Kuna tetesi kuwa wabunge 19 wa viti maalumu wa CHADEMA wanapanga kugomea wito uliotolewa na Katibu Mkuu J. Mnyika kufika mbele ya Kamati Kuu kesho tarehe 27.
Kitendo cha wabunge hao kutofika mbele ya KK kitaonyesha mwendelezo wa dharau nyingine kwa mamlaka hiyo, vilevile watakuwa wamepoteza haki yao ya msingi ya kujitetea ikiwa ni pamoja na kujibu kwanini wasifutiwe uanachama.
Ifahamike kwamba Kamati Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kuteua majina ya viti maalumu, KK imepewa mamlaka ya kusimamisha au kufuta uanachama wa mwanachama yeyote.
Kama bado ni wanachama wa Chadema nawashauri waendelee kuheshimu mamlaka za chama ikiwemo KK na viongozi wakuu wa chama.