Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Mchakato walipigiwa kura na wajumbe.Unaujua mchakato wake?Kaa kimya kama hujui,dada zetu wanadhalilishwa
Tupe ushahidi huyo aliyemdhalilisha dada yako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchakato walipigiwa kura na wajumbe.Unaujua mchakato wake?Kaa kimya kama hujui,dada zetu wanadhalilishwa
Haki kuifadhiwa haizuii haki hiyo kuendelea kupiganiwa.Hata wakoloni waliifadhi haki za waafrika ila mwisho wa siku waliziachia.sasa kinachokuliza humu kuwa ni haki yako ni haki yako ni nini? tulia wewe ulichelewa kutambua kuwa chadema ni kampuni tena ya mtu binafsi utaumia sana huku wenyewe wanakula maisha wewe endelea kudai haki wakati unatambua kabisa haki zote zimehifaziwa.
Ndugu yangu tumia akili angalau kidogo...jifunze kupambanua mambo...usikariri tu mambo...kwa mawazo yako serikali imefoji...hivi Mdee na wenzake wanaweza kukubali serikali ifoji halafu wao waapishwe?Kweli wazazi waliuza ng'ombe ili wapeleke ng'ombe Shule. Hivi wewe huoni kinyaa serikali nzima inashiriki uhalifu wa kugusbi nyaraka na kudanganya umma?
Yote haya juu ya nini?
Kwa mujibu wa tamko la Kimataifa kuhusu haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo lilibainisha msingi wa kutokubaguliwa kifungu cha (2)kinakariri
’kila binadamu ana haki sawa na uhuru bila kubaguliwa kwa misingi ya rangi utaifa jinsia lugha na itikadi za kisiasa’
Vile vile mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 unasisitiza kwamba
‘Ubaguzi dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki zao za msingi hususani haki ya kuheshimu utu wao na haki zao za msingi.’
Pia katika tamko la shirika la maendeleo kusini mwa Afrika SADC(2005) ambayo Tanzania ni mwanachama liliweka kiwango cha jinsia chini ya uwakilishi wawanawake kutoka kuwa asilimia 30%na baadae kupandisha hadi kufikia 5O%.
Kwa utanguizi huo hapo juu ni wazi kuwa jamii inapaswa kuelimishwa na kuoneshwa umuhimu wa wanawake kushiriki katika uongozi kutokana na umuhimu wa kundi hili ndani ya jamii na kupiga vita wale wote wanaotumia hila na nyadhifa zao kuwadhalilisha na kuwanyima haki zao wanawake.
Hivi sasa tatizo la udhalilishaji na rushwa ya ngono kwa wanawake kwenye vyama vya upinzani limekua kubwa kiasi cha kuwanyima fursa wanawake kushiriki katika uongozi ndani na nje ya vyama vyao.Ni wanawake wachache wanaoshiriki siasa nchini bila kukutana na vikwazo hivi kutokana na misimamo yao mikali ndani ya vyama vya upinzani.Hii inapelekea ushiriki wa wanawake ndani ya vyama vya upinzani kuwa mdogo ukilinganisha na ushiriki wao ndani ya chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni,yapo mambo kadhaa ambayo yalifanyika ndani ya uongozi wa vyama vya upinzani yanayodhihirisha uwepo wa rushwa ya ngono na udhalilishaji mkubwa wa kundi hili muhimu la wanawake ndani ya vyama hivi.Miongoni mwa mambo haya ni kama yafuatayo:
1.Ucheleweshaji wa haki za wanachama wanawake
Baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitakiwa kwa mujibu wa sheria kupeleka majina ya wanawake viti maalumu kuwakilisha chama na wanawake bungeni.Ucheleweshaji wa haki hii kwa wanawake waliostahiki umegubikwa na udhalilishaji na viashirishi vya rushwa ya ngono kwa wanawake waliostahili kupewa nafasi hizi.Mzozo unaoendelea hivi sasa ndani ya CHADEMA ni matokeo ya msimamo mkali wa wanawake waliokataa kudhalilishwa na viongozi wachache ndani ya chama.
2.Uteuzi ndani ya Vyama vya Upinzani
Ili uweze kugombea ndani ya Chama chochote ni lazima chama kikupitishe ndipo jina lako likubalike kwa ajili ya kugombea.Uteuzi ndani ya vyama vya upinzani kwa mwaka 2020 uligubikwa na usiri mkubwa na hujuma ambazo baadhi yake zilihusiha udhalilishaji mkubwa wa wanawake na rushwa ya ngono.Haya yaliwekwa pia wazi na Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) katika ripoti yake ya vitendo vya rushwa katika uchaguzi.
3.Gharama za uchaguzi
Kutokana na mfumo dume wa kurithi wa kiafrika ambao ulimpa mali mwanaume na kumnyima mwanamke ni wazi kuwa idadi kubwa ya wanawake wanaotaka kushiriki siasa kipato chao kinakuwa kidogo.Hivyo kuhitaji msaada ndani ya vyama au familia ili kumudu uchaguzi ambao unakua na gharama kubwa.Gharama za uchaguzi ndani ya Chadema zimekua zikitolewa kwa maamuzi ya viongozi wachache ambao wamekua wakitumia nafasi zao kutekeleza matakwa yao binafsi yakiwemo ya ngono na udhalilishaji wa wanawake.
4.Vitendo vya udhalilishaji katika uchaguzi
Viongozi wa juu wa Chadema wamekua wakiwatumia wanawake kwa kuwadhalilisha ili jamii na mataifa ya nje yaone kuwa Tanzania inawadhalilisha wanawake.Mfano,tukio la kutengeneza la kura za jimbo la Kawe ambalo lilipelekea Mh Halima Mdee kudhalilika kwa kujua kura zilizoletwa na waliotengeneza tukio na kuondosheka zililetwa na mgombea wa CCM.
5.Kuwatumia wanawake kuvunja sheria
Viongozi wa juu wa Chadema wamekua wakiwatanguliza mbele wanawake katika matukio mbalilmbali ya uhalifu kuwakabili polisi na kusababisha taharuki huku wao wakiwa nyuma,hii imepelekea mara kadhaa wanawake ndani ya vyama hivi kuanguka na kuvunjika mkono kutokana na matukio ya kutengeneza ya viongozi wao.
Zipo sababu nyingi zinazothibitisha udhalilishaji na rushwa ya ngono iliyokithiri ndani ya CHADEMA na umuhimu wa serikali kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizi kwa lengo la kuwalinda wanawake na jamii ya Kitanzania kwa ujumla.
Chadema ndiyo kazi yao. Hata wabunge wa viti maalum waliopita walilalamikia issue hii.Unaujua mchakato wake?Kaa kimya kama hujui,dada zetu wanadhalilishwa
Unaujua mchakato wake?Kaa kimya kama hujui,dada zetu wanadhalilishwachadema ilipitisha wanawake 68 kugombea majimboni hebu tuambie hao wanawake nani aliwadhalilisha kingono na wapi mpaka kuwapa hizo nafasi?
Chadema ndiyo kazi yao. Hata wabunge wa viti maalum waliopita walilalamikia issue hii.
Siasa ni sehemu ya maisha.Achana na siasa we chapa kazi
Punguza stress mkuu utakufa bure kunywa maji kidogo. Hebu angalia mwenye chama alivyo tweet hapa chini!!Sio uongozi wa chama....
Nchi hii inaendeshwa ki dikteta.. Unafikiri hao Covid 19 wameapa kwa hiari?
Kuna mwingine alikua jela Uhuru wake unatakana na kukubali ubunge
Halima baada ya kukubali kesi Zake zote zimefutwa.. Kama nchi taasisi zote kubwa zipo kisiasa unategemea nini
Mahakama..TRA.JESHI LOTE.. TAKUKURU.. USALAMA WA TAIFA
Hizi idara zote zipo kisiasa sana... Sasa unategemea maajabu gani?
Dada zako walidhalilishwa kwa kupendaUnaujua mchakato wake?Kaa kimya kama hujui,dada zetu wanadhalilishwa
Wewe bongo yako hamna kitu kabisa. Unafikiri hayo ya ngono na mambo mengine hayapo kwa CCM?Kwa mujibu wa tamko la Kimataifa kuhusu haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo lilibainisha msingi wa kutokubaguliwa kifungu cha (2)kinakariri
’kila binadamu ana haki sawa na uhuru bila kubaguliwa kwa misingi ya rangi utaifa jinsia lugha na itikadi za kisiasa’
Vile vile mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 unasisitiza kwamba
‘Ubaguzi dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki zao za msingi hususani haki ya kuheshimu utu wao na haki zao za msingi.’
Pia katika tamko la shirika la maendeleo kusini mwa Afrika SADC(2005) ambayo Tanzania ni mwanachama liliweka kiwango cha jinsia chini ya uwakilishi wawanawake kutoka kuwa asilimia 30%na baadae kupandisha hadi kufikia 5O%.
Kwa utanguizi huo hapo juu ni wazi kuwa jamii inapaswa kuelimishwa na kuoneshwa umuhimu wa wanawake kushiriki katika uongozi kutokana na umuhimu wa kundi hili ndani ya jamii na kupiga vita wale wote wanaotumia hila na nyadhifa zao kuwadhalilisha na kuwanyima haki zao wanawake.
Hivi sasa tatizo la udhalilishaji na rushwa ya ngono kwa wanawake kwenye vyama vya upinzani limekua kubwa kiasi cha kuwanyima fursa wanawake kushiriki katika uongozi ndani na nje ya vyama vyao.Ni wanawake wachache wanaoshiriki siasa nchini bila kukutana na vikwazo hivi kutokana na misimamo yao mikali ndani ya vyama vya upinzani.Hii inapelekea ushiriki wa wanawake ndani ya vyama vya upinzani kuwa mdogo ukilinganisha na ushiriki wao ndani ya chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni,yapo mambo kadhaa ambayo yalifanyika ndani ya uongozi wa vyama vya upinzani yanayodhihirisha uwepo wa rushwa ya ngono na udhalilishaji mkubwa wa kundi hili muhimu la wanawake ndani ya vyama hivi.Miongoni mwa mambo haya ni kama yafuatayo:
1.Ucheleweshaji wa haki za wanachama wanawake
Baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitakiwa kwa mujibu wa sheria kupeleka majina ya wanawake viti maalumu kuwakilisha chama na wanawake bungeni.Ucheleweshaji wa haki hii kwa wanawake waliostahiki umegubikwa na udhalilishaji na viashirishi vya rushwa ya ngono kwa wanawake waliostahili kupewa nafasi hizi.Mzozo unaoendelea hivi sasa ndani ya CHADEMA ni matokeo ya msimamo mkali wa wanawake waliokataa kudhalilishwa na viongozi wachache ndani ya chama.
2.Uteuzi ndani ya Vyama vya Upinzani
Ili uweze kugombea ndani ya Chama chochote ni lazima chama kikupitishe ndipo jina lako likubalike kwa ajili ya kugombea.Uteuzi ndani ya vyama vya upinzani kwa mwaka 2020 uligubikwa na usiri mkubwa na hujuma ambazo baadhi yake zilihusiha udhalilishaji mkubwa wa wanawake na rushwa ya ngono.Haya yaliwekwa pia wazi na Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) katika ripoti yake ya vitendo vya rushwa katika uchaguzi.
3.Gharama za uchaguzi
Kutokana na mfumo dume wa kurithi wa kiafrika ambao ulimpa mali mwanaume na kumnyima mwanamke ni wazi kuwa idadi kubwa ya wanawake wanaotaka kushiriki siasa kipato chao kinakuwa kidogo.Hivyo kuhitaji msaada ndani ya vyama au familia ili kumudu uchaguzi ambao unakua na gharama kubwa.Gharama za uchaguzi ndani ya Chadema zimekua zikitolewa kwa maamuzi ya viongozi wachache ambao wamekua wakitumia nafasi zao kutekeleza matakwa yao binafsi yakiwemo ya ngono na udhalilishaji wa wanawake.
4.Vitendo vya udhalilishaji katika uchaguzi
Viongozi wa juu wa Chadema wamekua wakiwatumia wanawake kwa kuwadhalilisha ili jamii na mataifa ya nje yaone kuwa Tanzania inawadhalilisha wanawake.Mfano,tukio la kutengeneza la kura za jimbo la Kawe ambalo lilipelekea Mh Halima Mdee kudhalilika kwa kujua kura zilizoletwa na waliotengeneza tukio na kuondosheka zililetwa na mgombea wa CCM.
5.Kuwatumia wanawake kuvunja sheria
Viongozi wa juu wa Chadema wamekua wakiwatanguliza mbele wanawake katika matukio mbalilmbali ya uhalifu kuwakabili polisi na kusababisha taharuki huku wao wakiwa nyuma,hii imepelekea mara kadhaa wanawake ndani ya vyama hivi kuanguka na kuvunjika mkono kutokana na matukio ya kutengeneza ya viongozi wao.
Zipo sababu nyingi zinazothibitisha udhalilishaji na rushwa ya ngono iliyokithiri ndani ya CHADEMA na umuhimu wa serikali kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizi kwa lengo la kuwalinda wanawake na jamii ya Kitanzania kwa ujumla.
Cheki tweet hapa ya mwenye chama. Acha utopolo mkuu.Dada zako walidhalilishwa kwa kupenda
Yule nusrat kakaa jela na kufanywa mbaya na askari wa CHADEMA?
Acha umbea mtoto wa kiume
Halima hana jinsi tangu jiwe kaingia madarakani Leo Ndio mara ya kwanza kalala bila kesiPunguza stress mkuu utakufa bure kunywa maji kidogo. Hebu angalia mwenye chama alivyo tweet hapa chini!!
View attachment 1634586