Uchaguzi 2020 Mnyika: Uchaguzi 2020 mawakala kutopewa fomu za matokeo

Duh! Kwa hiyo baada ya uchaguzi tusitegemee kesi za kupinga matokeo maana hakutakuwa na ushahidi kwa walalamikaji

Kafulila alipigana usiku na mchana kwasababu ya hizo fomu hadi alipofika bei (msemo ulioenea sasa hivi) ya kupewa cheo serikalini ndio akakubali
 
Hapo ndio pa kutoshiriki uchaguzi. Afadhali ijulikane tu kwamba wameshiriki peke yao. Kushiriki uchaguzi kwa kanuni hizi ni "kuhalalisha" ushindi wa Magufuli na ccm yake, na vyama "washirika" CUF na NCCR na vingine kama TLP nk.
 
Hapo ndio pa kutoshiriki uchaguzi. Afadhali ijulikane tu kwamba wameshiriki peke yao. Kushiriki uchaguzi kwa kanuni hizi ni "kuhalalisha" ushindi wa Magufuli na ccm yake, na vyama "washirika" CUF na NCCR na vingine kama TLP nk.
Hakuna uchaguzi ni kuhalalisha wateuliwa wa mkulu
 
Hongera Mnyika na wadau wengine makini. Kuna watu wajinga sana wanacheza na amani ya Watanzania kwa sifa za hovyo.
 
Mm sijaisoma, ila iwapo kipo hicho kpengele basi haiasksi tafsiri halisi ya haki na wajibu. Iweje asipewe alichokisimamia kama ushahidi
NEC acheni kuandaa mazingira ya watu watakaoshindwa kwa haki kulalamika na kuleta ghasi bila sababu. Naamni wadau watalifanyia kazi kwa kuwa NEC nayo inawatu ambao hawajamilika Kama wanadam
 
Hakuna kukubaliana na hizo kanuni, na inatakiwa iwekwe wazi wananchi wote wajue. Huo ni ushahidi kuwa ccm imechoka kushindana.
Mkuu tindo unaongelea Wananchi wa nchi gani hiyo?

Umesahau yaliyofanyika katika uchaguzi wa serikali za Mitaa na yamepita na kusahaulika?

Na wasipo saini uchaguzi Mkuu ndio basi tena kama uchaguzi wa serikali za Mitaa mapema mwaka huu!

Hii nchi ngumu sana aisee!
 
Hakuna kukubaliana na hizo kanuni, na inatakiwa iwekwe wazi wananchi wote wajue. Huo ni ushahidi kuwa ccm imechoka kushindana.
Napendekeza vyama vya upinzani wasiishie hapo, kulalamika tu. Huu ndio wakati mwafaka wa kuwahusisha wananchi wayaelewe vyema mambo yanayopangwa kufanyika kabla ya uchaguzi.

Tatizo wanaishia kulalamika na hawaweki juhudi kubwa zaidi angalao basi wawaeleze wanachama wao (milioni 10?).
Hawa wanao uwezo kamili wa kuzuia uchaguzi wa kipuuzi usifanyike.

Hiyo kanuni haiwezi kutenguliwa mahakamani? Ni wakati wa kuwa-'proactive' sana sasa hivi kuzuia hizi mbinu za kishetani.
 
Hawa mbwa ccm kwa nn wanaogopa sana uchaguzi?
 
Wakati viwanda vikivyoachwa na JK tu vimeshakufa
Itapendeza sana kama kutakuwepo mjadala hapa JF kuhusu viwanda vilivyoanzishwa Tanzania miaka minne (tukiondoa mwaka wake wa kwanza, kwani hivyo ni mipango ya mtangulizi wake).

Kiasi cha uwekezaji nchini, miradi ya wananchi wenyewe, na wale toka nje ya nchi.

Bahati mbaya wasomi wetu katika eneo hili hawawezi kuifanya kazi hii kulinda usalama wao. Hali kadhalika waandishi wa habari nao ni mwiko kuchapisha habari hizi.

Kile kitengo cha uwekezaji kilichokuwa moto moto wakati wa Kikwete, siku hizi ni kama hakipo kabisa, kwa sababu hawana kazi ya kufanya tena!
 

Mkuu uko sahihi, acha wasishiriki kuliko kushiriki huku watu wakipata vilema kisha waendelee kuporwa ushindi. Bora watu wawe wachache ili hawa wanaopora ushindi wajue hawakubaliki kwa kiwango gani, huko mbeleni itatafutwa plan B. Kujazana vituoni huku dunia ikiona kisha wakaiba, dunia inajua wanakubalika. Wao kukaa madarakani sio shida, hata waliopindua nchi hukaa madarakani.
 
Hiyo kanuni kama itakuwepo inaweza kupingwa Mahakamani
 
Siku nchi ikipata Uhuru na Katiba mpya kanuni za Uchaguzi Mkuu ziwekwe katika Katiba, ili zisitungwe na watawala kwa maslahi ya chama tawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora arudi mkoloni mzungu aendelee kututawala kuliko kutawaliwa na mkoloni mweusi maana mpk roho zao nyeusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…