Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Aina gani ya msongo
  1. Kukataliwa
  2. Kutengwa
  3. Kutosikilizwa
  4. Kudanganywa
  5. Kukopwa
  6. Kudaiwa
  7. Kudhihakiwa
  8. Masomo
  9. Makazi duni
  10. Kelele za majirani
 
Na umri pia nakumbuka wakati wa adolescence nilipatwa na hali kama yako tena ya kwangu ilikuwa mbaya sana mpaka huwa nashangaa nilipita vp wakat ule.,
All in all kuna trigger ya hyo em chungza vzur mkuu..
pole lakini.
 
Pole sana best,naelewa sana ulicho pitia..wasio pitia hawawezi kuelewa unacho kielezea. Nmejifunza nitailinda Afya ya akili kwa gharama yoyote ile...ni vyema nikose millions of money lakini niwe na Afya njema ya Akili.
 
Nenda kwa therapist ukamueleze shida yako, atakuandikia dawa umeze kwa muda mfupi baadae utjisikia uko sawa!
Nafahamu unavojisikia[emoji22]
Mimi huwa naiita kuumwa roho
Maana concentration inakuwa hamna, kila kitu unakiona meaning less!
Kapate dawa upesi kabla haija kuwa deep depression, maana ikiendelea hiyo hali utaanza kusikia sauti za watu hapo ndipo unapoingia kwenye schizophrenia!
Pole sana!
 
Pole sana kwa ulichopitia [emoji3064][emoji3064]
 
sure sana sana iwe chronic alafu nasikia stresa inapunguza immune system kuna ukweli.?
 
Nashukuru ndugu najitahid kuswal napata relief kwa mda tatizo mawazo yakinijia najikuta napata mfadhaiko tena sio siri usiku nauogopa maana ndo mda unakuwa peke yako ninachoshukuru Mungu sijafikia stage yakukosa usingiz
Pole brohhh..Mimi tofauti nikiwa naswali nikimaliza mawazo yote yanapungua na moyo unapoa huwezi amini yaani nakua mpya kabisaa kama sio mimi
 
Asante sana ntajaribu maana hii hali huwa inaniondelea interest ya vitu vingi naweza nikasema nachek muvi ikifikia nusu natoa ntaingia social network kidogo tu ntazima data yaani nakuwa nusunusu

Anza kusoma simulizi za UMUGHAKA! utashangaa stress zinapotea!!
 
Muombe Mungu kuna muda unaweza usione wa kuongea kulingana na changamoto uliyonayo but omba sana tena ukiwa unaomba jifungie lia adi huzuni iishe
 
Pole sana best,naelewa sana ulicho pitia..wasio pitia hawawezi kuelewa unacho kielezea. Nmejifunza nitailinda Afya ya akili kwa gharama yoyote ile...ni vyema nikose millions of money lakini niwe na Afya njema ya Akili.
Asante sana, Bilgert.
Upo sahihi, afya ya akili ikiwa vibaya hata millions of money haziwezi kukufaa.
 
Tafuta mtu usiemjua nasisistiza usiemjua, umsimulie inasaidia kupunguza mawazo..... huyo mtu anaweza kuwa hata wa huku online, usijichanganye kumsimulia rafiki au jamaa watafanya habari halafu itakuzidishia stress...pole kwa unayopitia.
 
Msongo ni Kwa sababu Jambo ulilonalo halijapata ufumbuzi likipata ufumbuzi msongo unaisha.
Namna ya kutatua Jambo linalokupa msongo ni kulikabidhi Kwa Yesu Kwa njia ya maombi. Utapata ufumbuzi.

Pia tumia panadol na vitunguu saumu vya asilia na tangawizi. Ili kuifanya akili itulie. Akili inatatua Jambo vizuri ikiwa imetulia.

Ubarikiwe sana na Yesu Mungu Mkuu.
 
Hua nasomaga riwaya ni dawa kubwa sana na dawa nyingine ni kupuuza yaliyo leta stress hatakama kuna maslahi au mambo ndio yanazidi kuharibika hua naacha muda ufanye kazi mpaka mwisho kabisa ndio najua pakuanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…