Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Hao wanawake wanafukuzwa alafu kama hakuna kitu kilichotokea
 
Uzalendo gani huo? Kutwa kubambikiwa kesi kupigwa risasi uonevu kibao kisha useme kuna Uzalendo huko?
Kwa hiyo wewe ndio unaujua uonevu zaidi kuliko Mdee, Matiko,Bulaya na wengine?! wote hao ni wanachama halali wa chadema tena viongozi, Halima Jems Mdee ni Mwenyekiti wa umoja wa wanawake chadema Taifa sio mtu mdogo ndani ya chadema,
naamini mde kaona ukweli na kaamua kuwa mzalendo
 
Majina ya wanawake wa viti maalum huchakatwa mapema hata kabla ya uchaguzi mkuu. Hili ni swala la kisheria zaidi na mdee ni lawyer.
Mdee ni lawyer wa Mahakama ipi? Alishawahi hata kusimamia kesi ya kuku?

Hivi hujui hata Paskal Mayalla ni mwanasheria lakini siyo lawyer.?
 
Amen na iwe hivyo ukasikie sauti ya Bwana ambayo ayaambia makanisa....

Na hivyohivyo kwa watawala wetu rais Magufuli na viongozi wote wa serikali

Kwa waaminio Mungu tunakumbushwa

Warumi13

1Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.

2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu.

3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.

4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu.

5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7 Walipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mlipe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye heshima, mheshimu.

surat an nisa ayat 59
59. Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.
Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na
Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi
na ndiyo yenye mwisho mwema.
 
Unaelewa kuwa kisheria chama hakiwezi kuteua wala kupeleka jina NEC la viti maalum la mtu ambae yupo jela? Unaelewa kuwa leo kesi ya kina Nusrat imeitwa Jaji akabaki anashangaa maana hakuona watuhumiwa wala mawakili wa pande zote mbili?...
Haya mwanasheria kafungue kesi yakupinga basi
 
Haya mwanasheria kafungue kesi yakupinga basi
Yaani kesi ya Tumbili nipeleke kwa Ngedere?Hapo kuna kutolewa haki kweli?Unaelewa kuwa kwa sasa hivi mahakama imewekwa mfukoni na mtu mmoja,tena mfuko wa shati?

87659087.jpg
 
Yaani kesi ya Tumbili nipeleke kwa Ngedere?Hapo kuna kutolewa haki kweli?Unaelewa kuwa kwa sasa hivi mahakama imewekwa mfukoni na mtu mmoja,tena mfuko wa shati?View attachment 1634566
sasa kinachokuliza humu kuwa ni haki yako ni haki yako ni nini? tulia wewe ulichelewa kutambua kuwa chadema ni kampuni tena ya mtu binafsi utaumia sana huku wenyewe wanakula maisha wewe endelea kudai haki wakati unatambua kabisa haki zote zimehifaziwa.
 
Wanafukuzwa bila kujali jinsia yao kwakuwa wamejiteua wenyewe wanafukuzwa vizuri kabisa bora kuwa na chama cha watu wachache kuliko hao wanaopigania matumbo yao. Demokrasia ina Faida zaidi kuliko matumbo ya hao wachache. Wamejulikana kwa sababu ya chama hivo wao siyo wakubwa kuliko chama kuwa wataachwa wakiuke sheria na katiba ya chama
Chama kimewafaidi vya kutosha. walikuwa mirija ya kupeleka pesa kwa mbowe. Wafukuzeni sasa tuone, jinsi mtakavyozidi kuwa imara kwa uchache wenu.
 
Tunasubiri mahakama ikanushe mtu kuteuliwa na NEC akiwa gerezani.
Mimi nipo hapa nacheki hii move yenye visa vya kusisimua ikiongozwa na shujaa Mbowe.

Mr mtu makini ngoja kwanza niweke akiba ya maneno nitakutafuta baadae nadhani tutaongea lugha moja. 🤣 🤣
 
Inamaana unataka kusema kuwa wanawake wote 19 walienda kula kiapo bila hata mmoja wao kumwaga bosi wao? Dahh
Kwa Chama kinachojinasibu kua na Intel nzuri kama Chadema,na baadhi ya wabunge kuwa wake wa viongozi wa juu wa Chana bado unaamini Boss wao hakuwa na taarifa?!
Hawa jamaa sijui wanaonaje watanzania
 
Nanukuu.
Mimi nimepigiwa simu kuwa nimeteuliwa na kwamba nije kuapa.

Swali
Ikiwa chama kitawaadhibu kwa kuwafuta usnachama?

Esther
Ikiwa chama kitaona mwingine anafaa nipotayari.

Hii inaonesha mipango hii umeasisiwa na mfumo na kwa upande wa chadema mdee na bulaya wamehusika kwa kiwango kikubwa sana
Baada ya kuona mambo yamekaa dawa wengine wakaitwa tu.
Halima na bulaya wamevuta mpunga mrefu sana ili kufanikisha mpango wa watawala
 
Hivi matiko ameolewa .mwenye namba yake anitumie ,ule mguu sio wa kitoto wengine ndio ugonjwa wetu ule
 
Kwa mujibu wa tamko la Kimataifa kuhusu haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo lilibainisha msingi wa kutokubaguliwa kifungu cha (2)kinakariri
’kila binadamu ana haki sawa na uhuru bila kubaguliwa kwa misingi ya rangi utaifa jinsia lugha na itikadi za kisiasa’

Vile vile mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 unasisitiza kwamba
‘Ubaguzi dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki zao za msingi hususani haki ya kuheshimu utu wao na haki zao za msingi.’

Pia katika tamko la shirika la maendeleo kusini mwa Afrika SADC(2005) ambayo Tanzania ni mwanachama liliweka kiwango cha jinsia chini ya uwakilishi wawanawake kutoka kuwa asilimia 30%na baadae kupandisha hadi kufikia 5O%.

Kwa utangulizi huo hapo juu ni wazi kuwa jamii inapaswa kuelimishwa na kuoneshwa umuhimu wa wanawake kushiriki katika uongozi kutokana na umuhimu wa kundi hili ndani ya jamii na kupiga vita wale wote wanaotumia hila na nyadhifa zao kuwadhalilisha na kuwanyima haki zao wanawake.

Hivi sasa tatizo la udhalilishaji na rushwa ya ngono kwa wanawake kwenye vyama vya upinzani limekua kubwa kiasi cha kuwanyima fursa wanawake kushiriki katika uongozi ndani na nje ya vyama vyao. Ni wanawake wachache wanaoshiriki siasa nchini bila kukutana na vikwazo hivi kutokana na misimamo yao mikali ndani ya vyama vya upinzani.

Hii inapelekea ushiriki wa wanawake ndani ya vyama vya upinzani kuwa mdogo ukilinganisha na ushiriki wao ndani ya chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni,yapo mambo kadhaa ambayo yalifanyika ndani ya uongozi wa vyama vya upinzani yanayodhihirisha uwepo wa rushwa ya ngono na udhalilishaji mkubwa wa kundi hili muhimu la wanawake ndani ya vyama hivi.Miongoni mwa mambo haya ni kama yafuatayo:

1.Ucheleweshaji wa haki za wanachama wanawake
Baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitakiwa kwa mujibu wa sheria kupeleka majina ya wanawake viti maalumu kuwakilisha chama na wanawake bungeni.Ucheleweshaji wa haki hii kwa wanawake waliostahiki umegubikwa na udhalilishaji na viashirishi vya rushwa ya ngono kwa wanawake waliostahili kupewa nafasi hizi.Mzozo unaoendelea hivi sasa ndani ya CHADEMA ni matokeo ya msimamo mkali wa wanawake waliokataa kudhalilishwa na viongozi wachache ndani ya chama.

2.Uteuzi ndani ya Vyama vya Upinzani
Ili uweze kugombea ndani ya Chama chochote ni lazima chama kikupitishe ndipo jina lako likubalike kwa ajili ya kugombea.Uteuzi ndani ya vyama vya upinzani kwa mwaka 2020 uligubikwa na usiri mkubwa na hujuma ambazo baadhi yake zilihusiha udhalilishaji mkubwa wa wanawake na rushwa ya ngono.Haya yaliwekwa pia wazi na Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) katika ripoti yake ya vitendo vya rushwa katika uchaguzi.

3.Gharama za uchaguzi
Kutokana na mfumo dume wa kurithi wa kiafrika ambao ulimpa mali mwanaume na kumnyima mwanamke ni wazi kuwa idadi kubwa ya wanawake wanaotaka kushiriki siasa kipato chao kinakuwa kidogo.Hivyo kuhitaji msaada ndani ya vyama au familia ili kumudu uchaguzi ambao unakua na gharama kubwa.Gharama za uchaguzi ndani ya Chadema zimekua zikitolewa kwa maamuzi ya viongozi wachache ambao wamekua wakitumia nafasi zao kutekeleza matakwa yao binafsi yakiwemo ya ngono na udhalilishaji wa wanawake.

4.Vitendo vya udhalilishaji katika uchaguzi
Viongozi wa juu wa Chadema wamekua wakiwatumia wanawake kwa kuwadhalilisha ili jamii na mataifa ya nje yaone kuwa Tanzania inawadhalilisha wanawake.Mfano,tukio la kutengeneza la kura za jimbo la Kawe ambalo lilipelekea Mh Halima Mdee kudhalilika kwa kujua kura zilizoletwa na waliotengeneza tukio na kuondosheka zililetwa na mgombea wa CCM.

5.Kuwatumia wanawake kuvunja sheria
Viongozi wa juu wa Chadema wamekua wakiwatanguliza mbele wanawake katika matukio mbalilmbali ya uhalifu kuwakabili polisi na kusababisha taharuki huku wao wakiwa nyuma,hii imepelekea mara kadhaa wanawake ndani ya vyama hivi kuanguka na kuvunjika mkono kutokana na matukio ya kutengeneza ya viongozi wao.

Zipo sababu nyingi zinazothibitisha udhalilishaji na rushwa ya ngono iliyokithiri ndani ya CHADEMA na umuhimu wa serikali kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizi kwa lengo la kuwalinda wanawake na jamii ya Kitanzania kwa ujumla.
 
CHADEMA ilipitisha wanawake 68 kugombea majimboni hebu tuambie hao wanawake nani aliwadhalilisha kingono na wapi mpaka kuwapa hizo nafasi?
 
Back
Top Bottom