Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Nami pia namkumbuka mzee wetu Sheikh Othman Matata Kawia huyu alikuwa mtaalam wa kusoma taarifa habari kwa lugha ya kiingereza, na ninafikiri pia alikuwa na ndugu ambae alikuwa BBC nafikiri huyo ndie anaemzungumzia faiza
Nimemkumbuka, yeye nadhani ni mdogo wake na Mzee Othman Matata, ni kweli anaishi Uingereza.
 
Sheikh Othman Matata ninae mfamah mimi ni yule alikuwa Chief Security Officer pale Railways na alikuwa kwenye mihadhara ya Kiislaam sana, huyo ni rafiki yake mume wangu na tunajuana sana, sijui kama ni huyo ambae alikuwa akitangaza pia External Service, kweli anaongea kiingereza kizuri sana.

Ndio yeye huyo.
Naam hujakosea ndio huyo huyo sheikh Othman matata na hata wakati ule anatangaza external service alikuwa yukoTanzania Railways Corporation, nilipata bahati ya kumtembelea miaka hiyo wakati anaishi Ohio street- Railway flats
Nakumbuka kweli alikuwa akiishi Ohio St, nyumba za Railway, nishawahi kufika kwake mara kadhaa, na hata uko alipo hamia sasa alinialika, maana kuna kazi nilimpa ya kuhariri kitabu changu, Dah! Alinipiga maswali sana, maana alitaka kuhakikisha kama kweli nilicho kiandika ni changu...Alisaidia sana kushape idea zangu. Ni wazee wachache ambao wanapenda sana kusaidia vijana kimawazo.
 
Ndio yeye huyo.Nakumbuka kweli alikuwa akiishi Ohio St, nyumba za Railway, nishawahi kufika kwake mara kadhaa, na hata uko alipo hamia sasa alinialika, maana kuna kazi nilimpa ya kuhariri kitabu changu, Dah! Alinipiga maswali sana, maana alitaka kuhakikisha kama kweli nilicho kiandika ni changu...Alisaidia sana kushape idea zangu. Ni wazee wachache ambao wanapenda sana kusaidia vijana kimawazo.
Duu m'mungu amzidishie rehma mzee wetu kwani amesaidia wengi, nathubutu kusema ni mtu makini sana hata mimi binafsi alinisaidia sana, mzee yule kingereza chake murua saaana halafu changanya na ile lafudhi yake, wanaomfahamu vyema watalithibitisha hili
 
  1. Abdallah Mlawa
  2. Nassoro Nsekeli
  3. Bujaga Kadago
  4. David Wakati
  5. Khalid Ponera
  6. Christina Chokunogela
  7. Ahmed Kipozi
  8. Siwatu Luwanda
  9. Salim Seif Nkamba
  10. Salama Mfamao
  11. Bartholomew `Bati' Kombwa
  12. Ahmed Jongo
  13. Dominic Chilambo
  14. ngalieni Mpendu
  15. Sekioni Kitojo
  16. Chisunga Steven
  17. Edda Sanga
  18. Mikidadi Mahmoud
  19. Deborah Mwenda
  20. Danstan Tido Mhando
  21. Mshindo Mkeyenge
  22. Sara Dumba
  23. Steven Makwaya. (not sure huyu kama si huyo wa namba 26).
  24. Chama Omari Matata
  25. Paul Sozigwa
  26. Steven Mlawa
  27. Kasanga Tumbo
Hapo juu sio SEKIONI KITOJO huyu anaitwa SEKIONE KITOJO nae pia ninafahamiana nae kipindi kirefu tokea anakaa magomeni miaka ile ya 80 kabla ya kwenda idhaa ya kiswahili ya ujerumani duu mmenikumbusha mbaa....li sanakuna mtangazaji mwingine pia alikuwa anaitwa mama nelly kidela (mama mkeremi)
 
Hapa MM utakuwa umetukumbusha mbali kweli Huyo WAJADI FUNDI WAJADI alikuwa nae moto kwenye salaam..dah wapo wengi kweli naona hii thread itakuwa balaaa inakumbusha mbaaali kweli wakati hakuna option ya kusikiliza radio nyingine zaidi ya RTD na external service yao!!..nakakumbuka hadi kale kamziki kao ka salamu...afu kulikuwa na kipindi maalum cha mabingwa wa salam..kadi ngapi wametuma ..afu zawadi zenyewe flana au pesa kiduchu enzi hizo

Limonga Justin Limonga
 
Hapo juu sio SEKIONI KITOJO huyu anaitwa SEKIONE KITOJO nae pia ninafahamiana nae kipindi kirefu tokea anakaa magomeni miaka ile ya 80 kabla ya kwenda idhaa ya kiswahili ya ujerumani duu mmenikumbusha mbaa....li sanakuna mtangazaji mwingine pia alikuwa anaitwa mama nelly kidela (mama mkeremi)

Mwenyewe alikuwa anapenda kujiita kwa majina yote matatu mkuu: Bujaga Izengo Kadago
 
Unawakumbuka watuma salamu wa zamani RTD kipindi cha salamu? Kuna jamaa mmoja namkumbuka Chidi Chidi Chitanda alikua hakosekani kipindi cha saa sita mchana. Taja wengine.
 
Kuna thread nzima inaongelea hii maneno.
Jaribu kuisearch!...utafurahi!
 
je yule jamaa anayejjita rais wa msasani.. muntala tala V tala vencha.. though alikuja kuibuka kpindi cha radio one
 
Wajadi Fundi wa Mahuta shimoni, newala, Ubwa K Kombo, kabichi shirima !
 
Hao wote mnawataja waliwika zaidi kipindi cha Radio One pamoja na kina
Baba Dula One,
Baba Dula Original,
Limonga J. Limonga,
N.k.
Watu walikua wanapewa nafasi ya kusalimia watu watatu,
But mtu anasalimia mpaka watu kumi kwa ile nafasi ndogo tu aliyopewa!!!
 
Back
Top Bottom