Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Hiyo fomu haiwezi kujazwa gerezani?
Kwa interest ya nani hadi ijaziwe gerezani? Nani aliyehusika kumtoa huyo Nusrat gerezani usiku? Umesikia kiongozi yeyote wa CDM aliyehusika kumtoa huyo Nusrat? Utakumbuka ambavyo imekua ni vigumu kuwatoa wapinzani magerezani wanapokua wametuhumiwa na kuwekwa huko. Kwa nini kwa huyu kumekua na huu wepesi tena usiku?

Ukumbuke pia shauri lake lililomuweka huko ilikua lisikilizwe tarehe 25 lakini yeye katolewa gerezani tarehe 23 na kusafirishwa Dodoma kwenda kuapa tarehe 24 siku moja tu kabla ya siku ya kufika mahakamani kusikiliza shauri lake. Jiulize shauri lake limeishaje?
 
CHADEMA hapa wamewekwa mtu kati. Maamuzi yoyote ya kukurupuka yana kwenda kuimaliza Chadema.

Wakijaribu kuwafukuza hao wabunge basi wajue imekula kwao na ndio mwisho wa Chadema.

Maana Nfugai hatawafukuza bungeni. Hawa wadada wataendelea kuwa wabunge for the coming five years.

Bila kujali itakuwa hawana chama. Warejee bunge lililo pita.
Hapa inahitajika busara ya hali ya juu kufikia muafaka wa hili jambo.
 
Kwa uwezo wa akili yako hayo ndio uliyoyaona. Hali halisi nchi haikufanya chaguzi zozote.

Pili nchi sasa hivi hakuna sheria zinazofanya kazi kwa manufaa ya umma...
Ndugu yangu jazba imefunika hata uwezo wako mdogo wa kufikiri....umebaki kulalamika tu na kuelekeza shutuma Bila kujua ni Nani anastahili shutuma zako...Mdee na wenzake ni werevu na wajanja ...umemsioia Mdee anavyomponda Mnyika? Anasema alikuja Chadema na malapa na hawezi kushindana na heavy weights...Akina Mdee wameruhusiwa na Kamati Kuu ya Chadema...Kama hutaki hayo baki hivyo hivyo..
 
Ndugu yangu jazba imefunika hata uwezo wako mdogo wa kufikiri....umebaki kulalamika tu na kuelekeza shutuma Bila kujua ni Nani anastahili shutuma zako...Mdee na wenzake ni werevu na wajanja ...umemsioia Mdee anavyomponda Mnyika? Anasema alikuja Chadema na malapa na hawezi kushindana na heavy weights...Akina Mdee wameruhusiwa na Kamati Kuu ya Chadema...Kama hutaki hayo baki hivyo hivyo..
Ndio uwezo wako wa kufikiri Sina ushauri nikionacho hukioni. Nakuonesha mwezi wewe unaangalia kidole changu.
 
Maoni yangu kwa chadema ni kuwafuta uanachama wabunge wote waliofanya usaliti huu wa kihistoria, CHADEMA ni chama kikubwa zaidi ya hao wasaliti,,kinyume chake wanachama wengi watakosa imani na chama na kusababisha mpasuko hata kufa kwa chama .

Mytake;
Nasubiri tamko nijue chakufanya!!
Hongera ACT kwa msimamo mkuu.
FB_IMG_1606300776903.jpg
 
Hiyo fomu haiwezi kujazwa gerezani?

Ha ha ha ha Yohana Mbatizaji katika ubora wako kabisa. Sasa umeanza kutufunulia miujiza na mazingaombwe!

Dah, ndio kwanza tunashuhudia katika Tanzania yetu hii mtuhumiwa wa ugaidi akipelekewa ubunge kwenye beseni akiwa gerezani! Endelea kutupa darasa maridhawa Mkubwa.[emoji38]
 
Ndugu yangu jazba imefunika hata uwezo wako mdogo wa kufikiri....umebaki kulalamika tu na kuelekeza shutuma Bila kujua ni Nani anastahili shutuma zako...Mdee na wenzake ni werevu na wajanja ...umemsioia Mdee anavyomponda Mnyika? Anasema alikuja Chadema na malapa na hawezi kushindana na heavy weights...Akina Mdee wameruhusiwa na Kamati Kuu ya Chadema...Kama hutaki hayo baki hivyo hivyo..
Hiyo audio nimeisikia, haimuhusu Mnyika wala hiyo ishu yao ya viti maalum. Kwenye audio Mdee anamsema Silinde.
 
Majina ya wanawake wa viti maalum huchakatwa mapema hata kabla ya uchaguzi mkuu. Hili ni swala la kisheria zaidi na mdee ni lawyer.
Kama ni hivyo mbona wanasema hakuna orodha iliyopelekwa kwa msajili? Basi makosa yalianzia hapo. Hawakutimiza takwa la kisheria.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unafikiri kina Halima ni wajinga?

Kina Lijuakali waliporudi bungeni baada ya kina Mbowe kugomea bunge kisa corona mbona walifukuzwa bila kuitwa? Alafu hawa wanabembelezwa tena wamewekewa na tarehe ya mbali ili wapate muda wa kujiandaa unafikir ni kwanini?

Kwa taarifa yako hayo yote yliyofanyika yana baraka zote za Mbowe, na baada ya tarehe 27 utajiona mjinga sana.
Na hata Mnyika anajua ila wana buy time ili nyie wajinga msivurugike mazima.
we unawaona wanaakili hao? akili zao zimeshikiliwa na ******
 
Hiyo audio nimeisikia, haimuhusu Mnyika wala hiyo ishu yao ya viti maalum. Kwenye audio Mdee anamsema Silinde.
Sawa...ok...elewa hivyo hivyo....hainihusu ...mtaelewana wenyewe...whether ni ya Mnyika sijui silinde sijui wewe sijui Nani mtajuana wenyewe mnaopambana...bavicha wameshatoa tamko...tunaeubiri makundi mengine ya chadema mkiwamo myie wa mtandaoni...
 
Kujiuzulu kwa sababu ya makosa ya wengine ni kukosa utambuzi,,, yeye asimamie mamlaka yake basi na kuhakikisha utaratibu na sheria vinafuatwa! Huko ndiko kuonesha ukomavu wa kiongozi
Nadhani inapaswa kuwa hivyo katika uongozi. Inaitwa kuwajibishwa au kitu kama hicho (accountability ). Fuatilia habari za vifo vya wafungwa gerezani enzi hizo. Kuna kiongozi mkubwa kitaifa aliwajibika (alijiudhuru).
 
Chadema imebakiwa na masaa 24 ya uhai wake hadi kesho mchana. MkiwafutaHalima &co then; NO MORE NO LESS.Haahahah wanawake ni jeshi kubwa
 


Leo Novemba 25, 2020 katibu mkuu wa CHADEMA amezungumza na vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho eneo la Ufipa, Kinondoni mada kuu ikiwa uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambapo uapisho wao ulifanyika jana bungeni jijini Dodoma jana.

Yafuatayo ni maelezo kwenye mkutano huo kuanzia mwanzo hadi mwisho pamoja na maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

PIA, SOMA: Hatimaye Wabunge wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

=> Ester Matiko: Kama chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

============​

JOHN MREMA: Mbele yetu katibu mkuu wa chama, John John Mnyika akiwa na mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na mahusiano ya mambo ya nje na msemaji mkuu kwa siku ya leo atakuwa katibu mkuu wa chama.

JOHN MNYIKA: Tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi ulioitwa uchaguzi mkuu ambapo mtakumbuka kati ya mambo yaliyofanyika ni hujuma za wazi za mfumo wa kiserikali ukihusisha tume ya Taifa ya uchaguzi kupika matokeo ya uchaguzi.

Chama cha demokrasia na maendeleo hakijateua wabunge wa viti maalum au wagombe ubunge viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum.

Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.

Pili katibu mkuu wa chama ambae ndie mwenye mamlaka ya kimawasiliano ya kuwasiliana na tume ya Taifa ya uchaguzi, katibu mkuu wa chama sijawahi kuwasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya wanaoitwa waliopendekezwa wabunge wa viti maalum.

Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.

Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.

Chama inabidi kichukue hatua, katiba yetu inasema hatua zozote zisichukuliwe bila ya wahusika kuitwa, kujieleza. Sasa kwa kuwa hili jambo ni la dharula, chama kitatumia utaratibu wa dharula katika kushughulika na jambo hili na tutaongozwa na kanuni za chama.

Kwa kuwa mamlaka ya jambo hili ni kamati kuu ya chama, naomba kuwatangazi kwamba tumeitisha kikao cha kamati kuu ya chama maalum, kitafanyika siku ya Ijumaa tarehe 27 hapa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa tutawaandikia wahusika, ili kusitokee kisingizio kwa yeyote kwamba hakuitwa, hakupata taarifa ya kuitwa naomba kutangaza 'Public notice' kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana tarehe 24 kufika makao makuu ya chama bila kukosa.

Kuna tukio la mwanachama wetu ambae ni kiongozi wa baraza la baraza la vijana la CHADEMA, Nusrat Hanje ambae amesota ndani kwa kesi ya kubambikiziwa kwa siku 133 akiwa mahabusu na leo tarehe 25 mahakama kuu ndio ilikuwa inakutana kutoa uamuzi juu ya rufaa ambayo amekata baada ya kusota ndani kwa muda mrefu.

Kituko kinachoashiria mfumo kuhusika katika huu mchezo, tarehe 23 usiku alikwenda kutolewa gerezani ili kesho yake apelekwe kuapa na alitolewa na mfumo bila hata kuzingatia masharti ya kisheria. Tunashkuru kwamba mwanachama wetu na kiongozi wetu ametoka baada ya kusota ndani kwa muda mrefu lakini mfumo ulimtoa ili kutekeleza malengo yao.

Sasa Ndugai amesema alipelekewa majina tarehe 20 Novemba na tume, Nusrat Hanje alietolewa gerezani tarehe 23 Novemba, uteuzi wa tume unasema umefanyika tarehe 20, fomu yake aliijaza lini, hakimu aliemuapisha alikuwa wapi kabla ya tarehe 20 tume ilipomteua mambo ambayo yanadhihirisha wazi kwamba hili jambo ni kazi ya mfumo.

Lengo la wazi la mfumo ni kutaka kufifisha ajenda ya kwamba Tanzania ilifanya uchaguzi haramu tarehe 28 Oktoba ulioitwa uchafuzi wakati umma ukishinikiza, jamii ya kimataifa ikishinikiza, bunge likionekana la chama kimoja ili kujaribu kulipa uhalali serikali ya illegitimate president Magufuli ikaamua kushiriki huu mchezo haramu wa kuhusisha tume, spika wa bunge na hatimaye tumefika hapa tulipofika.

Nitoe rai kwa watanzania, jambo hili lisitutoe watanzania kwenye mjadala mkubwa na muhimu zaidi kwamba tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi na kwamba sisi tunataka uchaguzi ufanyika upya chini ya tume huru ya uchaguzi.

Sisi tunaotaka hilo tunatengenezewa mazingira ya mjadala kuhama, umma wa watanzania usikubali kuingizwa kwenye mtego wa dola wa kuhamisha mjadala na kufifisha hasira za wananchi.

Kauli iliyotolewa jana wakati wa kuapishwa iliyotaka kujenga ishara kama mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe alihalalisha hili linaloendelea, hii kauli sio ya kweli na mwenyekiti wa chama ndie atakaeongoza kikao cha kamati kuu ya chama kitakachofanyika tarehe 27.

MASWALI NA MAJIBU

MWANDISHI (Halifa-Mwandishi wa kujitegemea):
Swali la kwanza kwa Mnyika, unadhani hili suala litaiacha vipi CHADEMA kama chama kwa sababu kuna hofu, ukizingatia watu walioenda bungeni kuapishwa, kina Mdee, Ester Matiko ni watu wakubwa kwenye chama, unadhani litakiacha chama salama?

Swali la pili, umesema hili suala limetengenezwa na mfumo kwamba kuna hujuma flani unadhani CHADEMA kinafanyiwa, katika mazingira kama hayo unadhani CHADEMA kinapaswa kuchukua hatua gani? Mnakabiliana nalo vipi suala la mfumo kujaribu kuhujumu chama chenu ili kuepusha matukio kama hayo kujirudia siku za mbeleni.

JOHN-Dar Mpya: Swali la kwanza, katibu mkuu umesema sakata zima hili la kuwaapisha kina Halima limekuwa 'engineered' na dola lakini kuna taarifa ambazo mimi binafsi nnazo kwamba majina haya, mchakato mzima huu wa maandalizi ulifanyika ndani ya ofisi ya katibu mkuu aidha ni wewe au wasaidizi wako. Kama kiongozi nilitegemea utaweka pia 'doubt' kwamba dola haiwezi kulikamilisha jambo hili bila kushirikiana na viongozi ndani ya chama maana yake wewe kwenye uongozi mzima wa chama haujaonyesha hata mashaka yoyote yale kwamba inawezekana dola imesaidiwa na either watu ndani ya ofisi yako au ndani ya CHADEMA kwa sababu wewe umejaribu kutuonyesha fomu hapo kwamba fomu za tume umekadhibiwa katibu mkuu lakini what If mtu anajenga hoja kwamba ya msaidizi wako alipitia mlango wa nyuma alienda akazichukua hizo fomu ofisi ya tume akaja akazisaini kwa niaba ya katibu mkuu kwa sababu unavyosema saini ni ya katibu mkuu inatakiwa, what if kuna barua ambazo chama kimekuwa kikifanya mawasiliano na tume kupitia naibu katibu mkuu

Swali la pili, uasi na usaliti ndani ya CHADEMA, hawa watu walioenda kuapa ni viongozi wakubwa ndani ya CHADEMA, mimi naona jambo hili hawa watu hawawezi kuwa wamekwenda bila 'top management' kuwa nyuma yao. Hii 'courage' na 'doubt' yangu inaweza kuwa inasapotiwa na kauli ya Halima jana kwamba alimtaja mwenyekiti, unazungumziaje level ya uasi huu?

REGINA-Mwanahalisi: Kilichofanywa na kina Halima Mdee ndio hichi hicho kilichofanywa na mbunge Aida Khenan lakini hapo katibu mkuu amesema wanaopaswa kuja siku ya Ijumaa ni hao wabunge 19 walioapa jana, vipi kuhusu Aida?

MAJIBU
JOHN MNYIKA:
Nianze na la Aida, nilisema leo nimekuja kuzungumzia walioapa jana, hizi ni kesi mbili zinashahabiana lakini ni case mbili tofauti kwa sababu case ya walioapa 19 kimsingi inahusisha cilevile kughushi orodha ya majina ya chama na mchakato mzima wa fomu.

Suala la Aida linahusisha kukiuka tamko lililotolewa na viongozi wakuu wa chama, haya yote mawili tutayashughulikia na kila moja tutashughulikia kwa namna yake.

Maswali ya Halifa, kwamba chama kitabaki salama, naomba niwahakikishie watanzania chama hiki kitaendelea na kitabaki kuwa salama, kitapita katika mchakato huu kikiwa na nguvu zaidi ya kuendelea kujipanga kushika dola na historia ya CHADEMA inadhihirisha hivyo.

Umenukuu jambo hili limehusisha mfumo, sasa tutachukua hatua gani. Naomba nisizungumze hatua kwa sasa kwasababu kama nilivyosema tunakwenda kufanya kikao cha kamati kuu tarehe 27 na nitoe wito kwa wanachama na viongozi popote pale, milango iko wazi na wadau wa demokrasia kutoa maoni kwa chama juu ya ni hatua gani zikachukuliwe na kamati kuu tarehe 27 kwahiyo sitaki kutoa hukumu.

John, Dar Mpya mpaka ninavyozungumza na nyinyi sijaletewa ushahisi na yoyote juu ya uhusika wa mtu yoyote ndani ya ofisi ya katibu mkuu kushirikiana na mfumo kufanya jambo hili. Jambo ambalo nina hakika nalo moja kwa moja, hao 19 walioenda kuapa walishiriki kwenye huu ubatili na wanaufahamu huu ubatili.

Narudia kusisitiza halina baraka zozote za mwenyekiti Mbowe kwa hiyo ndugu John ulieuliza swali ni vyema ukafatilia na ukaandikana pia ukapata 'quotation' kati ya viongozi wakubwa unaosema wamebariki au wameunga mkono jambo hili, ni kiongozi gani?

Jambo la kuzingatia, kiongozi mmoja mmoja anaweza akawa na mawazo yake binafsi, wapo waliokuwa na maoni kwamba tupeleke majina haraka, wengine wanasema tusipeleke, wapo wanaosema tuendelee na msimamo wetu uleule wa kutopeleka majina, hiki ni chama cha demokrasia na maendeleo, watu wanaweza kuwa na maoni lakini ajitokeze mtu mmoja aseme ni kikao gani kimekaa kikafanya uteuzi wa majina, hakuna mtu atakaekwambia.

Kwa ufupi hawa waliokwenda kuapa, kimsingi walijiteua na wakashirikiana na dola kwenda kuhalalisha huo ubatili, usaliti, uasi na uharamu wa kushiriki kiapo, sasa chama kitachukua hatua gani? Hio sio kazi ya katibu mkuu. Kazi ya katibu mkuu ni kuhakikisha kamati kuu imeitishwa, itafanyika Ijumaa na chama kitaeleza hatua ambazo itachukua, tunawashukuru sana.


Kwa hilo nalo mnaisingizia chama utawala? Kwani waliapa kwa kushikiwa bunduki? Si kwa hiari yao??
Tukikua tutaacha
 
Back
Top Bottom