Mnawezaje kuishi na Wageni wanaochagua sana vyakula?

Mnawezaje kuishi na Wageni wanaochagua sana vyakula?

Kingine nawe mgeni ukienda kwa watu hata kama una machaguo yako,pale tuliza shobo,hujui watu maisha yao yapoje,usiwape watu uzito na ugumu na stress kwa uwepo wapo pale.

Kama ulipanga kukaa siku nyingi basi jikatae mapema kama hakuna viwango vyako vya chakula unavyo vihitaji,au kama upo fresh ingia sokoni nunua Mazaga zaga kisha bwaga pale ule kitu roho inapenda

Ila usije kuwapa watu dhiki mpaka wakajuta kwanini ulienda kwao

Alone min -me kwenye file lake pale kilabuni
 
Yani mgeni akikaribishwa chakula inabidi afanye kama anakataa kataa kwanza huku mwenyeji akizidi kushawishi alafu mwisho mgeni anakubali
Unakutana na mtu anakwambia yeye maji ya kuchemshwa hanywi anataka yasiochemshwa
Nimecheka sana aisee. Unakataa na unashawishiwa..ukikubali moja kwa moja unaonekana mlafi, na akikataa mara moja usipomshawishi unaonekana mchoyo.
 
Mgeni una vyakula vyako kwanini utembelee watu na kwenda kuwabadilishia ratiba ya Kula?, watu huishi Kwa bajeti halafu mgeni anaiharibu, kwanini usipite kusalimia siku moja Tu ukaondoka zako, suala si Kula hiki au kuacha hiki maana wengi hawali baadhi ya vitu Kwa jinsi walivyo au mazingira waliokulia, suala ni ww mgeni tena mtu mzima kulazimisha kubadilishwa Kwa ratiba za vyakula ilihali unajua hali ya uchumi ya mwenzako.
 
Nimecheka sana aisee. Unakataa na unashawishiwa..ukikubali moja kwa moja unaonekana mlafi, na akikataa mara moja usipomshawishi unaonekana mchoyo.
mkuu hiyo dhana napingana nayo kila siku, ni utamaduni wa ajabu sana
 
Jamaa wanataka watunyweshe maji ya bombani yasiyo chemshwa mkuu.
Mwenzetu unaweza kunywa?
Uliposema standards zako nikajua kama wale wanabagua maji hadi ya dukani anasema sinywi uhai nakunywa kilimanjaro tu , ama sinywi kilimanjaro nakunywa afya... mtu hadi anaangalia pH ya maji...

Ni sahihi kukataa yasiyochemshwa kama hutumii..
 
Labda ana allergy na hiko chakula na pengine kwenye maji nyumba zingine hawachemshi, labda anaogopa kuugua tumbo.. nje ya hapo ujue huyo ni mpuuzi mmoja ambae hana lolote....

Mimi ugenini mfano kijijini wali na maji ya kunywa nitakula kikubwa nisiwakwaze wenyeji wangu..

Kubagua chakula ugenini inaonyesha ni jinsi gani mtu huyo kalelewa hovyo na jinsi gani hajitambui...
Kama ana hela zake sawa.
 
Vidonda vya tumbo, mzio na umri wa mgeni utazingatiwa.

Kwamfano watoto wote wa 0-10 wa nchi hii wana mfanano wa kupenda Wali na Maharage awe ni mtoto wa spika, au wa Samia, au mwigulu au wa Bahresa wote wanaunganishwa na mapenzi yao kwa Wali maharage..
Ni nadra mno kusikia mtoto ukiusema vibaya ubwabwa.

Vyakula vingine wanakula pia kama side dish...lakini ukiwaondolea options , kwa watoto wali na maharage ndio main staple.

Lakini pia wapo watu wasiopenda chakula cha aina fulani kwasabu za kiimani, kisaikolojia au kiafya.
Mimi hapa nina mtoto asiye kula samaki mbichi, leta kitoweo chochote atakula ila sio samaki mbichi sasa
Ikiwa mgeni wako huyo hali chakula cha aina fulani badala yake akakupa cheaper options, kwanini uone shida.

Mimi sili dagaa kwa mfano, lakini naweza kutumia mboga za majani kama replacement....shida haipo.
Njoo nq bajeti yako ama kaa kwako.
 
Labda ana allergy na hiko chakula na pengine kwenye maji nyumba zingine hawachemshi, labda anaogopa kuugua tumbo.. nje ya hapo ujue huyo ni mpuuzi mmoja ambae hana lolote....

Mimi ugenini mfano kijijini wali na maji ya kunywa nitakula kikubwa nisiwakwaze wenyeji wangu..

Kubagua chakula ugenini inaonyesha ni jinsi gani mtu huyo kalelewa hovyo na jinsi gani hajitambui...
Binafsi sichagui sana vyakula lakini kuna mitindo ya mapishi inanikera.

Mfano unakuta dagaa zimejazwa mchuzi au unapewa ugali na majani tu bila mboga nyingine.

Nakwepa sana ugeni. Siku zote ugeni ni mzigo kwa mwenyeji, ni vile wabongo tuna unafki. Hata kama huchagui vyakula, kuna tabia au maneno vitamkera mtu tu.
 
Seran
Na wewe mwenyeji ukipata mgeni jiongezage.... pia walau jua abcd za alikotoka !

Mtu ametoka pwani, amekuja usukumani... unasonga bonge la ugali unampa na kopo limejaa mtindi ndo unategemea ale ashibe ? Hapo angepata japo vimboga vya majan, maziwa yawe kama kishushio tu pengine
r
 
Kingine nawe mgeni ukienda kwa watu hata kama una machaguo yako,pale tuliza shobo,hujui watu maisha yao yapoje,usiwape watu uzito na ugumu na stress kwa uwepo wapo pale.

Kama ulipanga kukaa siku nyingi basi jikatae mapema kama hakuna viwango vyako vya chakula unavyo vihitaji,au kama upo fresh ingia sokoni nunua Mazaga zaga kisha bwaga pale ule kitu roho inapenda

Ila usije kuwapa watu dhiki mpaka wakajuta kwanini ulienda kwao

Alone min -me kwenye file lake pale kilabuni
Naunga mkono hoja
 
Ila watanzania buana yaan Kuna mtu Hali dagaa? Tutoe wale wa vidonda mbona mashauzi mengi
Motivation speaker mko wengi ooh Kuna watu hawapend kula hichi ama kile eeeh as long as umezaliwa TZ vyakula tunakula vizur tu maana asilimia kubwa tumetoka kwenye familia za kawaidaaa saaaana
 
Back
Top Bottom