Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Chadema wako vizuri sana kwenye kuchukua maamuzi magumu, hao wafukuzwe tu, alifukuzwa Slaa Zitto , na katibu mkuu Dr. Mashinji na bado wakashinda uchaguzi mkuu wa 2020,na ccm wakakimbia na maboksi
 
Kweli wanasiasa hawapo kwa ajili ya wananchi bali matumbo yao na familia zao. Watajuana wenyewe kwa vilemba
Ni wakati wananchi wa tanganyika waelewe kuwa hii nchi si ya kupiganiwa na chama fulani, bali watu wote. Hata kama huendi vitani, watie moyo waliopo vitani, sio unawaacha unaenda kula bata unategemea wafie huko kwa ajili yako. Wananchi mjifunze. Chama hakiwapiganii msipojipigania wenyewe

Acheni upumbavu bwana.
 
Nimeamini kwenye mpira professors na darasa la saba failer hawana utofauti kiushabiki.
Ngoja tusubiri hiyo ijumaa tutajua mbivu na mbichi
 
Yawezekana ulisoma stage zote hizo kumi lkn hujawahi kuongoza hata kikundi cha watu 30. Kuongoza taasisi ya watu wazima, wenye umri, elimu, uelewa na dini tofauti ni kazi.

Pamoja na kusoma na kuandika, wewe mtoa maada ukipewa hata nafasi ya Katibu wa wilaya unaweza KUCHEMKA kupita maelezo.

Safari ya CHADEMA bado inaendelea, matukio kama haya ndo yanaifanya safari iwe safari halisi, ili watakaofika hadi mwisho watasimulia haya mapito na mitihani.

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Chadema wako vizuri sana kwenye kuchukua maamuzi magumu, hao wafukuzwe tu, alifukuzwa Slaa Zitto , na katibu mkuu Dr. Mashinji na bado wakashinda uchaguzi mkuu wa 2020,na ccm wakakimbia na maboksi
Mbona kwenye list yako aliefukuzwa ni zitto tu!
 
Hizi busara na hekima hazikutumika mlipo pora ushindi na kutoheshimu maamuzi ya wananchi ili muendelee kutawala kwa mabavu.
 
Mnyika akiri tu bila aibu kuwa hili jambo hakushirikishwa na wenzake if at all ni kweli hana taarifa.

Na asipoangalia hii ndio tiketi yake kutoka CHADEMA toka ziwepo fununu za kutaka kujitoa Slaa alipoondoka.

Yaani haiingii akilini watu wazima 19 wafunge safari toka huko walikokuwa mpaka Dodoma kuapa Bila Baraka za Chama. No way.
Propaganda zenu za kijani kibichi ndio mnafikiri mtatutoa kwenye reli , majitu mizima Haina hata aibu inaenda kuteka wanawake na kuwalazimisha ubunge wa viti maalum ? Mlivyo majinga mkaenda kumtoa na Nusrat Hanje jela ,kesi yake si haina dhamana?

Eti mmepangia Mdee maneno ya kusema eti anamshukuru Mbowe kwa kuwaruhusu , mapimbi kweli nyinyi , Mbowe awaruhusu bila kamati kuu ? Mbowe awaruhusu bila maandishi ? Halima hebu tupe maandishi weka hapa Mbowe amewaruhusu kwenda bungeni? Tafuta hata barua ya kufoji.

Waambie maafisa vipeuo mamasta wa hili zoezi wskusaidia kufoji barua Mbowe amewaruhusu kwenda bungeni , halafu kesho muisambaze mitandaoni nyie mapimbi wa fikra .
 
Katibu mkuu wa CDM leo katika mkutano wake na vyombo vya habari, pamoja na mambo mengine aliwaomba wadau kutoa maoni na ushauri wao kwa kamati kuu ya chama itakayokutana tarehe 26/11/2020 kuamua hatua za kuchukua dhidi ya wabunge 19 wa viti maalum walioapishwa jana...
Jomba lazima watu wajue matumizi ya sheria wakati wote..na hi itatujenga wananchi...sheria ifuate mkondo wake..ukizungumzia busara hapa utafika sehem utakwama
 
Wabunge 19 wa viti maalum wa chadema ni ajira mpya inaandaliwa baada ya kufukuzwa hao wote.

Hovyo kabisa,walimu,madaktari,wauguzi,askari hali zao ngumu kimaisha halafu wao wanatumia fedha ktk mambo ya kijinga.
 
Imekuaje raia wa TANZANIAA wanaishi kama wageni kwenye Taifa Lao? Maana hawajali lolote wala chochote kuhusu serikali na mambo yanayofanyika ndani ya serikali, ili mradi maisha Yao yanasonga mbele kwa kupata ubwabwa na mboga wanaona ni Sawa tu.

Ukimya wao unaweza Sema Wana Taifa lingine tofauti na hili, Kwamba hapa wamekuja kutafuta tu na hawana haja ya Kutengeneza mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho.

Tume fika pahala raia wa Tanzania bila aibu anasema yeye siasa haimuhusu kwasababu sio mwana siasa! Anyway hapo utasema labda walinyimwa elimu ndio maana wanatoa kauli kama hizo.

Tuzidi kuwaombea hawa raia.
 
Hizi busara na hekima hazikutumika mlipo pora ushindi na kutoheshimu maamuzi ya wananchi ili muendelee kutawala kwa mabavu.
Tuachane na hiyo dhana ya CCM kupora ushindi kwani hadi sasa hakuna hata mgombea ubunge yeyote aliyeshindwa katika uchaguzi huo aliyefungua kesi mahakama kuu kulalamikia kuporwa kura zake.

Turudi kwenye mada. Tushauri kamati kuu ya CHADEMA ili maamuzi watakayoyatoa hiyo kesho kutwa yawe ya busara na hekima wakimtanguliza Mwenyezi Mungu!
 
1. Ripoti polisi suala la kufoji mihuri ya Chama (kama kweli kuna forgery)

2. Fukuza uanachama wasaliti hao, maana wametenda kosa kubwa kabisa la kikatiba ya chama kwa kula njama na kutekeleza njama hizo za kufoji maamuzi ya chama wakati siyo kweli. Pia kufukuza wasaliti hao kutakiimarisha chama kwa sababu mtu mwingine yeyote in the future bila kujali cheo chake atakuwa anajua kuwa aivuka mipaka ya chama kwa kutanguliza maslahi yake binafsi chama hakitosita kumshughulikia. Chadema wakirembaremba kwenye hili tutajua uongozi umewapa baraka wasaliti wale na hivyo nao tutawapuuza
 
Tuachane na hiyo dhana ya ccm kupora ushindi kwani hadi sasa hakuna hata mgombea ubunge ye yote aliyeshindwa katika uchaguzi huo aliyefungua kesi mahakama kuu kulalamikia kuporwa kura zake.

Turudi kwenye mada. Tushauri kamati kuu ya cdm ili maamuzi watakayoyatoa hiyo kesho kutwa yawe ya busara na hekima wakimtanguliza Mwenyezi Mungu!
Hizi mahakama za bongo zimeshakuwa na element za "kuunga mkono juhudi" , haziaminiki, ukienda huko CCM watafuraaahi, maana wataitumia mahakama kulegitimise uhuni wao
 
Leslie Mbena asante sana.Yaani unasoma kitu unakisikia kinavyoingia akilini.Sitaki niongeze niakuhazeribia post yako.Ila nawaomba wasomi wengine kama Leslie wazidi kutupa vitu kama hivi sisi ambao shule siyo sana nadhani JF itakuwa uwanja mzuri sana wa siasa zetu za ndani.
 
Jomba lazima watu wajue matumizi ya sheria wakati wote..na hi itatujenga wananchi...sheria ifuate mkondo wake..ukizungumzia busara hapa utafika sehem utakwama
Kwa hiyo wewe hata familia yako unaiendesha kwa mtindo wa STK ie Sheria, Taratibu na Kanuni tu?
 
Inawezekana,angalia tweets ya Mbowe.

2624063_IMG-20201125-WA0019.jpg

Sio kila mtu ana imani na Mbowe, ila hii uliyoileta ni fake news. Nenda kwenye chanzo cha hiyo taarifa yako utakutana na maelezo ya huo upotoshwaji wa makusudi.
 
Hizi mahakama za bongo zimeshakuwa na element za "kuunga mkono juhudi" , haziaminiki, ukienda huko CCM watafuraaahi, maana wataitumia mahakama kulegitimise uhuni wao
Mkuu Missile of the Nation hadi leo sijui unaamini nini zaidi ya lawama tu, kama huamini Tume ya Uchaguzi, ushindi halali wa CCM, utawala wa sheria, maendeleo yaliyopatikana, nk lakini unamwamini M/Kiti wa chama mlevi kupindukia. Sakata la wabunge wateule kuidhinishwa na yeye kinyume cha Katiba ya chama ni ushahidi wa utawala wa kidikteta ndani ya chama.

Kama kweli wewe ni mtu makini ni vyema ukachunguza na kutathmini kinachoendelea kwenye hicho chama chako. Toa boriti jichoni mwako kwanza
 
JOHN MNYIKA AMEMNTANTALIZE TUNDU LISSU.

Leo 22:05 hrs 25/11/2020

Nianze kwa kusema kuwa Tundu Lissu siyo mwanasiasa makini bali ni mwanaharakati mropokaji tu! Chadema hawawezi kamwe kuendelea na mtu kama Tundu Lissu,huwezi kuwa unatoa matamko yako binafsi halafu unataka yawe ndo msimamo wa Chadema!?....
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787][emoji85] Umeweka na namba moja kwa moja !!. Mbona baba yako amesema hateui tena ?!.

Mchezo uliofanyika ktk sakata la viti maalumu 19 vya Cdm ni uhuni dhidi ya Cdm yenyewe. Na ni uhuni dhidi ya democracy ya nchi.
 
Maswali yafuatayo yanapaswa kujibiwa na Mbowe/ Mnyika:

1. Nani amepeleka Orodha ya Majina ya Wabunge wa Viti Maalum NEC?
2. Orodha hiyo imepelekwa kwa njia gani?
3. Kama msimamo wa chama na wa Katibu Mkuu ni kuwa Orodha haikupelekwa, walioapishwa jana walipatikanaje?
4. Hatua gani zinachukuliwa na CHADEMA ikiwa usaliti umetokea?
5. Ilikuwaje Nusrat Hanje aachiwe tu kutoka mahabusu na asubuhi yake aapishwe kuwa Mbunge wa Viti Maalum?
6. Nani yuko nyuma ya suitafahamu hii nzima ndani ya CHADEMA na anashughulikiwaje?

Kisheria, timeline ya kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wabunge wa kuteuliwa ikoje? Tunaweza kuwa tunahangaika na swala ambalo kisheria lilifanyika hata kabla ya tarehe ya uchaguzi. Kumbuka, mapendekezo sio uteuzi per se. Uteuzi rasmi unafanywa na NEC baada ya uchaguzi wa wabunge wa majimbo kukamilika!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom