Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Katika Mgomo wa wafanyabiashara, kosa la Mwigulu Nchemba ni lipi?

Shida ya hii serikali ni kupenda cheap politics ndio kinacho wa cost leo; kwa upande mwingine unaweza sema wanavuna walichopanda.

Suala la kulipa kodi sio jepesi na watanzania awajazoea kulipishwa kwa sheria zote zilizopo au kudaiwa na kuchunguzwa kwa mujibu wa sheria.

Magufuli aliwaanzishia hiyo safari sema yeye ali-target wakepwa kodi wakubwa kwa sana sio hawa vidagaa, either way huko chini nako wakaelewa kodi sio swala la mzaha.

Sasa inachukua muda watu kubadili na kuzoea utaratibu mpya wa kulipa kodi. Wao wameingia na porojo zao za kukumbatia mafisadi, kutunga uongo ulikuwa utaratibu mmbovu ili kumchafua mtangulizi wao na kuondoa team waliyoikuta TRA na kupotosha umma ule sio utaratibu wa kudaiana.

Madhara yake ndio wanayaona leo, 90% ya malalamiko ni purely lack of understanding kwenye maswala ya kodi, pamoja na elimu ya biashara kwa ujumla.

Watu wanatafuta mitaji ana akili ya kununua mzigo kwa bei A na kuuza kwa bei B ya faida. Costs zake ni mishahara, kodi na kodi ya pango na haulage labda.

Akianza biashara akikutana na business rates za halmashauri, taka, insurance na mambo mengine ambayo alikuwa hayajui kabla anabaki kushangaa na kudhani anaonewa wakati ni costs za kawaida tu.

Akiambiwa TRA inaweza kukufanyia inventory audit, ukikutwa unaongopa fines anashangaa wakati hiyo ni serious offence. Analetewa mzigo kiholela hana stakabadhi sahihi anashangaa wakati sheria inamtaka kuwa na evidence ambayo wanaweza trace mzigo ulipotoka ndio maana ya invoices kuwa na unique numbers.

Huko kwenye ma-lorry ndio kabisa watu wamechekewa kwa muda mrefu hiyo kodi ni ndogo mno kwa mtu magari zaidi ya mawili.

Issue za msingi ni usumbufu wa kila siku wanaopewa wafanyabiashara kwa kutembelewa na TRA, idadi ya tozo wanazokutana nazo halmashauri (nyingine ni za kufutwa) kutokuwa na one stop centre ya kulipia hizo tozo zenyewe tofauti na kuondoa ghasia ya kutembelewa na watu mbali mbali katika shughuli zao.

La mwisho ni import duty kwa sasa ni 25% hiyo ni kubwa sana kwa consumer goods inatakiwa isizidi 5% kwenye kuzidisha CIF kwa sababu kuna VAT juu ya 18% ambayo ni fair and can be claimed back.

Bila ya kusahau hoja za yule mtu wa Zanzibar bidhaa za personal use watu wanazopelekea ndugu au kwa matumizi binafsi sio kutoka visiwani tu bali ata nje ya nchi hazistahili kutozwa kodi import duty huo ni ushamba. Begi la nguo lisilozidi kila kilo 100 common sense that’s for personal use au kilo tano ya sukari kutoka Zanzibar.

Mengine ni uelewa mdogo tu wa biashara na kujipanga; Mwigulu ni bozzo hilo halina ubishi ila kwenye hili shida ni uelewa.
 
Hizi ndio sababu Magufuli anawapa watu ukweli uliopo, sio kupotosha potosha haya ndio madhara.

Wewe kama ni retailer wa finished products halafu utaki kusajiliwa kulipa VAT maana yake unaigharamie kwa sababu uwezi dai uliyolipia mzigo.

Mtu mwenye maslahi ya kutosajiliwa VAT ni mtu anaeuza huduma, lakini muuza bidhaa kukataa inakula kwako.

Kuna capital gain taxes ipo kesheria sasa ukitupiwa hiyo ukiuza fixed asset za biashara usishangae siku jamaa wakikudai chako; awafanyi tu hayo kwa sasa. Au wewe unauza magari unatakiwa ulipe income tax huna ata TIN ila by law unatakiwa usajiliwa kulipa kodi, bado wapangishaji na wengineo wengi. Kodi sio mchezo nchi za wenzetu.
 
Wakuu Salam,

Naomba nitangaze maslah, mimi ni mfanyabiashara, nipo Kariakoo, nje ya kariakoo na mkoa wa Pwani.

Malalamiko yetu wafanyabiashara mengi ni justifiable.. lakini hili la kumlaumu Mwigulu Nchemba bila supporting evidence is ungrounded.

Kuna watu wanatumia udhaifu wa migogoro ya sheria zilizopo kumgandamiza bila sababu.

Mfano.

1. Hoja ya fine ya kutokutoa EFD recept sio ya leo, na hii ilipingwa sana na aliekuwa mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka, nilishangaa saana yale mapendekezo, kama kawaida ya bunge letu.. papatu papatu hoja ikapita ikawa sheria, Kipindi hicho Mwigulu ni Wazir wa mambo ya ndani.

2. Hoja ya ushuru wa malori, Ndugu Chuki anaweza kuwa ana issues personal na Mwigulu na siwez kuwaingilia , ila kodi ya 2.7M sio kubwa kama anavyodai, kumbuka kubeba tonneau 10 had mwanza ni zaid ya 1.5M na hiyo ni non negotiable.... kutaka hiyo gharama iingizwe kwenye diesel ni ku shift tax burden to non beneficiaries, ambayo ni unfair taxing.

3. Hoja za registration of warehouse sio kitu kipya na wengi tumesajili nikiwemo, hoja za umiliki ni jambo jingine, labda tuseme issue ya With holding Tax ndio haijakaa Sawa, lakini kulalamika kwamba tusisajili sio Sawa kabisa.
Kwenye ethical business ni lazima usajili store na ulipie usimamiz wake, ikiwa na vigezo vyote.... hii ni excuse ambayo kumlaumu nayo Mwigulu ni ku choose easy victim.

4. Hoja za task force zilikuwepo toka kipind cha mwendazake... kwamba tunasumbuliwa hili ni kweli na ni sualq la kuweka utaratibu tu wa namna ya ku control, ambayo sikuona sabab ya kumzodoa mwamba vile.

5.Utitiri wa kodi kwenye biashara na mamlaka nyingi zinazosimamia jambo moja ni suala la kurith na Mwigulu sidhan kama ni wa kulaumiwa 100% , issue hapo ni CCM kuweka na kuunda hizi taasisi kutafutia washkaj wao ulaji.
Kuna kila sabab ya kuunganisha taasisi nyingi sana ili kuondoa usumbufu.

Ni hayo tu... tumuhukumu Mwigulu kwa mengine lakini sio moja kwa moja kwa baadhi ya sheria ambazo amezikuta.
Mwamba umeongea ndivyo sana, wanaokupinga ni either sukuma gang au ni wakwepa kodi full stop
 
Kwanza hawezi badili sheria ya Bunge,hili amewahi lizungumza mara nyingi tuu,kama jambo Hilo au sheria ilipitishwa na Ngazi zote haliwi la Mwigulu Bali la Serikali yote Ili libadiloke ni lazima Rais aingilie kati..

Ujue watu wengi hamjielewinna sijui nyie mnafanya kazi zipi, Mwigulu hatungia sheria Wala kupendekeza sheria ,hayo yote hufanywa na Wataalamu wa Fedha, uchumi na Kodi baada ya kujiridhisha..

Waziri anaenda ku act kama.msemaji na mjenga hoja ya hicho kilichopendekwzwa na anaanzia kwenye Baraza la Mawaziri ndio linaenda Bungeni,wote hao wakipitisha na Rais kusaini haliwi suala la Mwigulu,sheria inaipa Wizara mamlaka ya kutunguia kanuni na miongozo kwenye sheria mama.

Kwa hiyo Mwigulu hawezi kulaumiwa kwenye sheria za Bunge,mara ooh utitiri wa Kodi Sasa hizo ni Kodi za Mwigulu au za Serikali? 🤣🤣🤣
Wewe na fortilo nimewafuatilia michango yenu nimegundua yafuatayo;

1. Id mbili ni mtu mmoja.
2. Hamjawasikiliza vizuri wafanyabiashara.
3. Umejikita kumtetea mwigulu bila kuonesha hao wafanyabiashara walipaswa kufanya nini?
4. Wewe siyo mfanyabiashara.

5. Hili ndilo haswa lililo nifanya nichangie mada ni kwamba hata wewe haujui kazi ya waziri.

Siyo kweli kwamba waziri ni msikilizaji tu wa utngaji wa sheria hapa unadanganya maksudi ili Mwigulu asionekane na kosa ktk sakata hili.

Moja ya kazi muhimu Sana na inayotarajiwa kwa waziri yeyote ni kutoa ushauri wa kitaalam ktk sekta husika, haijalishi yeye ni mtaalam au laa atajua atumie nini ili kutumiza wajibu huo. Ktk wajibu huu hapa ndipo palipo na makosa ya Mwigulu kama ifuatavyo;

(a) Yeye kama waziri alikuwa na uwezo wote wa kushauri juu ya sheria mbovu za kikodi ambazo wewe unakiri kuwa hazikuanza leo wala jana. Fursa ya ushauri ipo ktk baraza, bunge, na kwa Rais mwenyewe.

(b) Huyu Mwigulu amekaa na wafanyabiashara na kupata changamoto zao wala hakujali (rejea nukuu za wafanyabiashara).

(c) Waziri wa fedha anayehusika na uchumi hakupaswa hata kidogo kupuuzia mvutano wa wafanyabiashara na TRA hata kama sheria zilikwisha pitishwa eti tu suala hilo linamhusu mkuu wa mkoa, kea waziri wa namna hii hakika hafai ni sawa na yule wa biashara. Yaani mgogoro uko ndani mwako unakaa eti mkuu wa mkoa asiye na wajibu huo aingilie Kati! Hapa Elimu haijatumika!

(d) Pamoja na makosa mengine pia kauli ambazo Mwigulu amekuwa akizitoa juu ya kudhadadia sheria zinazokandamiza nayo imeibua hisia hasi ktk mgogoro huu ikiwa ni pamoja na kauli ya waziri wa viwanda. Na hii imekuwa tabia mbaya kwa baadhi ya mawaziri.
 
Hizi ndio sababu Magufuli anawapa watu ukweli uliopo, sio kupotosha potosha haya ndio madhara.

Wewe kama ni retailer wa finished products halafu utaki kusajiliwa kulipa VAT maana yake unaigharamie kwa sababu uwezi dai uliyolipia mzigo.

Mtu mwenye maslahi ya kutosajiliwa VAT ni mtu anaeuza huduma, lakini muuza bidhaa kukataa inakula kwako.

Kuna capital gain taxes ipo kesheria sasa ukitupiwa hiyo ukiuza fixed asset za biashara usishangae siku jamaa wakikudai chako; awafanyi tu hayo kwa sasa. Au wewe unauza magari unatakiwa ulipe income tax huna ata TIN ila by law unatakiwa usajiliwa kulipa kodi, bado wapangishaji na wengineo wengi. Kodi sio mchezo nchi za wenzetu.
Tumekwambia VAT ianzie billion 1 sio million 100
 
Wewe na fortilo nimewafuatilia michango yenu nimegundua yafuatayo;

1. Id mbili ni mtu mmoja.
2. Hamjawasikiliza vizuri wafanyabiashara.
3. Umejikita kumtetea mwigulu bila kuonesha hao wafanyabiashara walipaswa kufanya nini?
4. Wewe siyo mfanyabiashara.

5. Hili ndilo haswa lililo nifanya nichangie mada ni kwamba hata wewe haujui kazi ya waziri.

Siyo kweli kwamba waziri ni msikilizaji tu wa utngaji wa sheria hapa unadanganya maksudi ili Mwigulu asionekane na kosa ktk sakata hili.

Moja ya kazi muhimu Sana na inayotarajiwa kwa waziri yeyote ni kutoa ushauri wa kitaalam ktk sekta husika, haijalishi yeye ni mtaalam au laa atajua atumie nini ili kutumiza wajibu huo. Ktk wajibu huu hapa ndipo palipo na makosa ya Mwigulu kama ifuatavyo;

(a) Yeye kama waziri alikuwa na uwezo wote wa kushauri juu ya sheria mbovu za kikodi ambazo wewe unakiri kuwa hazikuanza leo wala jana. Fursa ya ushauri ipo ktk baraza, bunge, na kwa Rais mwenyewe.

(b) Huyu Mwigulu amekaa na wafanyabiashara na kupata changamoto zao wala hakujali (rejea nukuu za wafanyabiashara).

(c) Waziri wa fedha anayehusika na uchumi hakupaswa hata kidogo kupuuzia mvutano wa wafanyabiashara na TRA hata kama sheria zilikwisha pitishwa eti tu suala hilo linamhusu mkuu wa mkoa, kea waziri wa namna hii hakika hafai ni sawa na yule wa biashara. Yaani mgogoro uko ndani mwako unakaa eti mkuu wa mkoa asiye na wajibu huo aingilie Kati! Hapa Elimu haijatumika!

(d) Pamoja na makosa mengine pia kauli ambazo Mwigulu amekuwa akizitoa juu ya kudhadadia sheria zinazokandamiza nayo imeibua hisia hasi ktk mgogoro huu ikiwa ni pamoja na kauli ya waziri wa viwanda. Na hii imekuwa tabia mbaya kwa baadhi ya mawaziri.
Mkuu Mbogi heshima kwako.

Kwanza nikanushe kwamba hizi ID mbili ni mtu mmoja, labda ni kufanana mitazamo kinakufanya ufikiri hivyo, na huwa linatokea.

Lengo la uzi huu haikuwa kumtetea ndugu Mwigulu, lakini kuonyesha namna gani anahukumiwa kwa hisia zaidi kuliko uhalisia.
Kama umefuatilia mjadala vizur,

mkuu Mayor Quimby amejibu na maelezo yake mazuri sana kuhusiana na hili Sakata, hasa upande wa matokeo ya uelewa mdogo na wanasiasa wetu kupenda siasa nyepesi, lakini ziaid ukilinganisha na utayar wa wananchi wengi kwenye mazoea ya kulipa Kodi .
Hili la Mwigulu kuwa na kiburi na jeuri mara nyingine ndio matokeo yake anabebeshwa lawama hata kwa mambo ambayo angeweza toa ahadi ya kuyafanyia kazi.

Kuhusu wazir wa Biashara sijamzungumzia kabisa kwakuwa sijawah ona umuhim wake kabisa hasa ukilinganisha na majibu aliyotoa bungeni.

Suala la yeye kukaa na wafanyabiashara na kupuzia changamoto linaweza kuwepo, lakin malalamiko mengi yapo juu sana ya uwezo wake, na hizi sheria kusema ukwel ni zakupitiwa upya kabisa .

Kwahiyo mimi msimamo wangu ni kwamba Mwigulu hajahukumiwa kwa haki, kama utaangalia kwa undani hoja za wafanyabiashara.

Ahsante.
 
Pumbavu moja anaona shemeji yake sijui ni mjomba wake anarudi kulala nyumbani akiwa hajamkamilishia ahadi zake[emoji2958][emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959]

Kafie mbele na upumbavu wako!

Hayo yanayopigiwa kelele na wafanyabiashara tanzania nzima ndio yanayo sababisha mfumuko wa bei, kuzorotesha biashara na kudhohofisha uchumi, ambapo wafanyabiashara wengi wanashindwa kulipa kodi, inafika mahala hata hizo rushwa wanashindwa, wanafilisika, biashara zinakufa, serikali inakosa ubunifu wa kukusanya kodi inabidi hao walio bakia ndio waongezewe kodi za kijambazi ili kufidia pengo la waliofilisika, pumbavu na nusu
 
Mkuu chuki sio nzur
Vitu vingi vimeanza zamani.....
Ila Kwa hiyo Sheria mpya ya Kila mtu akakomboe mzigo wake mwenyewe hiyo unsionaje?
Sijui ndo consolidation....
SI Iko chini ya mwigulu au?
 
Huwezi kuwa mfanyabiashara ukaja kumtetea Mwigulu..
Mfumo WA Kodi WA kukadiria unaotoa mwanya Kwa watu wa TRA sio fair..
Mtu anakdiriwa Kodi milioni 350 wakati Kenya Kodi milioni 45 Kwa kontena Hilo Hilo...yote hayo ni policy..na usimamizi na Mwigulu ndo mhusika wa kubadilisha vyote...na kashauriwa kagoma ....

Wewe labda kakutuma uje umsafishe

Watu wanashushia contena Mombasa wanaleta mzigo kidogo kidogo
 
Mwiguluw anapitia comment moja baada ya nyingine [emoji1787][emoji1787]
 
Tumekwambia VAT ianzie billion 1 sio million 100
Tofauti ya unafuu unaitoa wapi hapo

Tuchukulie bidhaa ambayo profit margin 20%.

Umenunua bidhaa ambayo unit net cost ni 15000 ujasajiliwa VAT. Utauza kwa 15000 x 120% = 18000, faida yako 3000

Aliesajiliwa kwanza atatoa VAT ya kununulia (15000 x 100)/118 = 2288 anaenda wadai TRA.
Gross price ya bidhaa 15000-2288 = 12712
Faida 12712 x 120% = 15255

Faida yake hapo 15255 - 12712 = 2543

Hiyo faida yake hapo 2543 plus VAT return 2288 jumla 4831; ambayo ni zaidi ya 3000 ya mtu ambae ajasajiliwa

Bei atakoyouza kwa mteja 15255 x 118%= 18001 mmpeshina kwa shillingi moja na wewe ambae ujasajiliwa kutoza VAT

Na TRA wapo happy kwa sababu kawalipa VAT ya 18001 - 15255 = 2746; wakati wao wamemrudishia 2288 ongezeko la thamani kwao 2746 - 2288 = 458

Usually mtu anaelipa VAT ana maslahi zaidi kama ni trader kuliko asiesajiliwa; yeye hapo anaweza kuweka ata profit margin ya 15% akawa rahisi kushinda wewe kwenye bei na faida.

Kama unauza huduma badala ya finished goods, na wewe ndio unaenza kutoza VAT hapo sasa kuna maslahi ya kutotoka kujiunga; ila kwa trader una kila sababu ya kujiunga ata voluntary kama ujafikisha threshold. Ni kuto kuelewa tu.
 
Mkuu Mbogi heshima kwako.

Kwanza nikanushe kwamba hizi ID mbili ni mtu mmoja, labda ni kufanana mitazamo kinakufanya ufikiri hivyo, na huwa linatokea.

Lengo la uzi huu haikuwa kumtetea ndugu Mwigulu, lakini kuonyesha namna gani anahukumiwa kwa hisia zaidi kuliko uhalisia.
Kama umefuatilia mjadala vizur,

mkuu Mayor Quimby amejibu na maelezo yake mazuri sana kuhusiana na hili Sakata, hasa upande wa matokeo ya uelewa mdogo na wanasiasa wetu kupenda siasa nyepesi, lakini ziaid ukilinganisha na utayar wa wananchi wengi kwenye mazoea ya kulipa Kodi .
Hili la Mwigulu kuwa na kiburi na jeuri mara nyingine ndio matokeo yake anabebeshwa lawama hata kwa mambo ambayo angeweza toa ahadi ya kuyafanyia kazi.

Kuhusu wazir wa Biashara sijamzungumzia kabisa kwakuwa sijawah ona umuhim wake kabisa hasa ukilinganisha na majibu aliyotoa bungeni.

Suala la yeye kukaa na wafanyabiashara na kupuzia changamoto linaweza kuwepo, lakin malalamiko mengi yapo juu sana ya uwezo wake, na hizi sheria kusema ukwel ni zakupitiwa upya kabisa .

Kwahiyo mimi msimamo wangu ni kwamba Mwigulu hajahukumiwa kwa haki, kama utaangalia kwa undani hoja za wafanyabiashara.

Ahsante.
Nami nikushukuru kwa kumsoma vizuri Quambly na amekazia vizuri ila kwa neno kali moja lenye maana juu ya uhusika wa Mh Mwigulu.

Ktk maelezo yako mtazamo wako ni kuwa suala hili lisiendeshwe kisiasa na kwamba uelewa wa sheria, kodi na elimu Ndiyo tatizo.

Hapa ndipo ninapokufafanulia kwamba sera za kisekta zisipoeleweka kwa watekelezaji na walaji waziri anakuwa amefeli.

Ipo aya haujaigusia kuijibu nairudia, kama waziri aligundua kuwa sheria zilikuwa na ama kutokueleweka, au mbovu hakupaswa kuacha hadi kufikia kuwa na mgogoro maana ushahidi wa kimazingira unaonyesha dhahiri kuwa waziri alikuwa anajua kukua kwa mgogoro huu.

Kama nilivyosema awali moja ya kazi namba moja ya waziri ni kuwa jicho la kubalini kasoro za kisera na kisheria ktk sekta yake na kutoa ushauri wa upatikanaji wa suluhu kabla ya tahatuki na zaidi kwa lengo la kuboresha na kurahisisha maisha ya Wananchi.

Je ktk hili Mwigulu alishiriki vipi? Maana sekta yake pia inaguswa.

Kuhusu elimu, nani alipaswa kuandaa elimu ya kodi hizo ili iwe na tija kwa pande zote?
 
Mkuu Mbogi heshima kwako.

Kwanza nikanushe kwamba hizi ID mbili ni mtu mmoja, labda ni kufanana mitazamo kinakufanya ufikiri hivyo, na huwa linatokea.

Lengo la uzi huu haikuwa kumtetea ndugu Mwigulu, lakini kuonyesha namna gani anahukumiwa kwa hisia zaidi kuliko uhalisia.
Kama umefuatilia mjadala vizur,

mkuu Mayor Quimby amejibu na maelezo yake mazuri sana kuhusiana na hili Sakata, hasa upande wa matokeo ya uelewa mdogo na wanasiasa wetu kupenda siasa nyepesi, lakini ziaid ukilinganisha na utayar wa wananchi wengi kwenye mazoea ya kulipa Kodi .
Hili la Mwigulu kuwa na kiburi na jeuri mara nyingine ndio matokeo yake anabebeshwa lawama hata kwa mambo ambayo angeweza toa ahadi ya kuyafanyia kazi.

Kuhusu wazir wa Biashara sijamzungumzia kabisa kwakuwa sijawah ona umuhim wake kabisa hasa ukilinganisha na majibu aliyotoa bungeni.

Suala la yeye kukaa na wafanyabiashara na kupuzia changamoto linaweza kuwepo, lakin malalamiko mengi yapo juu sana ya uwezo wake, na hizi sheria kusema ukwel ni zakupitiwa upya kabisa .

Kwahiyo mimi msimamo wangu ni kwamba Mwigulu hajahukumiwa kwa haki, kama utaangalia kwa undani hoja za wafanyabiashara.

Ahsante.
Hasira za Mwigulu ni lugha yake mbovu na tozo za miamala watu wamezitolea hapo. But it has nothing na malalamiko yao ya kodi huko ni purely lack of their understanding.
 
Mkuu haya mambo nakuelewa sana, hoja yangu hapa ni kwamba Mwigulu amekosea nini?
Tumelia na haya masheria mabovu kwa miaka hata kabla ya Mwigulu, leo nashangqq kishabiki kabisa anabebeshwa zigo lote.
Jua kuwa TRA iko chini ya wizara ya fedha, TRA wanapoboronga na waziri akashindwa kuchukua hatua lazima alaumiwe, pili ana majibu ya hovyo, anatakiwa kuheshimu taasisi mbalimbali anazofanya nazo kazi kitenda cha kukataa kuwasikiliza viongozi wafanya wa wafanyabiashara namna ya kuongeza au kupunguza kodi ni kosa kubwa sana hastahili kuwepo hapo wizarani.Awe na adabu iweje mbunge mwenzake amwite mganga wa kienyeji hiyo si ni dharau kubwa.
 
Wakuu Salam,

Naomba nitangaze maslah, mimi ni mfanyabiashara, nipo Kariakoo, nje ya kariakoo na mkoa wa Pwani.

Malalamiko yetu wafanyabiashara mengi ni justifiable.. lakini hili la kumlaumu Mwigulu Nchemba bila supporting evidence is ungrounded.

Kuna watu wanatumia udhaifu wa migogoro ya sheria zilizopo kumgandamiza bila sababu.

Mfano.

1. Hoja ya fine ya kutokutoa EFD recept sio ya leo, na hii ilipingwa sana na aliekuwa mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka, nilishangaa saana yale mapendekezo, kama kawaida ya bunge letu.. papatu papatu hoja ikapita ikawa sheria, Kipindi hicho Mwigulu ni Wazir wa mambo ya ndani.

2. Hoja ya ushuru wa malori, Ndugu Chuki anaweza kuwa ana issues personal na Mwigulu na siwez kuwaingilia , ila kodi ya 2.7M sio kubwa kama anavyodai, kumbuka kubeba tonneau 10 had mwanza ni zaid ya 1.5M na hiyo ni non negotiable.... kutaka hiyo gharama iingizwe kwenye diesel ni ku shift tax burden to non beneficiaries, ambayo ni unfair taxing.

3. Hoja za registration of warehouse sio kitu kipya na wengi tumesajili nikiwemo, hoja za umiliki ni jambo jingine, labda tuseme issue ya With holding Tax ndio haijakaa Sawa, lakini kulalamika kwamba tusisajili sio Sawa kabisa.
Kwenye ethical business ni lazima usajili store na ulipie usimamiz wake, ikiwa na vigezo vyote.... hii ni excuse ambayo kumlaumu nayo Mwigulu ni ku choose easy victim.

4. Hoja za task force zilikuwepo toka kipind cha mwendazake... kwamba tunasumbuliwa hili ni kweli na ni sualq la kuweka utaratibu tu wa namna ya ku control, ambayo sikuona sabab ya kumzodoa mwamba vile.

5.Utitiri wa kodi kwenye biashara na mamlaka nyingi zinazosimamia jambo moja ni suala la kurith na Mwigulu sidhan kama ni wa kulaumiwa 100% , issue hapo ni CCM kuweka na kuunda hizi taasisi kutafutia washkaj wao ulaji.
Kuna kila sabab ya kuunganisha taasisi nyingi sana ili kuondoa usumbufu.

Ni hayo tu... tumuhukumu Mwigulu kwa mengine lakini sio moja kwa moja kwa baadhi ya sheria ambazo amezikuta.
Bro kuna watanzania zaidi ya milioni 60. Kama wafanyabiashara wamemkataa Mwigulu tuna watanzania idadi hiyo hiyo wanaoweza jaza nafasi yake. Mwigulu sio Mungu mmoja hadi atetewe hivyo.
 
Naomba nitangaze maslah, mimi ni mfanyabiashara, nipo Kariakoo, nje ya kariakoo na mkoa wa Pwani.
Mkuu, nchi hii siku hizi hutakiwi kutumia akili ili mambo yako yaende sawa.

Wewe ni mtu mkweli, na kuwa mkweli nchi hii siku hizi ni dhambi.

Sasa nijibu swali lako:
Kosa lake ni kuwasuta wabunge vilaza, wenye Ph.D. za mitaani wasiotambua hizo Ph.D. zinazotolewa vyuoni.

Kama wewe ulivyo mkweli, yeye pia alikuwa mkweli kuhusu jambo hilo, ambalo wabunge hawakutaka kulisikia, likichagizwa na "uganga wa kienyeji".
Mwigulu akawa mwenye majivuno tokea wakati huo.

Sijawahi kumtambua Mwigulu kuwa kiongozi mwenye 'impact' ninayeweza kumuunga mkono tokea zile enzi akiwahenyesha CHADEMA. akiwa Mwenezi wa CCM.
Uvaaji wake wa maskafu haujawahi kunikoga chochote kuhusu uzalendo wake kwa nchi hii.

Lakini kwa haya yanayotokea sasa hivi, na yeye ndiye kuwa kinara wa lawama, inalazimu nianze kumtazama upya kabisa, kama kuna uwezekano wake kuwa na vimelea hata kidogo vya uzalendo kwa nchi hii.

Baada ya kusema hayo yote, nirudi nyuma kidogo, kwamba Mwigulu kama waziri mwenye mamlaka juu ya TRA, hawezi kuepuka ubovu unaoonekana kufanyika huko.
Sheria mbovu zinazoruhusu mianya ya rushwa, ni wajibu wake kuzishughulikia kuondoa ubovu huo.
Kwa hiyo hawezi kuepuka lawama, kama ilivyo, kwa nyinyi wafanya biashara, pamoja na kelele zenu nyingi, inajulikana ndani yenu kuna takataka nyingi sana zinazowaharibia sura zenu kwa wananchi.
 
Bro kuna watanzania zaidi ya milioni 60. Kama wafanyabiashara wamemkataa Mwigulu tuna watanzania idadi hiyo hiyo wanaoweza jaza nafasi yake. Mwigulu sio Mungu mmoja hadi atetewe hivyo.
Ni wazi, wewe unalako jambo. Inawezekana ni mshindani wa Mwigulu, unasubiri tu mkono udondoke, ukitegemea utanufaika wewe.
Hao waTanzania milioni 60, na wewe unajihesabu kuwa mmojawapo anayeweza kuchukua nafasi ya Mwigulu?
Hivi vichekesho uwe unamsimulia mkeo tu, kwa huku vinakuonyesha usivyokuwa na uwezo wa kazi hiyo ya uchekeshaji.
 
Back
Top Bottom