Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

simu za wanawake hizo, limitations kibao kama napata bure bana
ku-share files na windows PC mpaka ni-install iTunes, si ubwege huo
Hakuna simu ya wanawake duniani, large percent of wanawake wana hold samsung na techno kuliko iphone.
So hiyo inafanya samsung simu ya wanawake?
 
Watumie wenyewe.
 
Pesa zetu za madafu hizi ni takataka tu hakuna kitu..ukiwa pale state utaona ni kitu cha kawaida..
 
Mimi kwa uelewa wangu, aliyeanzisha Apple lengo lake ni kuuza premium brands. Yaani auze vitu vyake bei juu kwa "niche" maalum ya wanaotaka vitu vya bei juu bila kujali bei na satisfaction ni sawa na anayetumia bidhaa zingine.
Ni kama kwenda kupata huduma hoteli kama The Kilimanjaro Kempinski pale. Huduma ni zile zile, kula, kulala ila bei mkasi sana.

Hilo sio tatizo, tatizo wabongo ni malimbukeni. Tunaona kutumia kitu cha Apple ndio sifa, ndio unaonekana mtu wa maana huku unapata tabu ya comfortability ya kutumia. Kutumia apple ni mateso kibongo bongo ambapo hakuna umeme wa uhakika, mitandao haina data za uhakika, ni mateso....
 
Mkuu mimi nadhani haya madude yote uliyotaja utayahitaji kama spare parts ila sio kama component ya bidhaa uliyonunua. Kama sivyo, basi hawa jamaa wa Apple ni wapigaji wakubwa.
 
M.kuu umeongea ukweli tupu. Ulimbukeni nao ni tatizo. Unakuta mtu anaenda Kempsik kununua soda kwa Tsh 10,000 wakati soda hiyo hiyo anaweza kuipata dukani kwa Mangi kwa Tsh 500 tu!

Kuna wakati unakuta mtu ananunua, kwa mfano, viatu vya bei mbaya lakini ukiangalia maviatu yenyewe hayatofautiani na yale wanayovaa wadudu wa Arusha....yaani hayana shape hata kidogo. Lakini kisa tu kayanunua kwa bei mbaya basi anapita nayo mitaani huku akijiona mjanja. Hii ndio shida ya wabongo.....ulimbukeni.
 
Hata wewe nitakukatalia mkuu.
Jobs au Apple kwa ujumla wakati wanatoa bidhaa wanasema jambo la kwanza lilikuwa kumpa mtu kilicho bora sio chochote kitu.
Lazima ukifanye kitu kiwe bora kimwonekano halafu kiutendaji pia,ndipo utaweza kuchukua hela ya mtu kirahisi.

Kwa nchi kama marekani bidhaa za apple wala si katika kundi la bidhaa luxury kabisa,ni bidhaa za msingi tu ila zenye ubora wa haki,saa zao ni smart lakini hata wakimbiaji hawazifanyi kama kipaumbele ktk manunuzi.

Kimsingi uchumi wetu wa daraja la 3,unatupelekesha sana,mpaka mwenye gari bongo ni mzozo,wakati wenzentu gari ni kama kuwa na feni kwa ajili ya joto.
 
Sijui kama umenielewa kwenye paragraph yangu ya mwisho. Apple haikuundwa kwa ajili ya soko la Africa, soko la dunia ya 3, soko la makapuku. Marekani Apple ni kitu cha kawaida, ila kibongo bongo ni mateso. Iphone huwezi kusikiliza radio bila kuwa na data.....haya niambie unataka kusikiliza radioa masaa 2 utatumia mbs ngapi? Mara ka notification ka voda umetumia 75% ya kifurushi chako.
 
Upuuzi tu, eti security......una nini wewe cha kuficha namna hiyo?
Unamuuliza wewe ni PEP? Hapana.....hauna cha maana unachoficha.
 
mimi sijasema watu wote wanataka iphone, lakini ni huyo anaepiga kelele kuhusu wanaotumia iphone wanapgiwa bei mbaya. Kila mtu ana uhuru wa kupenda apendacho na ndiyo maana kunakuwa na versions nyingi za kitu kimoja.
 
Ni kweli kabisa,huwezi zingatia watu ambao bei ya bidhaa yako ni pato la mtu mmoja kwa mwaka mzima,ndio maana walionunua iphone kwao ni kama wamefanikiwa .

Tena bado tunapewa feva nyingi tu,maisha ya kibepari sisi bado tunayaishi nusu,wakisema wasimamie kucha kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake,itakuwa balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…