Nimejaribu kutafakari sana kuhusu vichwa nilivyokuwa naviamini sana kwa misimamo yao ya kisiasa lakini wameamua kuchukua hatua kali ya kujitosa Bungeni aidha kwa nguvu yao au kwa kibali cha chama
Ukirejea maelezo ya katibu mkuu ni dhahiri chama hakina baraka ktk tukio hilo lakini upande wa pili m/kiti wao anaashiria kama yalikuwepo malumbano juu ya kupata muafaka
Sasa ni nini kimewasukuma kutenda hayo;-
1: Inawezekana hasara walizopata zimewachanganya gharama ya kampeni , kesi zisizokwisha, majeraha ya vipigo, kuwekwa rumande mara kwa mara na kudhalilishwa kwa ajili ya kutafuta maisha rafiki kwa wananchi
2: MREJESHO haukupatika maana yake ili tuvune mazao mazuri na mengi ni sharti tushiriki wote kuanda, kulima na kuvuna (nguvu ya pamoja)
Uchaguzi huu kila mtu kauona kwa hali kama hii iliojitokeza unadhni 2025 kunaweza kuwa na mabadiliko kwa wapiga kura hawa hawa? Ni kiongozi gani wa kisiasa atakubali kuathirika kwa ajili ya wananchi? Ambao hawana uwezo wa kujitetea?
Mm nashauri hao walioapishwa wasitengwe washirikiane na viongozi ili wajaribu kutafuta plan B waendelee kuwaelimisha wananchi naamini tukikaa nao vizuri watatufahamisha dhumuni lao la kuwa Wabunge
Nawaomba wanamageuzi wote kutokata tamaa ziko mbinu nyingi za kuleta mabadiliko tuwaamini viongozi na kuyafuata maelekezo yao