Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

wakuu kwanza poleni....
serikali haijakaa kimya kwa kifupi two to three week from today mtaona kazi ya serikali kwa sababu kuwapiga marufuku kunatakiwa kushirikisha wizara kadhaa.

tulipongeze jeshi la polisi kwa sababu ni siku nyingi tu wamekuwa wakitaka kupiga marufuku biashara hii haramu ya consumer fraud lakini changamoto ni mambo ya protokali za kisheria.

ushauri usijiunge, kama ndugu yako au rafiki yako yupo huko auze bidhaa fasta vinginevyo itakula kwake muda si mrefu

Good..cant wait for a swift action ..kamaya erolink..umesema kama wiki tatu sio..watu wangi wameumia sana
 
Biashara inahitaji kupambana nawajua wadau wa 4ever living wanapiga hela sana kuna m1 ana nyumba ya ghorofa na anapush ndinga ya 0 km biashara nzuri hii ukijituma! iendelee.

Sound zenu zinakuwaga hivi hivi.
 
Kuna siku huyo dogo anayenshawishi,nikamkuta amemweka kati mshua anampga lecture huku akitafuta namba ya bi.mkubwa.

Nikawaambia huko watalia kila siku,hawajaenda tena,na anaendlea kusumbua daily.

DOGO hadi soli zimetoboka halafu anauwaza U_MENGI
 
Du! Umechukia kweli!!!!
Kuna DECI ambayo imekuwepo humu nchini mda mrefu tu (Forever Living Products).., ipo disguised as a Multi level marketing sijui nini.., eti una nunua dawa kwa shillingi laki saba then unaenda kuziuza sijui.., alafu eti ukimshawishi mwenzako kwenda kukunua hayo madawa eti ile pesa yake mnagawana.., yaan dawa ambazo kiu halisia zina-gharimu elfu 20 we una-nunua kwa laki saba..!!!, then huyo unae-mleta na yeye akiweza kupata maboya wenzake wa kwenda kununua basi ile pesa yao mnagawana nyie up-liners wale and the pyramid goes on and on..! huu si wizi wa ki-mbwa kabisa..! kwanini hawapigwi mnyororo hawa.., kwanza hata sijui kama wana-mashine za EFD hawa..!!!

View attachment 163809
 
Aisee. Hii kitu ya ma Forever Living et al, nilidhani naiona mwenyewe kama ni style ya DECI. Lakini kila niki google sikuwa napata taarifa zao hawa jamaa wenye hizi style za marketing. Nadhani dunia imekaa kimya.
 
Lakini hamjatuambia kuhusu ubora wa product zao maana wengine sisi uwa tunazinunua tu kwa matumizi yetu tukiamini ni bidhaa bora kabisa.
 
ndugu hujui kabisa hawa forever living wanavyofanya kazi na unawahukumu wakati hata hujui wanachofanya. hayo unayoyasema hapo juu hamna hata moja la ukweli. hawa wanauza products, sio kama deci au telexfree hawana chochote wanachouza.
Mkuu ama HUJALIZWA au wewe ndo MLIZA WATU na huo wizi wenu wa kutuonesha mipicha ya maghorofa ya ulaya na kudanganya ni ya baadhi yenu
 
wakuu kwanza poleni....
serikali haijakaa kimya kwa kifupi two to three week from today mtaona kazi ya serikali kwa sababu kuwapiga marufuku kunatakiwa kushirikisha wizara kadhaa.

tulipongeze jeshi la polisi kwa sababu ni siku nyingi tu wamekuwa wakitaka kupiga marufuku biashara hii haramu ya consumer fraud lakini changamoto ni mambo ya protokali za kisheria.

ushauri usijiunge, kama ndugu yako au rafiki yako yupo huko auze bidhaa fasta vinginevyo itakula kwake muda si mrefu
Mkuu umesema wiki tatu sio.., mi naanza kuzihesabu kuanzia sasa..! TUNASUBIRI UTEKELEZAJI
 
Products zao nyingi ni food suplements concentrate. Ni za kweli ila njia yao ya kumarket ndio inafanya watu kuwa wajinga. Sio lazkma uache kazi ufanye marketing. Huo ni uongo.
 
Mi nilishawahi hudhurua mafunzo yao wakawa wananionesha eti watu waliofanikiwa kupitia hiyo biashara..alf cha ajabu wananionesha wazungu ndo wamefanikiwa...ukimuuliza wewe je tangu umeanza umefanikiwa lipi? anakuonesha sijui nilishawahi kupelekwa dubai,sijui South Africa ..nikaona wezi tu....
 
Nilishawahi kufanya, nilinunua mzigo wa 320,000 by then.

Kazi ilikuwa ngumu balaa, nikakomaa na huyo supervisor wangu aniuzie mzigo hadi nikaisha.

Baada ya kuisha nilikimbia kama sina akili nzuri na hivyo vibonus vyao nikawaachia
 
Aisee.....
 
Mi nilishawahi hudhurua mafunzo yao wakawa wananionesha eti watu waliofanikiwa kupitia hiyo biashara..alf cha ajabu wananionesha wazungu ndo wamefanikiwa...ukimuuliza wewe je tangu umeanza umefanikiwa lipi? anakuonesha sijui nilishawahi kupelekwa dubai,sijui South Africa ..nikaona wezi tu....

Me kalikuja kadada kamoja karembo ofisini kwangu kakanieleza blah blah zake nikawa nakatazama tu mara kaniambie ntavuna laki 6 per month...mara tiketi kwenda Nairobi sijui South Africa n.k....nikaona haka kana njaa tena ile ya somalia na labda kananichukulia poa. Kwa vile me mwenyewe ni kiwembe ile 'mbaya' na gegedo lilishaanza kudisa nikapanga nimle papuchi kabisa.
Basi nikamwambie ok nataka kujiunga nijazuga niko interested na hiyo bizinesi kumbe mwenzake nipo interested na Papuchi yake, nikamwambia kwavile kuna mtu namuwahi somewhere inabidi twende wote ili anielekeze vizuri jinsi ya kuopareti hiyo biashara. Nikamchukua mpaka kwenye ka verossa kangu (Nia ilikuwa kumuua kisaikolojikale) tukaenda mpaka hotel nikampiga lunch huku nikizungumza na jamaa yangu tuliepanga kukutana hapo. Then nikakipa hiko kibinti bizinesi kadi yangu kanitafute kesho jioni. Kesho kweli kakanitafuta as usual nikakitia ndimu kikakolea mwanaume nikala papuchi....Na mpaka sasa ni mchepuko wangu
 
ha ha ha eti njaa ya Somalia...
 
Biashara yao inaitwa network marketing.Wanakulaghai unanunua bithaa za laki 6 unaambiwa uatafute wengine wa4 nao wanunue bithaa za laki6 kila mmoja,kila wakinunua wewe unapata kamisheni.

Wana dawa za meno,za presha na dawa za kuongeza nguvu za kiume,kama una famasi au supermaket unaambiwa usiziweke over counter WHY?
 
Nijuavo mimi dawa au vipodozi au vyakula vitokavo nje ya nchi wazima zisajiliwe na TFDA je hawa living forever,gnld,tiash na wengine wa jamii hii wamesajiliwa na tfda na kama bado kwa nini wasifungiwe
 
Nimekusouma kaka, next time nitajirekebisha and sinta post thread yoyote hapa JF kwa kumix Swahili and Kiingereza.

Sio kweli mkuu changanya tu na huo ndio utanzania halisi we fikilia la kwanza mpaka la saba shule za serikali wanafundisha kiswahili, form 1 mpaka chuo unajifunza lugha ya malkia. mi naona ndio unaonyesha uhalisia wako.
 
Mie wamenichosha na kuna baadhi wamenuna kisa nimegoma kujiunga nao....
Hata mimi kuna rafiki yangu wa toka utotoni sasa hataki hata kuwasiliana na mimi, kisa nimemuyeyusha kujiunga na FOREVER LIVING.

FOREVER LIVING huwa wanafanya vikao vyao pale Millenium Towers, siku moja alinishawishi nikaenda, niliyoyakuta ni kama aliyosema LIKUD. Nilishauriwa nilipe 500,000 ili kujiunga na kupewa "PRODUCTS". Nilipotoka tu sikugeuka nyuma na mpaka leo jamaa yangu akipiga simu sipokei mpaka akachoka.

Kuna siku nilimpita kituoni Mwenge akiwa na begi lake jasho linamtiririka ile mbaya, sikutaka kumpigia hata honi maana angenisumbua tu...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom