MO alishatia Bilioni 20 kitambo na bado anaendelea kugharamika kwa mapenzi ya timu, ni wajinga pekee wanahoji nami nawaelimisha kuwatoa ujinga

Mambo ni kimya kimya hapa bongo, Umewahi kuuona hata mkataba original wa jezi wa Simba na Vunja bei ???
Alafu mumwambie aache tabia ya kujifanya kila mwaka anapata hasara, hasara awe anapata yeye tu GSM mbona hana hisa Yanga na halii kupata hasara.
 
Alafu mumwambie aache tabia ya kujifanya kila mwaka anapata hasara, hasara awe anapata yeye tu GSM mbona hana hisa Yanga na halii kupata hasara.
GSM ni waarabu mkimya kama Bakhresa
 
20bn plus za wanachama ziko kwenye account gani . Tuache kupiga kelele za Mo peke yake. Leteni balance ya hela za wanachama period.
Dah kumbe wewe ni kilaza hivi🙌🏽🙌🏽😩😩😩
 
Kakutuma mjinga wewe ama? Hivi mnawajua wahindi au mnawaskia. Aondoke bana. Hajaweka hiyo pesa hakuna ushahidi wa kibenki. Mjinga mmoja wewe. Anawahadaa na vihela vya hapa na pale wakati ni timu yenye potential kubwa sana. Hamna akili.
Upewe ushahidi wewe ni nani katika Klabu ya Simba?
 
Ndiyo kusema wakati hayo yote yanafanyika timu haikuwa na mapato yake nje ya udhamini wa Mwekezaji?
Yaani mapato yaliyotokana na gate collection, fedha za CAF, wadhamini kama Sportpesa, Mbet, Azam Media, nk!!!
Kipindi mnatembeza bakuli hizo gate collection, sportpesa hazikuwepo?

Hivi unajua gharama za kuendesha timu zinaweza kuwa covered na vyanzo vidogo vya pesa kama hiyo mifano yako?

Saizi mmepata mwekezaji lakini bajeti yenu ya mwaka imekuja na pancha kuwa mmepata hasara.

Na hapo mwekezaji yupo.

Haya niambie bila mwekezaji hali ingekuwaje?
.
 
Rejea interviews zake anazodai eti "ameinunua simba sc"
 
Mwekezaji mwingine sio issue, issue jee ni mwanamichezo? Jee ana mapenzi ya dhati kwa Simba?
 
Pesa ilitakiwa iwekwe Bank itumike kununua Bonds kama mtaji.

ELEWA au kasome MOU .

Pesa(Mtaji) haikuwa ya matumizi hiyo anayoidai
 
Kupitia haya maelezo yako, hivyo vyanzo vya mapato havina tija, na ndiyo maana mwekezaji wenu anadai mpaka hela aliyonunulia mchicha siyo!
 
Well said. Hivi km kuna watu wanafikiria matangazo kwenye jezi na udhamini Wa Azam, Mbet au Sportpesa vinaweza kuendesha timu kwann Yanga haikutoka kwenye dhiki hadi alipoingia GSM? Au bado anafanya nn pale Yanga kama mapato hayo yanatosha? Watu hawajui wanachokiongea. Akitoka Mo ndo watajua walikuwa hawajui. Biashara ya uwekezaji katika hizi timu za Nchi km Tanzania bado hazitoi faida yoyote ya kuweza kuwavutia wawekezaji. Hawa tulio nao/ tuliye naye si muwekezaji hasa, bali ni kama mfadhili tu mwenye mapenzi na timu. Ht Mo mwenyewe najua anajua kuwa hatarajii faida yoyote ya kifedha kutokana na huo uwekezaji wake any time sooneri. Ndo mana huku kwetu hatujawekewa ile Sheria ya FIFA ya financial fair play ambayo inavilazimisha vilabu kutumia kile tu kinachopata kutokana na biashara ya mpira. Sisi bado tunajiendesha kwa ufadhili wa matajiri wenye fedha, wawe wamiliki au wapenzi Wa vilabu hivyo.
Kumtoa Mo mnaweza kuona ni ushindi lkn huyo mnayemfikiria atawatoa hapo mlipokwama, hawezi kuwa Kigwangwala wala huyo CPA Massoud. Hawana uwezo huo.
 
Unaongea Pumba tupu mzee.

Mo angetaka kuwa Mfadhili angeendelea kuwa Mfadhili tu.

Dispute iliyopo ni Ulaghai wa ununuzi wa Hisa mkuu. Kwa sababu shida ya simba ni uendeshaji so ndo iwe sababu ya Mo kujimegea sehemu ya klabu?

Haya anamiliki asilimia 49 kijanja, kesho bahat mbaya hayupo au Mungu kamchukua means mrithi wake aendelee kumiliki klabu? Na kama huyu mrithi atakuwa hana nia nzuri kama Mo itakuwaje?

Shida ya matumizi si kigezo cha kuimega na kumiliki klabu. Tumieni akili basi , fikirieni The Bigger picture , msiwaze hapa tu miaka 5 .
 
Haya yote hayahalalishi UTAPELI anaotaka kuufanya MO ili amiliki Simba au sehemu ya Simba.
 
Mkuu agreement 20B siyo ya matumizi bali ni mtaji ukawekwe Bank na ununue Bonds.
 
Unadhani wachezaji na makocha ghali walikuwa wanatua simba kama zabibu chini ya mpera ?
Unajua 20B katika MOU zilitakiwa kununua wachwzaji au matumizi??.

Wengi hamuelewi na ndo maana Dewji anawahadaa.

Pesa ktk MOU ilitakiwa iwekwe Bank kama mtaji na inunue Bonds. Siyo kusajilia

Kwa nini Bonds?. Ndo hapo mnatakiwa muwaachie watu wa Hisa sasa. Na Hoya hoya mnazoleta
 
kusajili wachezaji na mishahara ya wafanyakazi pamoja na wachezaji, usafiri wa ndani na nje ya nchi,malazi pamoja gharama za kuvunja mikataba ya wachezaji na makocha,
Hata GSM anafanya hivyo. Je umesikia anamiliki Yanga au ana Hisa Yanga?

Au atasema hizo gharama ni sehemu ya manunuzi ya klabu?

Tumieni akili basi aisee.

Hivi mnaelewa mnachokibishia au ni Uzuzu tu?

Mo anamiliki timu kivipi?.. amenunua hisa lini?
 
Moto unawaka, hakikisheni mnasajili vinginevyo msimu ujao tutawaokota nafasi ya 5
 
Moto unawaka, hakikisheni mnasajili vinginevyo msimu ujao tutawaokota nafasi ya 5
Kwa huu mgogoro unaoendelea sina imani kama simba itafanya vzuri msimu ujao tena. ILA mbali ya yote hata kama mo ni tapeli au viongozi wanahujumu kwa timu zetu za kitanzania hazina uwezo wa kujiendesha zenyewe kwa mapato yake yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…