Pole sanaKuna watu awatumii nguvu wakitaka mambo yao yanawaendea tu. Ukiuliza wanasema ni kudra za mwenyezi Mungu kwa hiyo dawa ni kumuomba Mungu bila kuchoka.
Niwapeni tu mkasa kuhusu maisha yangu. Mimi ni mtu ambaye nna uhakika nimekumbwa na mkosi au gundu. Nna miaka mingi sana najitafuta ili niweze kutoboa lakini juhudi zangu hazizai matunda. Naweza kusema maisha yangu yenye furaha tangu niwe mtu mzima najitegemea yalikuwa ni miaka mitatu tu zaidi ya hapo mpk leo hii haijawai tokea siku nikawa na furaha mimi ni huzuni, upweke majuto majonzi ndio sehemu ya maisha yangu.
Lakini nikitazama sina tofauti yoyote na wenzagu waliofanikiwa.
Kama elimu nnayo masters kabisa ila siajiriki na nikipata kibarua basi ni cha nguvu nyingi sana.
Nna umri mkubwa sana ila sina mke wala watoto. Nipo vizuri kiafya naweza kupiga mzigo na kuzalisha sina dosari. Ila wanawake tukifikia stage ya ndoa au kupata mtoto either ana-abort au hataki kupata mtoto na mimi kifupi sio sweetheart kwa wanawake hawakai karibu na mimi.
Kwa maarifa niliyonayo niliwai anzisha miradi ya biashara na kijamii ila niliishia kuunguza pesa kila kitu kikafa yani mimi wateja kwangu kilikuwa kituo cha polisi.
Magonjwa, kutokubalika, kuonewa, kutapeliwa yani hivi vyote ni sehemu ya maisha yangu. Natumia pesa na muda mwingi kujitibia maradhi ambayo mengine yashakuwa ya kuishi nayo.
Nimejaribu kufanya mengi kujinasua nitoke kwenye hii dhahma lakini sitoki na kubwa nalofanya ni kuomba Mungu kwa bidiii sana. DSM hii hakuna kanisa sijaingia.
Nishaenda kwa waganga wa aina zote wa vitabu na wamanyanga, bara, pwani mpaka pemba lakini hakuna jipya nililopata maisha yangu ni yale yale. Nilichoelezwa ni huyo ndugu yangu anaenifanyia haya ni aunt yangu lakini ni kama hawajaweza mzuia.
Naomba sana Mungu haswa sala za usiku japo kwa sasa nimesitisha baada ya kuchoka.
Mpaka uwa najiuliza huyu Mungu nakosea vipi kumuomba?
Uwa anisikii au kama ananisikia uwa namkwaza kipi kisichosameheka?
Mbona kuna watu ni wabaya sana machoni lakini wanafanikiwa au wakisota basi miaka mitatu minne mambo yanatulia. Mimi nakosea wapi mpaka kustahili haya maisha?
Mungu natakiwa nimuombe vipi au nimtolee nini ili anipumzishe na mimi kwenye msoto?
Mwenye maarifa naomba nisaidie nimekwama sana.