Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Umenikumbusha mbali mpaka nimemkumbuka Catherine Chomago mtangazaji matata wa RTD aliyependa nyimbo za Vata Mombasa Juju man wa Le Orchestra Lipua lipua!
 
Huyu Chivalavala zake zilikuwa "nikiwa safarini kuelekea South, bila kusahau salamu zangu special kwa mke wangu kipenzi Ziada Napinda"
Mi nilikuwa nadhani ni South ya kwa Madiba kumbe ni south ya Mtwara.
Enzi zile sauzi ya kwa madiba mwiko kwenda. Maana mchonga na kaburu picha ilikuwa haiendi kabisaaa.
 
Baada ya kusikia taarifa za Kifo cha Gwiji la Salamu kimataifa Mzee Zakaria Ndemfoo nimewakumbuka Magwiji wenzake ambao wamepotea kabisa.Nawaomba wanaojua walipo magwiji hao tupeane taarifa zao,kama wapo waliotangulia mbele za haki tuwaombee.Binafsi kuna gwiji ninalolikumbuka anaitwa Nazareno K.Soffi wa Pawaga ,yupo jamaa mwingine alikuwa kariakoo kona ya Uhuru na msimbazi naomba tukumbushane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chesco mzee wa matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom