Mnawezaje kuishi na Wageni wanaochagua sana vyakula?

Kama hawataki basi waje na bajeti yao ya fwedha
 
Bro, ndio maana ya kuwa mtu mzima, being grown up means doing what you dont want to do and not getting what you want...


Nina maana kuwa mtu mzima ni kuamka asubuhi kwenda kwenye majukumu hata kama unahisi hujisikii, kuwa mtu mzima ni kujizuia/kujinyima kupata vitu fulani tokana na malengo uliyonayo au hali uliyonayo... hata kama hiko kitu unakitaka, unataka kunywa beer na nyama choma na rafiki zako lakini familia yako nyumbani wale ugali na maharagwe... lazima ujizuie...

Kuwa mtu mzima ni kushiriki mlo na wenyeji hata kama huo mlo huupendi ili kuonyesha umoja na wenyeji, upo kijijini kuna msiba, unaletewa ugali na dagaa wanaogelea kwenye mchuzi utakataa kula? mimi nitakula...
 

Sili dagaa kauzu.
Sili makande yaliyolala.
Sili kiporo hata mandazi mikate
Siku matembele

Ulitaka nisiseme. Vizuri nimeondoka
 
Sio kweli, kuna watu hawali kila kitu , mfano mimi nyama nikila ni ya kuku tu ng'ombe au mbuzi lazima nihisi kichefuchefu , na kunde za choroko ndio sili kabisa , dagaa nile mara moja tu na nikiona yale makitu meupe au kokwa la konokono wakati wa kuchambua sigusi
 
Kumbe ni kichefuchefu nikajua inakuletea madhara mwilini ila unakula
Nilipata bint wa kazi alikua Hali nyama iwe ya kuku au ng'ombe

Dagaa Kuna safi hazina hizo konokono acha kudeka wewe
 
senene unakula?
 
Kumbe ni kichefuchefu nikajua inakuletea madhara mwilini ila unakula
Nilipata bint wa kazi alikua Hali nyama iwe ya kuku au ng'ombe

Dagaa Kuna safi hazina hizo konokono acha kudeka wewe
Sasa madhara si hicho kichefuchefu ? Bora mboga yangu iwe maharage kila siku kuliko dagaa , toka nilitafunia kokwa la konokono hazipandi kabisa ,dagaa nitawapa kuku wakue halafu niwachinje hizi dagaa nizile zikiwa ndani ya kuku.
 
Kuharibu bajeti yako ya chakula kwa uwezo ulionao ni makosa. Asiyeenda na bajeti yako aondoke, mwambie ahamie huko kwa mama ntilie...
Naunga mkono hoja ila yote kwa yote hii kula nje na ulipofikia kwa mwenyeji wako
Duh inaleta PICHA MBAYA, inafika mchana dagaa zimepikwa hapo, mgeni wako anakuaga anaend sehem ila unajua anaenda kupakia msosi nje na kwako.
Wewe na mgeni wote hamtajihisi vizuri .
 
Sili aisee. Herd mentality iliyopo bongo ni mbaya sana. Lazima kuwe na mipaka. Na ndiyo maana watu wanapata kiburi cha kukuingilia uhuru, usipooa watakutenga, usipozaa watakutenga, usipolewa watakutenga nk.
 
Sasa madhara si hicho kichefuchefu ? Bora mboga yangu iwe maharage kila siku kuliko dagaa , toka nilitafunia kokwa la konokono hazipandi kabisa ,dagaa nitawapa kuku wakue halafu niwachinje hizi dagaa nizile zikiwa ndani ya kuku.
😳😳😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…