Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Haka kamtindo kakupost habari ambazo ndo tunaangalia sasa hivi kafutwe,.

Yaani mtu ukiona kipengele kimoja cha habari hata haijaisha ushapost.

Huku sio FB au udaku spesho.
 
Haka kamtindo kakupost habari ambazo ndo tunaangalia sasa hivi kafutwe,.

Yaani mtu ukiona kipengele kimoja cha habari hata haijaisha ushapost.

Huku sio FB au udaku spesho.
Tuma na wewe sasa.
 
Mimi sisapoti unafiki. Tume hawawezi kutangaza majina bila kupokea barua iliyosainiwa na mamlaka inayotambuliwa na msajili wa vyama plus muhuri. Huyo Mdee yuko very close na Mbowe. Hakuna kughushi hapo.
 
Mimi sisapoti unafiki. Tume hawawezi kutangaza majina bila kupokea barua iliyisainiwa na mamlaka inayotambuliwa na msajili wa vyama plus muhuri. Huyo Mdee yuko very close na Mbowe. Hakuna kughushi hapo.
Kuwa close na Mbowe, so what?
Unalazimisha hisia zako potofu zionekane kuwa kweli, wakati ni uhuni wako wa kihisia.

Msimamo wa CHADEMA na viongozi wake katika hili uko wazi na straight toka uchaguzi uishe, hakuna kuteua na hakuna kupeleka majina. Katika hili CHADEMA hakuyumba hata nukta moja mpaka sasa hivi.

Embu tafakari tu, Nusra Hanje ambaye alikuwa gerezani mpaka November 23, ilikuwaje uteuzi wake uthibitishwa na Spika tangu tarehe 20 November?

Note:
Huwezi ukateuliwa kuwa mbunge wa viti maalum bila wewe mwenyewe kujaza fomu ya uteuzi, kwenda kuapa mahakamani mbele ya jaji au Hakimu na kuirejesha kwa katibu mkuu wa chama chako.
 
Hivi aliekuwa anasema kufanya kosa sio kosa, kosa kurudia kosa ni nani!?? Mzee mwenzangu mlenda sio mzubo? Au ndo ukiwa mjenzi ujue kubomoa?
 
Mnyika akiri tu bila aibu kuwa hili jambo hakushirikishwa na wenzake if at all ni kweli hana taarifa.

Na asipoangalia hii ndio tiketi yake kutoka CHADEMA toka ziwepo fununu za kutaka kujitoa Slaa alipoondoka.

Yaani haiingii akilini watu wazima 19 wafunge safari toka huko walikokuwa mpaka Dodoma kuapa Bila Baraka za Chama. No way.
 
Wanachadema wanasubiri jambo moja tu hapa...FUKUZA!
Mnyika msanii tu, hivi unakuaje watu kama Halima Mdee na akina Matiko, waamke asubuhi, wavae suti wapendeze, waende bungeni kuapa bila hata kumpigia simu yeye au mwenyekiti wa CHADEMA? Hapa wanataka kuwazingua tu hao wamama
 
JOHN MNYIKA AMEMNTANTALIZE TUNDU LISSU.

Leo 22:05 hrs 25/11/2020

Nianze kwa kusema kuwa Tundu Lissu siyo mwanasiasa makini bali ni mwanaharakati mropokaji tu! Chadema hawawezi kamwe kuendelea na mtu kama Tundu Lissu,huwezi kuwa unatoa matamko yako binafsi halafu unataka yawe ndo msimamo wa Chadema!?

Ijumaa tutajua kwamba gharama ya kuwapoteza Tundu Lissu na John Mnyika hata kama wakijiuzulu ni ndogo kuliko kuwavua uanachama Wanawake 19 walioapishwa na hatimaye kuwataka wapoteze Ubunge wao ambao wamepata kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si hisani.

Kwa elimu ya Mdee na level yake chamani lazima awe na backup fulani kuongoza wamama 19 kuapa. Kihistoria Mnyika hana ubavu wa kumfanya lolote Mdee ndani ya CHADEMA nahisi kuna bomu kubwa linaenda kulipuka ijumaa kuigawa CHADEMA vipande vipande,Muda utaongea.

Chadema inabidi ing'olewe kutoka kwenye makucha ya viongozi wenye tamaa na wasio na maono kama Tundu Lissu na John Mnyika na kuiwekewa kwenye mikono ya wananchi kama taasisi. Mh. Aida Khenani Mbunge wa Nkasi, ameonyesha ukomavu wa kisiasa kuliko uongozi mzima wa Chadema ukiongozwa na John Mnyika.

John Mnyika chukua Madini haya,HALIMA J MDEE ni inner circle ya Chadema "asili' leo hii ndio Afukuzwe?!!!
Halima Mdee ndiye aliyewainspire wanawake wengi waliojiunga Chadema hasa Mabinti wa vyuo vikuu,yaani huyu Mdee atimuliwe Chadema simply?!!! Mnyika relax,take your time brother,

If you are smart Mnyika! There is something hidden by your Chairman ambacho labda hata wewe Mnyika haukijui ama unapretend kutokijua,lakini nikwambie Hallima Mdee anakijua😀 Wewe Mnyika endelea kuchoma mahindi,John Mrema where are you? Salum Mwalimu where are you? au kwa sababu kigogo kawataja mna wakeze😀 mmetulia tu mnasubiri upepo hadi Mwenyekiti Mbowe aongee😀

Sisi Wazee wa Leadership tulisomaga stage 10 za Communist Party of China, stage III ya the communist Party of China inaitwa "The art of political war",😀 Mnyika wakifika stage namba 3 lazima kuchemka😀

Stage III inasema :

a) Unatakiwa katika any political contest mshindani wako umpige sana achakae na adhalilike , na umwache hajitambui na hata kuomba msaada ashindwe kwa kuwa hajui anahitaji nini na afanye nini,( you have to strike hard and once to eliminate you leave him for dead, this must be beyond self examination )

b) Hata ikitokea amejikusanya kurudisha shambulizi,mashambulizi yake yawe hafifu mno kiasi hayawezi kuwa na madhara yakose shabaha na bila kulenga.

c) Lazima umwachie makovu makubwa (in his body politics and leadership) ambayo akitaka kuyatibu haraka basi makovu hayo yatamuuwa😀rudi shule bro Mnyika😀 unaweza kupigwa knock out round ya tatu.

Nimwambie John Mnyika ukiona jibwa lipo kwenye mti kileleni juu ujue kapandishwa na mwenyewe yupo chini na pengine mwenyewe uko nae,nimwambie John Mnyika hata aimbe agaregare chini hizo nafasi ni za wanawake,kama yeye Mwanamke basi aendelee kuzipinga,

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Katibu mkuu wa CHADEMA leo katika mkutano wake na vyombo vya habari, pamoja na mambo mengine aliwaomba wadau kutoa maoni na ushauri wao kwa kamati kuu ya chama itakayokutana tarehe 26/11/2020 kuamua hatua za kuchukua dhidi ya wabunge 19 wa viti maalum walioapishwa jana.

Busara na hekima zinatakiwa katika kuamua suala hili. Hasira siku zote huwa ni hasara. Tunapaswa siku zote kumutanguliza Mungu kwenye kila maamuzi magumu. Sheria zetu si cho chote dhidi ya hekima na busara. Sheria tumejitungia wenyewe na tunaweza kuzibadilisha wakati wo wote kama tunaziona zinatukwaza. Hekima na busara siku zote ziko juu ya sheria.

Ninashauri kuwe na maridhiano ya pande zote mbili on a win-win situation. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!
 
Kweli wanasiasa hawapo kwa ajili ya wananchi bali matumbo yao na familia zao. Watajuana wenyewe kwa vilemba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…