Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Si tuu kumsaidia, watu wamekosa ubinadamu kabisa. ..ntawapa kisa kimoja tukiwa kwenye basi moja kutokea mkoa fulani kunamtu tumbo lilimvurugukia kwa bahati mbaya yakatoka kutokana ni mtu mzima aibu, akajikaushaa watu tukahisi kuna mtu kajamba wote kimya, kufika sehemu ya kula tukashuka yule mtu hakushuka,kama kawaida kuna watu hua hawashuki. Jamaa akawa anafuta yale mavi kwa umakini mtu aaimwone, bahati mbaya kuna mama alimwona ile tumerudi kwenye gari na misosi yetu gari hapo imetembea kama 1km,watu bado wanalalamika harufu si ndo mama akafunguka huyo ndo kajinyea,watu ashushwe ashushwe kwa kua tulikua bado town akaingizwa stand akashushwa,baadae wale watu wa gari wakamuacha kwa madai wamechelewa, na jamaa alikua hajafika hata robo ya safari, binafsi nilijaribu kuwasii wenye basi wa simuache, cha kushangaza sikupata support ya hata abiria mmoja,hiyo hali inaweza mpata mtu yeyote wakati wowote. ..ukute yule jamaa alikua hana pesa ingine
mimi nasema wadau hao jamaa walikuwa wanatembeleana tu kwa kufahamiana kwa salamu,mimi namkumbuka baba dulla one.Nasikia kipindi hiko mtuma salamu anatoka tanga anakwenda kumsalimia mwenzake wa mwanza na akifika anapokelewa na anakirimiwa enzi hizo utu na ubinadamu ulikuwepo sio sasa mtu anapata ajali unamsachi kabla ya kumpa huduma.
 
Mi nawafaham RAMBO SEGEJA NG'WANASUSANA YUPO Ibindo NYAMBITI Kwimba na mmoja alikuwa ananikosha kwenye mechi za Simba na Yanga ikisomwa kuponi yake had raha alikuwa anaitwa PIUS MWANDOJE kutoka Mwandoje's mitumba mbeya anaitakia simba ushindi
 
Namkumbuka sana BS wa vipodozi wa temeke, ant flora John american lady wa magomen dar, Alfonsi yombo manyama wa air bariadi shopping center bweleli mtera, huyu aliwahi kuwa mshindi wa kutuma kadi nyingi redion zaidi ya 4000 kwa mwaka
 
Huwezi mtaja Bongoman mkongomani,mahuta wa mahuta lazima umuweke kabichi shirima ilikiwa lazima kwa siku uwasikie hata mara 10 Radio Tanzania
 
Kulikuwa na Gacha Shaban Gacha wa kariakoo sokoni , jamaa Kila kipindi anatuma salam.
 
Chivalavala S. Chivalavala........nahisi keshatajwa mahali.....
 
Kuna S. Tingisha sijui wa wapi huyu jamani.
Sebarua Tingisha. Shinyanga kama sikosei
Kung'ombe Chacha Mrema Sukari Mlili Obare....
Ugali Sokwe(Songea hiyo)

Fikiri Dalio/Dario
Uchumi Filbert .

HAWA JAMAA WA MWISHO WAPO SIKU ZOTE
 
Back
Top Bottom