kuwa bora bila juhudi zozote au kuwa mabaya pamoja na juhudi nyingi
Mungu yupo mkuu kwa uhakika kabisa me naweza kutoa ushuhuda wa mambo kadhaa yaliyowahi kunitokea
At least wewe kuna kitu unakiona nje ya yale tumekalilishwa.

Hizo laana sasa nani wa kuzitoa maana kama makanisani na mashekhe wamezishindwa inaamana Mungu nae kazishindwa?
 
Makanisa na Mashekh haviwezi kufua dafu suala ni wewe na Mungu
Katika kuomba
Ukiwa na nia ya kweli basi Mungu anakujibu mapema tu
Kuna Miungu na kuna Mungu wa kweli kwa hiyo unapoomba lazima umidentify Mungu unayemuomba pia maombi kama hayo yaendane na sadaka, sadaka siyo kitu cha ziada kwako bali toa kitu muhimu kwako
Mfano labda mimi ni boda boda leo nimepata elfu 40 naweza kutoa elfu 30 sadaka nikiambatanisha na maombi siku hiyo
Siyo lazima utoe kanisani
Kwa sababu makanisa ya siku hizi yamechangia sana watu kupoteza imani angalau kwa waislamu unaweza kutoa msikitini japo siyo lazima
 
Kuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.

Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.

Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.

Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.

Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.

Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.

Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.

Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.

Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?

Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?

Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?

Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?

Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.
Pole sana
 
pole kwa yanayokusibu.Ila pengine anza kwa kushukuru kwanza,mpaka unaposti hapa ni bila shaka una smart phone,na pengine hujakosa walau kula chakula cha mchana,elewa maana ya kushukuru na uache kujiona huna bahati.Jifunze kila siku kushukuru hata kwa huo uhai tu ,sio wote wanao,wako vilema,wako na matatizo zaidi yako.
Anza kiroho mambo yatakwenda tu.

Weka mipango sawa sawa,na uitimize kama ulivyopanga na utafanikiwa.Changamoto ni sehemu ya kukua na zinahitajika katika maisha yetu bila changamoto huwezi kuendelea ,usizikimbie bali zikabili.

Usione aibu kujaribu vitu vipya na vigumu,wasomi pia tuna shida ya kuchangua biashara.Mfano unaweza jifunza ufundi flani labda useremala,udereva,kilimo,ufugaji,ujenzi,kushona,kuimba katika kutafuta kipaji chako tofauti na ulivyosoma.

Kaa na watu waliofanikiwa ,na ambao unatamani kuwa kama wao,utajifunza kutoka kwao kwa urahisi na safari yako haitakua ngumu.

Weka plan yako na uifuate.Hapa ndio huwa kuna shida.Plan lazima uiandike na uwe unaiangalia kila siku kila saa.
 
Nineshafanya hii ila Mungu hajawai nisikiliza.
Inawezekana namna unavyoomba neno la Mungu limesema kwenye kitabu cha Yakobo 4:3 Hata mwaomba hampati kwa sababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa tamaa zenu
Ni kweli unaomba lakini je unaomba vipi? Kuomba kwa sauti kubwa au kuomba masaa mengi haimanishi ndiyo ticket ya Mungu kukusikiliza na kukujibu.

Mungu anaangalia utayari wa moyo wako je unachokiomba mdomoni na moyo wako umedhamiria hivyo? Je umeutoa moyo wako kikamilifu kwa Mungu au unamuomba kwa sababu tu unataka amalize matatizo yako halafu akishayatatua unakuwa hauna time nae? Kuna hii kanuni kwamba Ili upate vitu kwa Mungu unatakiwa ujitoe kwake fully kwamba hata akikujibu au asipokujibu bado utaendelea tu kuwa MWAMINIFU KWAKE KUWA IPO SIKU ATAJIBU(IMANI)

Jambo la pili inawezekana namna unavyoomba unaomba sana maombi ya kumlalamikia Mungu, ukisoma kitabu cha Nabii Habakuki utakutana na namna alivyokuwa anaomba kwa kumlalamikia Mungu kwamba kuna watu wanatenda maovu halafu Mungu ni kama vile hawaoni.. Alilalamika sana lakini Mungu hakujibu chochote mpaka alipojistukia kuwa analalamika akaachana na malalamiko ndipo Mungu alipomjibu kwamba kwa nini watu wanatenda uovu ila amenyamanza.

Kuna watu huwa wanadhani kuwa wanamkomoa Mungu baada ya kumlalamikia wanaona yupo kimya wanaamua kuzira eti wanaacha kumtumikia wakidhani Mungu atawabembeleza kumbe kadri unavyomtafuta na yeye ndivyo anavyokuwa karibu nae na kadri unavyojiweka mbali naye na yeye anakuwa mbali na wewe Mungu anao watu wengi sana

Kwahiyo tafakari namna unavyoomba kama ulikuwa unaomba maombi mengi ya kulalamika badili namna ya kuomba na pia kama uliwahi kumkasirikia Mungu kwa kutokukujibu omba toba na urudi kunyenyekea

Mwisho, inawezekana unaomba lakini hauhusishi neno kwenye maombi yako soma sana neno la Mungu ili likusaidie kukupa mwongozo unapoomba maana kwenye Yeremia 1:12 amesema analiangalia NENO lake apate kulitimiza. Inawezekana unavyoomba Mungu akiangalia haoni neno lake kwenye maombi yako ili alitimize
 
At least wewe kuna kitu unakiona nje ya yale tumekalilishwa.

Hizo laana sasa nani wa kuzitoa maana kama makanisani na mashekhe wamezishindwa inaamana Mungu nae kazishindwa?
Muombe Mungu toba halafu akusaidie kukuondolea uchungu ulio nao moyoni lakini pia Muombe akuunganishe na watu Sahihi na akupe neema ya kutulia katika Kanisa mmoja maana yako makanisa mengi sana lakini siyo yote yanayomuabudu Mungu wa kweli.. usipende kuingia kila kanisa na usipende kuwekewa mikono na kila mtumishi

Naona moyo wako una uchungu sana hapo ulipofikia unahitaji tu neema ya Mungu ikuvushe

Nakuombea kwa Mungu akukutanishe na watu Wake Sahihi aliowaandaa kwa ajili yako ili wakusaidie kukuvusha kiroho na kimwili.

Weka tumaini lako tu kwa Mungu usiangalie hali uliyo nayo hata kama unaona hafanyi yeye anafanya inawezekana kuna vitu vimekublock kuona vitu ambavyo Mungu anakufanyia unapaswa kujua tu hakuna aliyekuja Duniani kwa Hasara Mungu alikuwa na kusudi na kila mtu kuwepo na mpaka sasa hivi bado uko hai ujue kusudi lako bado lipo ni wewe kufanya bidii kumtafuta Mungu kwa kuomba neema yake

Mwisho usiwaze hata siku moja kuwa msaada wako utatoka kwa mtu, ni kweli Mungu hutumia watu au vitu kutuvusha mahali ila tunatakiwa kumtegemea tu yeye au kumuona yeye katika hivyo vitu hata kama ukiona ni fulani amekusaidia jua ni MUNGU amekusaidia kupitia huyo fulani kwa maana imeandikwa katika zaburi 146:3-4
3: Msiwatumainie Wakuu, wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4: Pumzi yake hutoka,huurudia udongo wake Siku hiyo mawazo yake yapotea
 
Wanaofanikiwa hawana dhambi?
Usiangalie hili kwa sababu kila mtu ana neema yake kuna mtu ana dhambi na mambo yake yanaenda na harogi hiyo ni neema ambayo Mungu alimuwekea tangu uumbaji na kuna wewe au mimi ambao tukifanya dhambi kidogo tu Mungu anatuacha ..

Kuna mwingine mambo yanaenda tu hata asipotumia nguvu na kuna mwingine lazima a force sana mambo ndiyo yaende. Tatizo linaanzia pale tunapojilinganisha na watu wengine kumbe kila mtu ana neema yake.

Mfano kwenye maandiko neema ya Mussa haikuwa sawa na Neema ya Yona. Musa baada ya kuambiwa hatoingia nchi ya ahadi tena kwa kosa alilosababishiwa na wana wa Israel haijalishi alimlilia Mungu vipi ili aingie Kaanani lakini Mungu alimkatalia tukija kwa Yona pamoja na kwamba mwanzoni alikataa kwenda ninawi mpka akatupwa bahari lakini Mungu alikuwa amemkusudia yeye kwenda huko ndiyo maana alivyoomba tu Toba Mungu akamruhusu kwenda kuhubiri ninawi
JIFUNZE KUFAHAMU MUNGU AMEKUWEKEA NEEMA GANI KABLA HAUJAWAANGALIA WENGINE
 
Kuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.

Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.

Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.

Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.

Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.

Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.

Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.

Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.

Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?

Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?

Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?

Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?

Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.
Mkuu pole sana kwa matatizo,umeelezea vizuri sana na nimekuelewa kutoka moyoni kabisa.
Unaishi mkoa gani mkuu?
Naomba unicheki pm muda wowote nina mambo ya kukushauri nishaelewa matatizo yako nina mambo mengi sana ya kukuhoji
 
Back
Top Bottom