Mnaotaka kuingiza bidhaa nchini kokotoo la TRA ndio hili

Mnaotaka kuingiza bidhaa nchini kokotoo la TRA ndio hili

We Jamaa unachekesha sana unasema VAT hain impact kwa mfanyabiashara?

Kama haina impact kwa wafanyabiashara kwa nini wanakuwa wagumu kutoa risiti au wanatoa risiti ya bei Pungufu ili kupunguza makali ya VAT?

Mfanyabiashara akikuzia bidhaa yenye thamani ya milioni 100 si anatakiwa ilipe VAT tena cash ya Milioni 18

Hizi elimu zenu za katika makaratasi ni ujinga mtupu
Huyu anazungumzia mambo ya uhasibu wa vyuoni, Hali halisi ya mtaani Ni tofaut kabisa.VAT inaumiza mno.

Kiuhalisia wanasema inapaswa kulipwa na mnunuaji wa MWISHO, maana ake muuzaji unapaswa umpandishie Bei mteja kufidia pesa ya vat uliyoilipa serikalini uko tra

Sasa ukipandisha bei Wewe TU,
Wenzako hawana hiyo vat kibiashara utoboi

VAT awamu iliyopita ilikua inatumika kuwanyoosha wale wapinzani wa JIWE.

Ukionekana unamdomo Sana,
Au unawadhamini upinzani Kwenye biashara yako unapigwa vat unyooke.

NA HUNA CHA KUFANYA MAANA IKO KISHERIA
 
Ameongea kinadharia zaidi,

Yaan serikali ichukue Kodi Yao,
Afu eti sheria inakuruhusu urudi kuwadai TRA Kodi yako.

Ha ha ha...utakua ujipendi Wewe[emoji23]
Inaumiza kuona mtu anaongelea kitu bila kuwa na uzoefu! Na ni wabishi ajabu
 
tuwe wakweli jamani kodi sihuwa TRA wanasimamia tu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Ndio wanasimamia, ila kama usha wahi fanya biashara kubwa ndo utajua kero ya hawa jamaa
 
Serikali ijitahidi ifufue viwanda baadhi ya bidhaa zianze kupatikana tu hapa nchini aisee
Sasa kama nguo tu kodi namna hio si balaa yaani hata kuvaa nguo iwe anasa 😃
Tatizo ni gharama za uzalishaji (hasa umeme) ambazo zinafanya bidhaa iliyotengenezwa hapa kuwa ghali. Idea ya JPM ilikuwa ni kupata umeme (ambao hauna ufisadi) kwa bei nafuu ili kupunguza gharama za uzalishaji. Ila sasa naona gharama za zinapaa huko Bwawa la Nyerere kiasi mwisho wa siku umeme utakuwa juu sana.
 
tuwe wakweli jamani kodi sihuwa TRA wanasimamia tu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Lawama tulitakiwa kuwatupia wale wanao lipwa milion 12 kwa mwezi na viyoyozi vya Milion 120.
Wao ndo walisema ndioooo bila kusoma kilicho andikwa ndani yake.
 
Kwenye tembea tembea zangu mitandaoni nimekutana na kikotozi cha TRA kinachotumiwa kwenye uingizaji wa bidhaa hapa nchini, kwakweli kinatia kichefuchefu na kukatisha tamaa.

Jioneeni wenyewe nisiseme sanaa;

View attachment 2474370
Unaambiwa, 'thamani ya bidhaa kiforodha'.
Maana yake ni bei za ajabu ajabu wanazoamua wao tra, zisizo na uhalisi wala ukaribu wa bei uliyonunua (mara zote ni juu/ aghali kuliko) wewe mhusika hiyo bidhaa.
Mfumo wa kukomoana, kufilisiwa, ati nchi inafunguliwa!!
 
Mzee baba, wewe itakuwa ndio hujui unalozungumzia, aliyekwambia VAT analipa mfanyabiashara ni nani??
Hapa ndipo ilipo shida ya elimu yetu ya Tanzania
Wewe unaizungumzia VAT kupitia ulichokisoma darasani na Mimi naizungumzia VAT katika hali halisi ya sokoni na sokoni ndiko unakutana na impact ya VAT kwa wafanyabiashara

Hivi wewe umeshawahi kukutana na mteja wa mwisho anayenunua kiatu dukani Cha kuvaa analalamika kuhusu VAT ?
Na kwa mujibu wa topic zinazofundishwa darasani huyu mteja ndio mlipaji wa hiyo VAT

Kwa upande wapili kwa nini wanaolalamika kuhusu VAT inawaumiza ni wafanyabiashara na sio wateja wa mwisho?

Na je vipi huyu mfanyabiashara ambae ambae ameingiza mzigo sokoni na akakuta labda fashion ya mzigo wake imeisha hivyo itamlazimu auze kwa bei ya hesara ili kuokoa msingi wake lakini pia katika hayo mauzo VAT inamsubiri aikusanye na kupeleka cash TRA
 
Mimi nikiangaliaga tu ushuru wa gari tena lililotumika nabaki kushangaa tu sijui tunaishi dunia ipi? Kuna kipindi tulikuwa nje ya nchi tukifanya kazi na mrundi alìkua akishangaa sana akisikia ushuru wa gari kwetu. Akituambia kwao kuingiza gari si issue kabisa...gharama ni kuinunua na kusafirisha tu lakini kuitoa wala alikuwa hawazii tax(Burundi)
Sasa napata hoja ya waTz kushauriwa tuhamie Burundi!!
 
Kwenye tembea tembea zangu mitandaoni nimekutana na kikotozi cha TRA kinachotumiwa kwenye uingizaji wa bidhaa hapa nchini, kwakweli kinatia kichefuchefu na kukatisha tamaa.

Jioneeni wenyewe nisiseme sanaa;

View attachment 2474370
Ushuru wa forodha, ushuru wa bidhaa na VAT kwa bidhaa ile ile kuna maana gani kimantiki?
 
Haya makampuni ya simu makubwa yaliweza kusimama kwa sababu kulikuwa na ile Sheria ya Exemption ya kusamehewa Kodi kwa miaka 5 Ila hi kampuni ya mwisho hiyo Sheria hawakuikuta ona jinsi inavyo inavyoyumba mda wowote wanaweza kufunga biashara na kurudi kwao

Believe me wasomi wa nchi hii wameshindwa kabisa kufanya Kodi kuwa rafiki kwa wafanya biashara kwa sababu wamezoea kucopy na kupest Sheria za nje Sasa kwa Kodi ni ngumu maana mazingira hayafanani na ya hao wazungu waliowacopy
 
Serikali ijitahidi ifufue viwanda baadhi ya bidhaa zianze kupatikana tu hapa nchini aisee
Sasa kama nguo tu kodi namna hio si balaa yaani hata kuvaa nguo iwe anasa 😃
Nguo au bidhaa nyingi zinauzwa bei ndogo sana huko nje ila shida ni hao TRA chochote kwao ni dili ndio maana watu wanafata nguo Uganda zinazopita bandari yetu ujue jinsi tulivyo na Udumavu...
 
Watanzania ni Wazalendo sana kulipa kodi pamoja na kwamba TRA badala ya kuwashukuru walipa kodi wanajipongeza wao kwa kukusanya kodi...Nchi zingine kila mwaka ile VAT wanayoirudisha kwa kununua bidhaa kwao huwa wanapongeza unakutana na barua nzito wanakutafuta wao sio bongo kila mlipa kodi anaonekana jambazi muda mwingine Jeshi linahamia dukani..
 
Back
Top Bottom