Mnaosukuma walemavu wa viungo kwenye baiskeli kuomba msaada, ni vyema hiyo nguvu mkaitumia kufanya kazi ili muweze kuwasaidia kwa uhakika hao walemavu

Mnaosukuma walemavu wa viungo kwenye baiskeli kuomba msaada, ni vyema hiyo nguvu mkaitumia kufanya kazi ili muweze kuwasaidia kwa uhakika hao walemavu

Hapo inategemeana na anae sukuma. Kuna mwingine unaona kabisa ni baba mtu mzima anasukuma katoto kadogo unaona kabisa huyu ni muhujumu uchumi.

Mara nyingi huwa wanapita kwenye bar muda kama huu. Anaomba 500 huku umeweka serengeti mezani na nyama kwa aibu inabidi utoe tu
Kha!kha!kha!,eti ni uhujumu uchumi.
 
dahh hatari sana. mwisho wa siku ukiwanyima uonekane mchoyo tu siyo kwamba hauna hela maana huwezi kuagiza msosi na kinywaji vinafika gharama ya elfu 10 alafu ukose buku ya kuwapa[emoji3]
😂😂😂😂😂 na hiyo ndio exact logic ya kuja pale unapokuwa umewekewa msosi mezani, mantiki ndio hiyo haswa, wanaijua saikolojia vizuri, ili kuepuka kuaibika basi unakuwa compeled kutoa tu
 
Wale wanaowasukuma wanalipwa na huyo anaesukumwa kwa hio wapo kazini wote.
 
Miaka ya 2000 nilikuwa napiga kazi uparen huko Usangi ....akaja ombaomba mmoja wale wa kubuluz miguu.....pale ofisini watu wakamchangia kama 40K ......akasepa ....mida so mida bosii akatuchukua Mimi na mshikaji wangu mmoja tuende naye Moshi ishu ya kazi...... kushuka tu Mwanga pale kwenye kona inapokutana na barabara ya lami inayotokea DSM kina bar fulani hivi ......sikumbuki jina lake ....tulimkuta jyule ombaomba kafunga baa ..anapiga maji na kelele nyingi

Bosii ndio wa kwanza kumuona akamfata na kumwambia unanikumbuka jamaa akasema ndio ......akamwambia sisi watatu pale tulikupa 15K hivyo bili yetu itakuwa juu yako na chenchi akarudisha.........kama 5K
 
Kuna mmoja namuonaga pale kituo cha mwendokasi kimara mwisho amekaa kwenye kiti cha walemavu anaomba..cha kushangaza anamiliki smartphone mpya...huwa anavizia kama hakuna wapita njia anaitoa anakuwa anaperuzi, akiona mpita njia anaificha..me nilimuotea jana,nikabaki kushangaa tu.
 
Huyo Naibu Waziri Kama kweli anapenda hao walemavu wapate haki zao asiishie kuchapa hao wasukumaji, apambane kuweka Sheria ya watoto walemavu kujengewa shule za boarding Kila wilaya zitakazotambulika kwaajili ya watoto walemavu peke yao, wakae huko wasome na hizo shule ziruhusiwe kukusanya sadaka kwa wanaojisikia kusaidia hao watoto, likizo wawe wanaruhusiwa kujumuika na jamaa zao, Sasa hapo wakiwa watu wazima yaani badala ya miaka 18 wao waongezewe iwe 25 kutambuliwa utu uzima, Sasa kuanzia 26 mlemavu huyo asiruhusiwe kutembea kuombaomba mtaani iwe ni kosa kisheria atumie taaluma yake kujiingizia kipato, na umri wa chini huo wawe shule maalumu pia iwe Sheria na lazima na misaada na sadaka zipelekwe huko kwenye shule zao.
 
Kuna mmoja namuonaga pale kituo cha mwendokasi kimara mwisho amekaa kwenye kiti cha walemavu anaomba..cha kushangaza anamiliki smartphone mpya...huwa anavizia kama hakuna wapita njia anaitoa anakuwa anaperuzi, akiona mpita njia anaificha..me nilimuotea jana,nikabaki kushangaa tu.
We toa pesa yupo kazini...hiyo ni Kazi Kama Kazi nyingne , matumiz ni juu yake ata akinywa bia au kununua malaya
 
Back
Top Bottom