Mnaoomba Mungu na anawasikiliza uwa mnatumia mbinu gani?

Iko hivi mkuu
Vyanzo vingi vya matatizo yetu ambayo mara nyingi tunashindwa kuyatatua ukubwani tuliyapanda nyakati tukiwa kwenye mchakato wa maisha mda mwingine utotoni huku ukubwani ni kuvuna tu
Mfano.
Labda umewahi shiriki kufukuzwa shule kwa baadhi ya wanafunzi wenzako ukacheka now unavuna ubaya
Labda uliwahi mtendea ubaya mtu kwa kumzulumu jasho lake ukacheka now unavuna
Labda ulishawahi fukuzisha watu kazi ukacheka now unavuna
So jitafakari mkuu maana kuna msemo unasema mbinguni hukumu, malipo hapahapa
Jitafakari kabla ya kusema unamkosi labda ndio mda wako wa kuvuna yale uliyopanda
 
Sio rahisi mtu kukuelewa mpaka awe amepita hapo. Na usipoangalia utajikuta unazeeka ukiwa hivyo hivyo.
U Fortunately sina suggestion yeyote ya kukupa lakini Uzuri umeshajua chanzo cha matatizo so ni rahisi kushughulikia.
 
Tatizo unataka kote, kwa Yesu na kwa shetani, mara uombe kanisani mara uende Pemba kwa maushetani na majini yao.
Amua moja na ukomae nayo.
Huko Pemba na hayo mavitu ya Pwani hata ulifaulu ujue nafsi yako ipo siku itateseka, na ndio kitu huwa tunajaribu kuhubiria watu wa muarabu humu

Covax The Icebreaker MOTOCHINI adriz
 
MUNGU/YESU/MTUME ni UTAPELI MTUPU aka Mental SLAVERY, .... AFRICA ni bara linaloongoza kwa kusali DUNIANI lakini Ndo linaloongoza KWA NJAA, MATATIZO, MAGONJWA, VITA, UMASKINI nk.....Jiulize na jibu utapata..
 
Kwanza unamjua Mungu wa kweli na haki zake? Pili je uko umbali gani na mapenzi yake?Tatu tubu kwa kuwa wote tuna makosa mbele za Mungu.Kisha utakuwa na ujasiri kumwomba akuponye shida zako ili umtumikie.Ukiamini kwamba Mungu amkusikia amini pia kuwa atayatimiza.Usiulize lini bali amini tu.(soma mapitio yaliyompata Ayubu)
 
YOHANA 12:49

Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe,ila Baba aliyenituma,
Ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini,

Hivi Mungu anaweza kupewa amri?
 
Niwie radhi, kwa sababu ya majukumu nimechelewa kupata nafasi yq kurudi hapa. Hata hivyo niweke sawa hivi hoja ulizozirudisha kwangu.

  1. Sijakuhukumu na sitakiwi kufanya hivyo hata kidogo maana maandiko yanazuia kabisa hilo. Iwapo imeonekana nimefanya hivyo, naomba msamaha kwako, kwa mwingine aliyetafsiri hivyo na mbee za Mwenyezi Mungu. Nilichofanya mimi ni kutoa mtazamo wa kile ninachodhani ni chanzo cha tatizo.
  2. Kuhusu Hoja ya kuongea na Mungu, kwa unyenyekevu na kuomba msamaha. Hapa unatakiwa uweke mazingira ya Mungu kusikia na kukusikiliza pale unapozungumza. Kumbuka, kuomba ni suala moja, na kuomba Mungu akasikia ni suala jingine, na kuomba Mungu akasikia na kusikiliza ni suala jingine pia. Hivyo lazima kujenga mazingira ya Mungu kuskia na Kusikiliza pale uombapo. Rejea 2 Nyakati 7:14-15, Zaburi 34:15
  3. Sasa, ukishatoka hapo tuje kwenye hoja ya kwamba Mungu hakusikilizi. Je, hakusikilizi kwenye muktadha upi? Kwamba dhambi zako hazijasamehewa au hoja ya kutopata mafanikio?
  4. Ikiwa kutosikilizwa unakomaanisha ni kwenye muktadha wa kutopata mafanikio, niruhusu tuchambue kwa kina kuhusu hili kwenye post itakayofuata, ni somo pana hivyo linahitaji utayari wako.
  5. Hoja ya kwamba nimesema waliofanikiwa ni wale walio karibu na Mungu nadhani umeilewa tofauti. Mafanikio hususan ya kiuchumi yako kwa wote, pengine walio mbali na Mungu wanayo makubwa na ni wengi zaidi (hapa pia ziko sababu zake na ni somo pana). Kwa msingi huo hii hoja isieleweke tofauti.
  6. Mwisho, narudia tena kukuomba uthibitishe kama kutosikilizwa unakosema ni kwenye masuala ya kiuchumi, ili tuongezeane uelewa.
Ubarikiwe sana (sio kiuchumi bali kiroho).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…