Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Wapo wapi hawa watu jamani? Walitamba sana kunako anga za burudani kupitia miziki ya Dansi kwa kutajwa sana, na pia hata kwenye salaam za radioni wakati huo walitisha sana..

Wapo wapi siku hizi???

cc ChescoMatunda
Kwani walikuwa wapi?
Na walitakiwa wawe wapi?
 
Mpaka nafika page ya sita sijaona aliyemtaja Mbago Mohammed Mbago, aliyenyakuwa ubingwa wa kwanza zilipoanzishwa zawadi za mshindi mwezi kwa mwezi RTD.

Kulikuwa na jamaa wanajiita mabingwa wa kulima ming'oko, mpaka leo sijui ming'oko ni nini.

Kuna dada alikuwa anaitwa aka Super White, dem old days.
 
Kulikuwa kuna Jumanne Sebarua Tingisha, Mahoo John Nguma, Zakaria Ndemfoo....

Alafu kuna wale wanaotumaga maoni BBC Swahili...unakuta eti Mtu anampa ushauri Bashar Al Assad...sasa huwa najiuliza ujumbe huwa unafikishwa kwa walengwa?
daaah sijui ni kwanini ila hii comment imenichekesha kuliko zote
 
mabingwa wa salam hao,wala haihitaji mvi kichwani kuwajua,ongezea na hawa,

Chivalavala M Chivalavala
Manka Mushi
manyota top manyota
msangi hamis
Hussen Makabureta
Chidi Chidi Chitenda
Zakaria Ndemfoo wa babati

Enzi zetu walikuwa akina Bambe Hussein Bambe na Moza Seif.

Hao mabingwa wa salaam ulikuwa huwezi kukosa kuwasikia kwenye redio na kuwasoma kwenye kurasa za salaam magazetini. Zakaria Ndemfoo nae wa kale, nnalikumbuka hilo jina.
 
[Ming'oko ni jamii flani ya chakula kimefanana zaidi na mihogo lakini Ming'oko ni miembamba na Ina ladha ya Sukari kwa mbali na imepoa Kama viazi vikuu. Wanalima Sana watu wa ikwiriri, Somanga n.k
 
Una umri gani?
Umewahi kuwasikia watu hawa?
1. Bokoman Mkongoman
2. Limonga Justin Limonga
3. Chidi chidi Chitenda
3. Wajadi Fundi
4. Mwalimu Mashaka Sabuni
5. Alafa Kapilima
6. Thomas Mushi Kimboka
Na Zakaria Ndemfoo wakiwa safarini kuelekea Mahuta Newala?
jumanne sebarua tingisha
 
Hao akina Manka Mushi na Hussein Makabuleta wamekuja kipindi hiki cha salam kwa njia ya simu...
Mi nazungumzia enzi zileee za post kadi kipindi cha Jambo, Mchana Mwema, Salam za mchana, Shambani, na pole kwa kazi...
Elenest mawaya,Suzy ngodoki,ngoswe mbeba ,
 
Habari wakuu,
zamani ilikuwa kutuma salaam redioni ni mtindo wa kijanja sana iwe kupitia Kadi au Njia ya simu ila kwa sasa naona mtindo wa Kadi haupo tena na kupitia simu kama umepitwa na wakati na hii ni kutokana na kuingia kwa mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram na Facebook.

Je wewe unawakaumbuka watuma salaamu gani..?
mimi nakumbuka wafuatao kwa redio mbalimbali
Manka Mushi
Filbert Kiyauki
Top Manyota
Lawena Nsonda
B 52
David beckham Onana
Mponeja wa Mponeja
Mwilio Bale
Mwl Kapingili
Bakari Makabali
Pido G Pido Guy
XX Mzozo
N a wengine wengi
 
Back
Top Bottom