Mnatuambia tusioe wakati nyie mmo kwenye ndoa, mnamaanisha nini?

Mnatuambia tusioe wakati nyie mmo kwenye ndoa, mnamaanisha nini?

IDD ya mwaka Jana nilikua unguja pale stendi ya saateni KARIBU na hospitali ya Lumumba yanapo paki magari ya kwenda nungwi, mara nikamuona MKE na mume wanatukanana barabarani mchana mume anaongea huku anawashirikisha watu eti muoneni HUYU watu nao KIMYA hawaingilii mambo ya NDOA za watu ilinisikitisha sana DEMU anamwambia mumewe nipige nipige kabeba mtoto mgongoni daah
Dahh hizi ndio ndoa tunazosakamwa kila siku hatuna? Hapana kwakweli.. mambo ya ndoa mnatakiwa mkazungumze mkiwa nyumbani na sio kwenye halaiki ya watu! Wanadhalilishana baadaye sijui inawaletea picha gani wakikaa wenyewe🤦🏽‍♀️
 
Nilijiuliza sana kama hadharani ni hivi je ndani hawa si wanaumizana sana, alafu jamaa shababi mwili wa misuli kademu kembamba ila kamemvaa huyo mumewe
 
Hili jambo linani umiza kichwa sana unakuta mtu anahamasisha tusiowe ilihali yeye yumo kwenye ndoa.

Mzee wa kaliua ukimsikiliza mambo yake huko Instagram, yeye na wrngine wana kandia ndoa sana, lakini inasemekana ye kaoa na ana watoto, sasa huku nikuhurumiana kupotoshana?
Wao walioa zamani wale wanawake wa kizazi kilichopita ambao walijua kujishusha
Ila hili toleo la wanawake wa sasa wajuaji wa kila kitu wasio na adhabu wala utii kwa mume hawa usijaribu kuoa kabisa kama una mpango wa kuishi maisha marefu
 
Wao wameshaona kuna tatizo hawataki na nyie muingie matatizoni..!!
Wanataka watu wazae watoto haramu, watoto wasio na baba/mama. Huo ni upotoshaji mkubwa, watu waoane waishi kwa raha na amani.

Ndoa sio lazima kwenda bomani, msikitini au kanisani. Makubaliano yenu tu!!!
 
Unapoingia kweenye ndoa uwe na moyo mgumu kwamba mke wako anaweza kulika any time kikubwa heshima IPO tu. Ujue wanandoa wanalika kweli huko
Screenshot_20260322-104321_Messages.jpg
ndani.
 
Zakuambiwa changanya na zako...kwenye utafutaji unakuta muajiliwa anashauli watu wajiajili,wafanyabiashara wengi wanasema hawapati faida ila nivile tu hawawez kukaa bule,kwenye mahusiano wengi wanapinga ndoa ila wao wapo kwenye ndoa au wanaenda uko tena wanaongeza idadi ya mahusiano
 
Wanataka watu wazae watoto haramu, watoto wasio na baba/mama. Huo ni upotoshaji mkubwa, watu waoane waishi kwa raha na amani.

Ndoa sio lazima kwenda bomani, msikitini au kanisani. Makubaliano yenu tu!!!
Hakuna mtoto asiye na baba wala mama.
Wote wamezaliwa na wazazi wao isipokuwa kuna watoto waliotelekezwa na wazazi wao.!!

Hapo kwenye makubaliano kwahiyo wewe unashauri watu waishi bila ndoa?

Naona unatengeneza mazingira ya Free P mahari isitolewe lol! 😹😹😹
 
kwamba ndoa za bila mahari sio ndoa?
 
Hakuna mtoto asiye na baba wala mama.
Wote wamezaliwa na wazazi wao isipokuwa kuna watoto waliotelekezwa na wazazi wao.!!

Hapo kwenye makubaliano kwahiyo wewe unashauri watu waishi bila ndoa?

Naona unatengeneza mazingira ya Free P mahari isitolewe lol! 😹😹😹
Kuzaa watoto kila mmoja ana mama/baba yake unaona no sawa. Mtu ana miaka 35 tu kazaa na wanaume wa kutosha. Unaona sawa eeeh, kweli kizazi cha nyoka hiki.

Maadili yanaanzia ngazi ya familia, sasa kama familia tu mnashindwa kuanzisha, hayo maadili ya kitaifa yanatoka wapi. Huyu yupo kwa baba yule, huyu umeenda ustawi maana halei mtoto, upo Njombe yeye yupo Dar kuna malezi hapo?
 
Hili jambo linaniumiza kichwa sana unakuta mtu anahamasisha tusioe ilihali yeye yumo kwenye ndoa.

Mzee wa kaliua ukimsikiliza mambo yake huko Instagram, yeye na wrngine wana kandia ndoa sana, lakini inasemekana ye kaoa na ana watoto, sasa huku nikuhurumiana kupotoshana?

Mimi sijawahi kusikia walioko kwenye Ndoa wakishauri watu wasioe/Olewa.
Hata hivyo kuoa au kuolewa ni maisha Binafsi ya mtu......... na maanisha kila mtu anauamuzi wake na wala hauhitaji kuja hapa eti ukashauriwe uoe au usioe!
 
Back
Top Bottom