Bro, ndio maana ya kuwa mtu mzima, being grown up means doing what you dont want to do and not getting what you want...
Nina maana kuwa mtu mzima ni kuamka asubuhi kwenda kwenye majukumu hata kama unahisi hujisikii, kuwa mtu mzima ni kujizuia/kujinyima kupata vitu fulani tokana na malengo uliyonayo au hali uliyonayo... hata kama hiko kitu unakitaka, unataka kunywa beer na nyama choma na rafiki zako lakini familia yako nyumbani wale ugali na maharagwe... lazima ujizuie...
Kuwa mtu mzima ni kushiriki mlo na wenyeji hata kama huo mlo huupendi ili kuonyesha umoja na wenyeji, upo kijijini kuna msiba, unaletewa ugali na dagaa wanaogelea kwenye mchuzi utakataa kula? mimi nitakula...