Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Duu, umenikumbusha mbali,
Enzi hizo miaka ya mwanzo ya 90, nilikuwa na rafiki wa karibu, mtangazaji RTD, alinihadithia mambo mengi.
Siku hizo mshahara wa Mtangazaji RTD akianza kazi ilikuwa ni Shilingi,
3,660.65.
Kikombe cha chai ya maziwa canteen yao pale Pugu Rd. ilikuwa Sh. 20, chapati, 20, andazi 10, mayai mawili ya kukaanga 40. Kipande cha kuku wa kukaanga ni sh.60.

Hao mabingwa wa salamu, walikuwa kila ukisoma kadi yake, kuna mahali unapita, anakupiga na Sh. 100. ukimaliza kipindi cha salaam, ukishuka canteen, hiyo 100, unapata chai, chapati 2 na mayai mawili ya kukaanga, kipande cha kuku na soda juu.

Jioni ukipita maeneo fulani, sio vi offer vinafululuza, akina dada ndio usiseme, enzi hizo redio yenyewe ilikuwa moja.

Hawa mabingwa wa salamu, ndio walikuwa wakiongoza kumwaga hizo 100, wakifuatiwa na wanamuziki wanaotaka nyimbo zao zipigwe, hawa walikata fungu kubwa zaidi,

Enzi hizo, Mghanii wetu akiwa 'Mzee Athumani Khalfani' akilipwa Sh.100 kughani kipindi cha nusu saa.

Jameni watu wametoka mbali!. Wee acha tuu!.
Mungu awarehemu watangazaji wote waliotangulia, na walibakia mpaka sasa, wapewe pongezi nyingi, na hata wazuri waliochipukia na wanaoendelea kuchipukia pia pongezi, ukiondoa wale wachache wana vamia fani.

kumbe virushwa vipo tangu siku nyingi!
 
Walikuwa wananifurahisha wale akina sijui nani Mwanyika akiwa "Safarini Uingereza" yaani bila kuweka hicho kipengele cha safarini bado hainogi.. Watu walikua wabunifu.
Wengine walikuwa wanasema "akiwa masomoni nchini Marekani" wakati wapo hapa hapa bongo kilabuni wakibugia ulabu.
 
Kwa wale waliofanikiwa kuwa na radio toka miaka ya nyuma nadhani haya majina si mageni masikioni pao...miaka ile ukisikiliza radio tanzania kwa siku nzima wakati tofaut tofaut ilikuwa nadra sana usisikie jina moja au karibia yote yakitamkwa kkatika vipindi vya salamu...najiuliza wako wapi kwa sasa watu kama akina
1.bokoman mwana mkongoman
2.tewa s. tewa
3.father nagumo fanani comoro
4.nyembo juma nyembo
5.kunguru mwoga
kwa hisani ya Tiger
6. Mbago Mohamed Mbago
7.Issa Hasan Majeshi a.k.a kamanda wa salamu.
8.Haji Mkitopaje
9.Kajole wa Kajole
10.Hawa Kirongo a.k.a super white.
11.Dr. Maulidi Msele
12.Kangomba H. Kangomba
kwa hisani ya MANI
13.Baba Dulla wa Ngamiani Tanga
14.Bi. Ngariba Jongo,wataalamu wakuuza Ming'oko toka Mahuta shimoni
nigepata hata number zao za simu ningependa kuwasiliana nao maana walifanya salamu ziwe na raha yake kutumiana redioni.
 
Kwa wale waliofanikiwa kuwa na radio toka miaka ya nyuma nadhani haya majina si mageni masikioni pao...miaka ile ukisikiliza radio tanzania kwa siku nzima wakati tofaut tofaut ilikuwa nadra sana usisikie jina moja au karibia yote yakitamkwa kkatika vipindi vya salamu...najiuliza wako wapi kwa sasa watu kama akina
1.bokoman mwana mkongoman
2.tewa s. tewa
3.father nagumo fanani comoro
4.nyembo juma nyembo
5.kunguru mwoga

nigepata hata number zao za simu ningependa kuwasiliana nao maana walifanya salamu ziwe na raha yake kutumiana redioni.

Wapi,
1)Hawa Kirongo a.k.a super white.
2)Dr. Maulidi Msele
3)Kangomba H. Kangomba
 
Kuna wale wanapiga simu halafu wanaongea harakaharaka kutoa salamu kwa watu wengi...mkali wao chesco MZEE wa matunda
 
Kuna wale wanapiga simu halafu wanaongea harakaharaka kutoa salamu kwa watu wengi...mkali wao chesco MZEE wa matunda

Hao unaowasema ni vijana wa dot com,mleta Uzi anawatafuta wale wa analogia kama vile wakina Mbago Mohamed Mbago na kina Issa Hasan Majeshi a.k.a kamanda wa salamu.
Upo?
 
Tiger umetisha sana naomba niongezee na majina yako tafadhar. well... nimekukubali nawe u mjini unao kitambo sana maana wale wajanja wa miaka ile ndo walikuwa wanakutana na vitu kama hivi...na vipindi vya rtd salamu kwa wagonjwa,wakati wa kazi,club raha leo show,mchana mwema n.k pia tulikuwa tunaopenda kujifunza tunasikiliza na rtd external services.... nmekukmbuka mbal sana haya hawa kangomba H. kangomba, issa hasani majeshi,mbago mohamed mbago...yaani umegusa mule mle
 
khaa...enzi hizo za Chaguo la msikilizaji, salamu za wagonjwa n.k nawakumbuka sana hao watumaji salam maarufu. kweli nami natamani nijue wapo wapi.... komeo la chuma umewaza mbali sana..( sijui ni kaka au dada) ila hongera sana naona umemgusa tiger.
 
Hao ni wa kwenu sisi tumewakuta akina mwili obale,mzee wa
naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam.
 
Last edited by a moderator:
Hao ni wa kwenu sisi tumewakuta akina mwili obale,mzee wa
naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam.

Kwi kwi kwi, you mean kina Manka Mushi?
Hata hao tunawajua bana ila enzi zetu walikuwepo kina Bi. Ngariba Jongo,wataalamu wakuuza Ming'oko toka Mahuta shimoni.
Unaijua majira salamu club wewe?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom