Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Pekejeng

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Posts
808
Reaction score
2,155
Siku ya jana, leo na sijui hiyo kesho itakwendaje. Napitia msongo mkubwa sana wa mawazo, najaribu kujiliwaza na kujifariji pamoja na kujichanganya na watu ila nikikaa kidogo na kufikiri najikuta narudi katika huzuni na mfadhaiko wa nafsi. Sio siri nakosa raha na hamu ya vitu vingi naomba mbinu ya kujikwamua.

Kama kuna mtu alishapitia hali hii naombeni msaada. Pia mimi sio mlevi wala situmii kileo chochote.
 
Napanda 'street fighter' Civilian moja iko njema sana, hairembi, huyoo mpaka Tabata, nagonga sana Makange na smoothies za kutosha

Narudi mpaka Gomes, nasubiria 'Konde Boy' TATA, huyoo mpaka home, napiga kimoja nalala.
 
1.maisha ndo haya haya humu duniani KILA kitu kinapita.[emoji4]
2. Kutokuchukulia vitu serious sn Hasa vile vinavyohusu hisia[emoji4]
3. Kutokua kua na imani hasi kwa kila linalokupata maishani[emoji4]
 
Siku ya jana,leo na sijui hiyo kesho itakwendaje napitia msongo mkubwa sana wa mawazo najaribu kujiliwaza na kujifariji pamoja na kujichanganya na watu ila nikikaa kidogo na kufikiri najikuta na rudi katika huzuni na mfadhaiko wa nafsi sio siri nakosa raha na hamu ya vitu vingi naomba mbinu ya kujikwamua
Kama kuna mtu alishapitia hali hii naomben msaada. Pia mimi sio mlevi wala situmii kileo chochote.
Pole moja ya vitu hatari sana ni msongo wa mawazo nakushauri usitumie kilevi chochote, bange au madawa ya kulevya.
 
Siku ya jana,leo na sijui hiyo kesho itakwendaje napitia msongo mkubwa sana wa mawazo najaribu kujiliwaza na kujifariji pamoja na kujichanganya na watu ila nikikaa kidogo na kufikiri najikuta na rudi katika huzuni na mfadhaiko wa nafsi sio siri nakosa raha na hamu ya vitu vingi naomba mbinu ya kujikwamua
Kama kuna mtu alishapitia hali hii naomben msaada. Pia mimi sio mlevi wala situmii kileo chochote.
Fanya maisha yako rahisi na ondoa kutaka visivyotakikana wala kufikiri visivyofikirika. Stresses nyingi zinaletwa na usasa utokanao na ubepari na kutamani usichoweza au kuataka kupata kingi au kujipa haki hata usipostahiki.
 
Back
Top Bottom