Mnapofanya Maendeleo msisahau kushirikisha ndugu zenu hata Kama mna ugomvi

Mnapofanya Maendeleo msisahau kushirikisha ndugu zenu hata Kama mna ugomvi

Wakuu Habari zenu.
Kuna jirani yangu huu mwaka wa 12 haonekani na namba yake ikawa haipatikani mpaka Sasa ukipiga amepewa mtu mwingine kabisa. Sijui nini kimemkuta ila Kwa asilimia kubwa atakuwa amefariki.

Kipindi nahamia kwangu, alikuwa hajaanza ujenzi na baada ya mda akaanza ujenzi wa Bangaloo lake, alikuwa na uwezo na alijenga jumba la kifahari haswa na mafundi aliotumia aliniomba nimuunganishe wale walionijengea.

Nyumba ikiwa hatua za mwisho hii ilikuwa October 2012 jamaa akapotea, simu ikawa hazipokelewi baada ya mda hapatikani kabisa, Hakuna mtu anaejua alikuwa anakaa wapi, site tulizoea kumuona akiwa mwenyewe.

Na viwanja vilikuwa Bado havijapimwa kipindi hicho, hata Ardhi hamna detail zake.

Nyumba yenye thamani ya zaidi ya Tsh 300m inapotea pasipo ndugu kujua.

Kuna mwingine ni mwanajeshi mstaafu alinunua bonge la pori Goba - Dsm kipindi Cha zamani, Hakushirikisha familia japokuwa alikuwa na mke na watoto wakubwa sana.

Alimuachia mamlaka yote ya uangalizi wa eneo balozi wa ule mtaa, Mwaka Juzi alianza kuuza lile eneo lake baada ya kulipima, Kipindi hicho alikuwa anaumwa Yuko Nairobi, mimi nilipelekwa na Dalali nikiwa natafuta kiwanja. Unapitia Kwa Balozi unaongea akiwa Nairobi anakupa Account unalipa mnaandikisha na Balozi Kwa niaba yake, Yule Mzee sijui Nini kilimkuta alikuwa anauza viwanja Kwa bei ya chini sana sqm moja Kwa Goba alikuwa anauza Tsh 45,000/=

Nilinunua baadhi ya viwanja pale, na Bado ananidai 30m

Mwaka huu tumepata taarifa kafa nashindwa kuitafuta familia yake kuwaambia kwamba baba yao anaidai maana wanaweza kuanziaha mgogoro, Japo mke wake yupo na watoto wake.

Tulinunua maeneo Yale wote tulishabadilishq umiliki

Alikuwa na bonge la eneo hekari 10 zinafika, mjumbe kafaidi huku mke na watoto hawajui Chochote.

Wakuu tunapofanya maendeleo tujitahidi familia zijue hata kama Kuna ugomvi kiasi gani, basi kama sio mkeo Tafuta ndugu mnaoelewana waoneshe, Hatujui kesho yetu, Kuna Vifo vya ghafla.

Huyu Kwa asilimia kubwa atakuwa kashakufa. Nyumba nimebaki naipalilia Mimi Kwa sababu ni Jirani yangu ili isiwe sehemu ya kutumza wadudu. Raia wanajua ni yangu
Huu ni ukweli mtupu
 
Ndio maana wazungu walishajua hili mapema.

Ardhi yao walitenga maeneo ya makazi ya watu. Wakajenga nyumba nyingi tu za watu kuishi.

Ukitaka nyumba wewe una nunua tu, Au unapanga ulipe Mortgage mdogo mdogo. Ili hata ukifa na hujulikani, nyumba inabaki mali ya serikali au ya wanao na hakuna kinacho potea.

Sasa huku Afrika unakuta mtu anamiliki ardhi kimya kimya tu, Siku akifa utata na ugomvi unaanza na unakuta mwishoni Ardhi inachukuliwa na mtu ambaye hata sio mhusika wa halali.

Stahiki za wamiliki na warithi wa halali zinakuwa zishapotea hivyo.
 
Back
Top Bottom